Safari ya JK Monduli, Nape una maoni gani?

Mie binafsi nawapa pongezi Invisible pamoja na team yake nzima mods Paw na wenzake kwa kuweka sawa jukwaa letu pendwa la siasa kwa kukupambana na wahuni walikuwa wanachafua thread mpaka viongozi wa vyama wanakimbia JF...

Leo Nape naona kaamua kuja kujibu hoja za wana JF ndivyo inavyotakiwa...ushauri wa bure kwa Nape, JF ndio sehemu ya kukujenga wewe usikimbie humu njoo JF fungua thread karibisha maswali upambane kwa hoja ndio unakomaa kisiasa..
 
Last edited by a moderator:
There are currently 144 users browsing this thread........Nnauye Jr............ajabu naona umezubaa zubaa tu, umeganda au? hakika akili ndogo zinaongoza akili kubwa, amejisemea Mch. Msingwa......Nape kama Nyerere akirudi na kucharaza wanafiki wote, basi wewe utapata mboko nyingi sana

ili akamhadithie mkewe kuwa mwanaume hafai kuwa muongo.
 
Mie binafsi nawapa pongezi Invisible pamoja na team yake nzima mods Paw na wenzake kwa kuweka sawa jukwaa letu pendwa la siasa kwa kukupambana na wahuni walikuwa wanachafua thread mpaka viongozi wa vyama wanakimbia JF...

Leo Nape naona kaamua kuja kujibu hoja za wana JF ndivyo inavyotakiwa...ushauri wa bure kwa Nape, JF ndio sehemu ya kukujenga wewe usikimbie humu njoo JF fungua thread karibisha maswali upambane kwa hoja ndio unakomaa kisiasa..
mwambie aache unafiki ataliwa buzz
 
Mkuu Ritz;
Viongozi wa CCM hawana tabia ya kukimbia hoja; kiongozi aliyekimbia na kupotea kabisa ni yule katibu wa chama kile kinachojiita chama kikuu cha upinzani; ndiye amepotea kabisa haonekani kabisa kwa sababu anaukimbia ukweli; lakini ndiyo matatizo ya kutumia ulagahai na uwongo mwingi kwenye majukwaa ya siasa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu wangu chama ni kweli sijui kwa nini amekimbia JF siku hizi yupo sana facebook.
 
Last edited by a moderator:
Wale Wote Tunaishindia Vipande vya Mihogo Mibichi tuwe tunashtuana Ikitokea Miniso Kama Hii Jamani siyo Wafaudu Peke Yao akina Nape

Albedo nimekuomba sana umuachie kijana apumue, madongo unayomrushia sio fair kwa umri wake. Kumbuka yeye binafsi na hata marehemu Snr hawana madoa. Tatizo nape ana kazi ngumu ya kutetea wahalifu ambao yeye binafsi anawachukia. Maswali mengine yalitakiwa yapelekwe kwa mukulu wa kaya
 
Mkuu wangu chama ni kweli sijui kwa nini amekimbia JF siku hizi yupo sana facebook.

Hii ngoma haiwezi jukwaa kubwa hili kule si anamwaga porojo kwa wapambe mwambieni arudi kwenye jukwaa huru tumfundishe hekima

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Bashemere,
Kwanza nikushukuru kwa ustaarabu mkubwa katika kutoa hoja! Hili linatoa nafasi ya kujadili hoja badala ya kejeli na matusi!naahidi kushirikiana na wote watakao kuja kwa hoja kuzijibu moja baada ya nyingine! Sitajishughulisha na kejeli na matusi!

Niweke wazi kuwa msimamo wangu dhidi ya ufisadi na rushwa (ambao kwakweli ni matumizi mabaya ya rasilimali)BADO UKO PALEPALE, NA SITAYUMBA KATIKA HILI!
Nape,nadhani tatizo hapa ni humwelewi mwenyekiti wako.Uko kwenye siasa kwa madhumuni gani?Ni heri usingekubali hicho cheo cha ukatibu mwenezi kwasababu inaonekana kama uko hapo ili tu mkono uende kinywani.Sasa inamnufaisha nani kusema una msimamo usioyumba na ukweli uko wazi kuwa misimamo yako yote ni kinyume na mwenyekiti wako?usipende kujidhalilisha mkuu,you could've been more usefull than becoming an embarassment.Siku 90 bado una msimamo nazo?acha kujidhalilisha kwa kukubali kuingizwa chaka na wasanii waliobobea.
 
Mie binafsi nawapa pongezi Invisible pamoja na team yake nzima mods Paw na wenzake kwa kuweka sawa jukwaa letu pendwa la siasa kwa kukupambana na wahuni walikuwa wanachafua thread mpaka viongozi wa vyama wanakimbia JF...

Leo Nape naona kaamua kuja kujibu hoja za wana JF ndivyo inavyotakiwa...ushauri wa bure kwa Nape, JF ndio sehemu ya kukujenga wewe usikimbie humu njoo JF fungua thread karibisha maswali upambane kwa hoja ndio unakomaa kisiasa..

Ushauri mzuri lkn jamaa ni mwepesi, ana loose temper haraka mno,nimefuatilia thread nilianza kufurahi namna anavojibu/kushiriki mjadala,,mara kaanza kutoa maneno ya ajabu ooo "ndo matatizo ya kushindia kipande ya mhogo na maji" What? Kuna watu kweli hawana cha kula mchana wanatingisha ama ndo kama vile vipande vya mihogo na maji,,Wapo! so inakuwa anawananga. Post ya ajabu unaikaukia hujibu basi.Mwepesi huyu ama shibe ishamlevya kabisa
 
Nape,nadhani tatizo hapa ni humwelewi mwenyekiti wako.Uko kwenye siasa kwa madhumuni gani?Ni heri usingekubali hicho cheo cha ukatibu mwenezi kwasababu inaonekana kama uko hapo ili tu mkono uende kinywani.Sasa inamnufaisha nani kusema una msimamo usioyumba na ukweli uko wazi kuwa misimamo yako yote ni kinyume na mwenyekiti wako?usipende kujidhalilisha mkuu,you could've been more usefull than becoming an embarassment.Siku 90 bado una msimamo nazo?acha kujidhalilisha kwa kukubali kuingizwa chaka na wasanii waliobobea.

jmushi 1;
Kama hoja ilikuwa ni kuulizana watu wameingia kwenye siasa kwa madhumuni gani nadhani hilo ungealianzia Chadema; ni bora ya Nape anayetetea ukweli kuliko yule mnafiki wenu Dr. Slaa anayejinadi kutetea wanyonge kwa manufaa yake na Josephina Nape hajawahi kuilamisha CCM imjengee nyumba na wala hajalamizimisha CCM imlipe kiasi gani, wala Nape hajampa mkewe tenda.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nape, kuna tofauti ya facts and truth. Majibu yako yote ni facts but not truth. Only time will tell ,
 
Hon nape
Ni utaratibu gani umejiwekea kuja kujibu hoja hapa kwa maana kwa wenzetu wa upinzani ni rahisi sana kutokeza hapa na kujibu hoja mbalimbali wewe na viongozi wenzako tunawahitaji sana kwenye jukwaa hili
 
jmushi 1;
Kama hoja ilikuwa ni kuulizana watu wameingia kwenye siasa kwa madhumuni gani nadhani hilo ungealianzia Chadema; ni bora ya Nape anayetetea ukweli kuliko yule mnafiki wenu Dr. Slaa anayejinadi kutetea wanyonge kwa manufaa yake na Josephina Nape hajawahi kuilamisha CCM imjengee nyumba na wala hajalamizimisha CCM imlipe kiasi gani, wala Nape hajampa mkewe tenda.

Chama
Gongo la mboto DSM
Sipo hapa kwa niaba ya chama chochote ndugu "chama".Wacha ajibu maswali kama ana uwezo huo.Na unapochaguwa kumjibia,inatakiwa ufanye hivyo na si kunilinganishia na chadema.Anajuwa ninachosema fika,haina haja ya kujidhalilisha utu,kuna kazi nyingine nyingi tu.Ukiamuwa kuingia kwenye siasa ujitayarishe kuwatumikia wananchi.Hii kuja hapa na kusema eti "Nina misimamo isiyoyumba" ni sawa na ku "insult intelligence" za wengine humu.Yani kwasababu kazidiwa nguvu na mafisadi ndani ya chama,keshagunduwa mwenyekiti anatofautiana na yeye,sasa kiungwana ni kujiondoa kama ni kweli una msimamo,otherwise usituletee dharau hapa.
 
Nape,nadhani tatizo hapa ni humwelewi mwenyekiti wako.Uko kwenye siasa kwa madhumuni gani?Ni heri usingekubali hicho cheo cha ukatibu mwenezi kwasababu inaonekana kama uko hapo ili tu mkono uende kinywani.Sasa inamnufaisha nani kusema una msimamo usioyumba na ukweli uko wazi kuwa misimamo yako yote ni kinyume na mwenyekiti wako?usipende kujidhalilisha mkuu,you could've been more usefull than becoming an embarassment.Siku 90 bado una msimamo nazo?acha kujidhalilisha kwa kukubali kuingizwa chaka na wasanii waliobobea.
Nape anajua wazi kuwa swala la kuvuana Magamba ndani ya CCM haliwezekani, hayo magamba ndio kwanza yamepigwa polish yanang'ara, Wote wanaongoza kamati za bunge zenye nguvu, Vikao vya wabunge wa CCM, Rais amewasafisha.
Nape ushauri ninao kupa kusanya hizo baga kwa sana, manake tayari shavu dodo, baadaya ya 2015 nakuonea huruma sijui utakuwa wapi manake jamaa haweata kuacha..Viongozi wako watakaa pembeni kama kawaida wakitoa tabasamu zao za kingese.
 
Mheshimiwa Nape Nnauye, je ni kweli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika mwezi wa Novemba mwaka jana ambapo hoja ya kuva gamba ilipendekezwa irudishwe Kamati Kuu ya CCM, ulishambuliwa na baadhi ya Wajumbe kuwa unakidhoofisha chama? Nitanukuu;

Mpango wa kujivua Gamba warudishwa CC, Lowassa, Sumaye waja juu

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa alinukuliwa akihoji.

Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

“Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?”Sumaye alinukuliwa akihoji.

Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.

Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: “Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu”.

Je Mheshimiwa kabisa Nape Nnauye, unakubaliana na taarifa hii?
 
##La Anna Kilango umesema wewe, ni uzushi mnajaribu kuwalisha watu kwa sababu mzijuazo nyinyi.
##. La Rais kumsafisha Chenge, nayo ni tafisiri yako. Alichosema Rais kwa mujibu wa taarifa za kimahakama nchini Uingereza "wanadai" hawajafanikiwa kupata ushahidi wa rushwa!(kwa akili ya kawaida UK wangefanyaje zaidi ya kulinda heshima ya nchi yao na kampuni yao kubwa kabisa duniani ya uuzaji silaha?) lLakini hivi tuhuma zilikuwa rada pekeake?! Na ikumbukwe hata Chama kilisema tuhuma na wala hatuhitaji ushahidi wa mahakamani.....

.
Nnauye Jr,

..Labda ulikuwa huna habari na kilichotokea ktk kikao cha wabunge wa CCM kabla ya kuwasilishwa kwa bajeti ya wizara ya nishati na madini. Sasa nakuomba upitie kipande hiki cha habari. Je, una maana gazeti hili limezusha habari za wabunge wa CCM kumsafisha Lowassa?

Lugola, alisema alifuatwa na Ole Sendeka, huku akiahidi kumhonga fedha ili aweze kumuunga mkono hoja yake ya kutaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliachim Maswi, wawajibishwe na Bunge.

“Hoja ya Ole Sendeka, ilimfanya Kangi Lugola kunyanyuka na kuanza kutoa maelezo ambayo kulikuwa na lengo la kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Alipinga wazi kuwawajibisha viongozi wa wizara hiyo, huku akifananisha kinachotaka kufanywa ni sawa na lililomtokea Lowasa.

“Alisema katika ripoti ile ya kamati teule ya Bunge, ilipelekea kumwajibisha Lowassa na baada ya muda iligundulika ilijaa upotoshaji mwingi na kusisitiza katu wabunge hawapo tayari kurudia makosa ya mwaka 2008, ambapo vilitolewa vielelezo vya mitaani,” alisema mtoa habari huyo.

Baada ya maelezo ya Lugola, naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), aliunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa mwaka 2008, Bunge liliaminishwa Lowassa, alikuwa mhusika na Richmond, kutokana na jambo hilo kukosa ushahidi alitahadharisha kutorudiwa kwa makosa tena.“Kilango, alisema wabunge waliamini alikula fedha kwa kulipwa na Richmond, lakini hakuna ukweli, hivyo hakuna sababu ya kumwajibisha Waziri wa Nishati wala Katibu Mkuu wake.

“Baada ya hapo aliinuka Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy Mohammed (CCM), ambaye alisema katu hayuko tayari kuunga mkono hoja ya Ole Sendeka, kwani tangu alipondolewa Lowasa katika nafasi ya uwaziri mkuu nchi imekuwa ikiyumba.

“Mjadala ulikuwa mkali ndugu yangu, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alisema wabunge hawako tayari kurudia makosa ya Richmond, hatakuwa tayari kuubariki mpango huo aliouita mchafu,” kilisema chanzo hicho

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom