Safari ya kuchosha kutoka Musoma - Arusha

Msafiri93

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
421
296
Habari WanaJamvi Leo Napenda Kushare Nanyi kisa hiki cha safari Fupi iliyochukua muda mreeefu na kuchosha Miili ya Wasafiri.

Ilikua siku ya Tarehe 13 mwezi Wa 12 mwaka 2014 Kutokea Musoma mkoani Mara kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro katika basi la Kampuni ya A.M the Dream liner

Nakumbuka wakati huo ulikua ni msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka Na mvua kubwa. Na kutokana na Njia inayotumika haikuwa na lami na inakatisha katika Mbuga za Serengeti na NgoroNgoro hivyo kupelekea kusiwe na luxury bus inayoweza kukatisha anga hizo Na kufanya bus zote zinazopita maeneo hayo kuwa Ni Scania na Man pekee

Safari hii ilianza asubuhi na mapema mida ya saa12alfajiri tuling'atuka kutoka mitaa ya musoma mjini na kupitia abiria kadhaa stendi kuu Bweri., Na safari kuanza Rasmi kupita vijiji kadhaa.

Mwanzoni safari ilikua nzuri Tukishangaa vijiji na Mazingira ambayo Mimi binafsi nilikua mgeni nayo hivyo nilivutiwa sana na mazingira Yale kama Bunda, Nata , Isenye yalikua mazingira flan ya kupendeza japo yako mbali.

Safari ilianza majanga tulipokaribia Mugumu Serengeti kumbuka ulikuwa ni msimu wa mvua na barabara inakatisha mbugani haina lami na magari mazito kama basi yanapitapita hivyo kusababisha mashimo ambayo wakati wa mvua yanajaa maji na kusababisha usumbufu.

Njia imezibwa.
Kwa kuwa maeneo Yale ni karibu kabisa na mbuga hivyo tulianza kuona magari ya watalii na moja ya magari hayo lilinasa kwenye Matope na kuziba njia Na hapo ndo ukawa mwanzo Wa matatizo
Kwa mara ya kwanza kuona foleni pasipo Traffic Lights, wasafiri ambao safari yetu bado changa kabisa ilitubudi Tutoe msaada kuondoa gari lililonasa njiani ili kuacha nafasi ya kupita bus tuendelee na safari kwani tulifika maeneo Yale katika majira ya saa 3 asbh na kila mtu alikua na shauku ya kufika mapema aendako.
Tulifanikiwa Hatimae na safari ikaendelea lakini tulishapoteza kama masaa 2 pale kwa sababu kawaida ya wasafiri kupendeza hvyo hakuna aliyetaka kuchafuka kwa kuingia kwenye Tope lakini ilikua haina maana Tuishie pale hivyo ilibidi tujitoe japo Tuliwakuta askari wa mbugani lakini ilibidi Tungeze nguvu kufanikisha.

Safari Ikaendelea hatimae tukafika katika kituo cha kwanza Ikona Gate ambapo kwa utaratibu ni lazima wasafiri wanaotumia mabasi lazima wahesabiwe ili kuhakiki idadi yetu kabla hatujaruhusiwa kuingia Rasmi katika mbuga ya Serengeti na kujionea wanyama na mazingira ya kijani na Nyika za kuvutia
Ama kweli Tanzania ni sehemu Ya Eden jamani nilijisemea mwenyewe kimoyomoyo huku nikitabasam kwa kuona Twiga wengi tena kwa ukaribu kabisa wakijichanganya na Ngiri kadhaa.
Tulitembea kilomita kadhaa tukafika katika kituo cha pili kilichoitwa Seronela ambapo tayari ulifika mchana na hapo tulitakiwa kupata chakula cha mchana kabla ya kuendelea tena na Ngwe ya pili kumalizia safari yetu.

Tulikula na kunywa huku Tukijiselfisha na wenyeji wetu na mazingira mazuri na masafi ya mbugani Tena ilikua furaha sana kwa sababu Tulikuwa wengi mno kwenye lile bus na wengi wetu tulikua ni vijana Tulifurahia sana mazingira Yale kwani kwa nilivoona Mimi wengi wetu ilikua Mara yetu ya kwanza kupita mbugani tulitamani kama safari isiendelee tena lakini hatukujua Kama Bus lile lilisikia kilio chetu.

Baada ya kula, kunywa na kujiselfisha sana Hatimae muda Wa kuinza safari tena mchana ule ukawadia Tukajipakia tena kwa bus na mwendo ukaanza kwa furaha na kelele nyingi ndani ya bus Tukielezana sifa tofauti Tofauti za wanyama Tuliowaona. Tukiwa tumesahau yaliotupata asbh. Tukiwa bado na Tabasam la kuona wanyama na mandhari nzuri. Bado mvua ikitusindika kwa mbaali.....Bado Tukiwa tunaulizana muda na umbali uliobaki kumaliza safari yote haya yalifanya Tufarijike japo Tupo katika safari.

LaaHaulla!!!! Bus limesimama ghafla tena kwa kishindo kikubwa tena mvua ikiwa imechanganya na tumefika kwenye eneo LA nyika ambalo kwa mujibu Wa maelezo ya maafisa walituambia kuwa maeneo Yale ndio maskani kubwa ya simba tena ikifika mida ya jioni..Loooooh maafisa wanatuambia maneneo hayo ikiwa zimesalia dakika chache kufika saa 10jioni.
Kidogo mood ilikata sikutamani kuwa eneo lile tena kumbuka tena wakati huo mvua inanyesha baridi inapuliza kwelikweli.
Safari hii tena bus ilikataka difu na kusababisha kushindwa kuendelea na safari tena. na wale maafisa walitupa Yale maelezo wakidai kwamba tutafute sehemu mbadala ya kusubiri bus likitengenezwa au Tusishuke katika bus kwa kuwa tutahatarisha maisha yetu na lile eneo kumbuka ni Nyika tupu na eneo kubwa hakuna mti Wa kujificha hapo na maafisa walishaenda zao.

Safari ya Kuchosha.
Hapa ndipo tulipochoka kabisa kwani Dakika 40 baade walirudi wale maafisa walikuja na polisi pamoja askari Gemu kadhaa. Na ndipo ikaamriwa Turudi katika kile kituo cha pili ambacho ni Seronela wakidai kwamba ndio sehemu salama ya sisi kusubiri bus lile likitengenezwa na kwamba pale wabakie watu wachache tu wasioozidi 4 wengine wote turudi seronela na bus litakapotengemaa litatufuata tena seronela..Daaaah hakuna alieamini kinachoendelea kwa shingo upande Ilibidi kutii Amri kulinda maisha yako zikaletwa Cruiser za kutosha na sisi tukawa kama watalii tukiangaza huku na huko kwa nafasi zaidi kwani cruiser zile nyuma ziko wazi hivyo kufanya uweze kuangaza mbaaali zaaid kuliko ukiwa kwenye bus. Tukarudishwa tena Seronela pale ambapo tulitamani tusiondoke kidogo Tulikuta mabadiliko pia Nitumie fursa hii kuwashukuru wahudumu Wa Kambi ile ya seronela kwa ukarim waliotuonesha kwani tuliporudi tena Mara ya pili tulikuta Nyama choma ya kusaza tena wakatushauru ili kudhibit baridi mnapaswa kula sana Nyama na kuchangamsha mwili na wakati tunafika tena Seronela ilikuwa ni mida ya saa11 Nawashukuru tena wahudumu Wa Serengeti kwa kujali kwao watanzania Kwa mda huo mfupi tuliwezA kushiriki michezo kama Mpira Wa miguu mazoezi ya viungo.
Kumbuka ni wasafiri lakini ilibidi tubadilike kutokana na mazingira na wale maafisa walijitahidi kutuzoesha mazingira na kwakweli Tulitulia.
Baada ya Giza kuingia unajua Kule ni mbugani haifai kutembea usiku na kupiga kelele kwani baadhi ya wanyama hawapendi kelele hivyo tulikaa kwenye jengo moja kubwa jipya humo tukapata chakula cha kumalizia siku tukiendelea na stories mpaka majira ya SAA 7 usiku Bus liliporejea tena kutufata baada ya kutengemaa.

Usiku Wa manane bus linatengemaa toka jioni ya SAA 10 lilipo haribika na hii ni baada ya kuagiza difu nyingine kutoka Mwanza,. Kwa sababu ukilala mbugani lazima ulipie na sisi tulilipa 1500 ambayo ni ada ya MTU mmoja kupita Serengeti akiwa ndani bus hivyo hatulipa ada ya kulala pale na vile walivyotufanyia ni kwasababu tulikua wengi na hatukukusudia kulala pale hivyo ikatulazimu kwa kuwa bus liko sawa sasa na Tukaruhusiwa kuendelea na safari usiku huo

Njiani Mbugani usiku
Amini usiamini kuna wanyama hawalali kama Ngiri, punda miria, Fisi, Mbogo, na wengine Tuliendelea kuwaona wakirandaranda mbugani usiku.
Tumekwama tena
Wakati tuko pale seronela mvua iliendelea kunyesha lakini kwa kuwa tulikua pale kamp hatukuona madhara yake lakini tulipokua safarini tena usiku ndio tuliona madhara ya ile mvua kwani ilijaza mito na kuifanya icheue na kusababisha kuziba baadhi ya madaraja ya chini yaliopo Serengeti.
Tulikwama tena kwa sababu njia ya kupita ambayo ni daraja LA chini ilijaa maji na kuwa njia ya maji na kufanya Kingo znazoonesha mwsho wa daraja kutoonekana ikatulazimu tusubiri tena mvua ishe ili maji yapungue pale kwenye daraja na njia ionekane.
Tulisubiri eneo lile mpaka saa11alfajiri kutoka saa9 usiku ndipo maji yakaanza kupungua na Kingo za daraja zikaonekana lakini licha ya maji kupungua bado speed yake ilionekana kubwa.
Ilibidi sasa tumtafute mtu Wa kupima ile speed ya maji kama itafaa kwa bus kupita.kulikuwa na wanawake kwa bus hawakuamini kabisa mwendo Wa Yale maji na ndio walifosi itafutwe namna ya kuyapima kama tutapita salama.
Nitumie Tena nafasi hii kuwapongeza vijana Wa kimasai waliothubutu kuhatarisha maisha yao kwa sababu ya watu wengine kwani wao ndio waliopima speed ya maji kwa kwenda wenyewe kukanyaga sehemu tulizohisi ndipo Kingo zilipo tuliwafunga kamba kiunoni na walifanikisha kazi Hatimae tukapita salama na kusaidia pia magari mengine madogo ya watalii ambayo yalitukuta eneo hillo asubuhi.

Bado Mvua ilituandama na hatimae tukafika katika mpaka kati ya Serengeti na ngorongoro na hapo pia kupita ilituchuku mda kidogo kwani hapo Daraja liliondolewa kabisa na maji hivyo kufanya shimo ambalo hakuna gari ingeweza kupita lakini hapa tayari taarifa ziliwafika wakuu masaa machache baadae lililetwa daraja lingine na kupachikwa pale hatimae napo pia tukavuka salama japo muda ulishatutupa mkono kwani ilikuwa inaelekea saa tano asbuhi Siku ya pili.

Faraja yarejea.
Baada ya kuvuka mpaka na kuingia ngorongoro sasa kidogo tukaneemeka.kwa Mara ya kwanza namuona tembo katika mabonde ya ngorongoro tena kwa mbali nashangazwa na ukungu uliofunika creta kidogo tena natabasam natoa simu yangu nachukua kumbukumbu bus inasimama kidogo kupisha gari nyingine.
Barabara za ngorongoro ni za hatari kidogo umakini zaid unahitaji kupita zipo nyembamba zimetanda ukungu na zimezunguka mlima.
Tukiwa bado tunaishaa ngorongoro ghafla tena tunasikia sauti za watoto wa kimasai wamejichora usoni wakitutakia safari njema.

Hatimae.
Hatimae tunaitoka salama ngorongoro yenye creta na tunafika getini tunapewa nafasi tena ya kusafisha viatu vilivyo na tope kuosha mwili kwa wenye waToto na kujiweka tena sawa kwani sasa Tunaingia kwenye lami.
Watu wanashusha pumzi na kuangalia tulipotoka tunajiliwaza na Rosholoo kwani hatukutaka kusimama tena mpaka tufike tuendapo.

Yamungu mengi jioni ya tarehe 14mwezi Wa 12 mwaka 2014 Hatimae tunafanikiwa kuingia Arusha mjini salama kabisa lakini tukiwa wachovu wa mwili.
Asili ya watanzania ni ukarimu kama kawaida Tunashuka kwenye basi tunapeana pole kila mtu anachukua njia yake na Mimi kwa umakini Wa hali ya juu nakamata chombo nyingine sasa ni luxury kuelekea moshi mkoani Kilimanjaro katika ujenzi w taifa hili Tanzania.

Wito: kwa vijana wenzangu wasafiri ni vyema Kujiandaa kisaikoloji kwa lolote hii itasidia kurelax pale litakapotokea tatizo na kuweza kuwa msaada kama kijana .

Msafiri93
 
Mmmmmh! Uwongo mbaya kiukweli cjasoma huu uz ni mrf mnooo!!! Nilicho note ni safar ya kutoka musoma kwenda Kilimanjaro
 
Hiyo inaitwa adventure safari,wazungu wanaipenda sana,ulichoeleza kina ukweli kabisa maeneo uliyoyataja nimepita na mengine nimeishi nakumbuka maisha ya porini seronera yana raha yake japo siyo mazuri sana,nakumbuka robanda,foti koma ndabaka gate,nabi gate,mbuzi mawe,lobo,sopa lodge,oldupai godge,shifting sand,bunda,kirawira,seronera air strip,koglatende aisee we acha tu,Tanzanite bar - Mugumu
 
Wewe unapajua mkuu
 
Back
Top Bottom