Saed Kubenea yuko wapi?

Jamani huyu saed kubenea ana mchango mkubwa hapa nchini kwa mageuzi, Mungu wangu wa israel ampe maisha marefu.Amen
 
Kaka yangu Kimbunga kama unakumbuka vizuri miaka miwili ya nyuma na kipindi cha kampeni za uchaguzi siku ya Jumatano ikifika saa tano asubuhi ulipati gazeti la Mwanahalisi leo siku ya Alhamisi pita kwenye vibanda vya magazeti uone mzigo ulivyojaa.

Wewe inaelekea unashinda kwenye kile kijiwe pale LUMUMBA ambapo gazeti la UHURU linaisha kabla ya saa mbili asubuhi.
 
Mimi mwenyewe kaka nimestuka kusikia jamaa anatafuta diploma! wakati kuna vijana kama 500 kila mwaka wanamaliza BA Journalism na BA Mass Com bongo! Kweli ukistaajabu ya Musa

Kubenea ni jemedari na jabali katka kutoa kisichoweza kuandikwa na magazeti mengine,soma comrade urudi tukomboe taifa
 
Usemayo sio kweli. Ni kweli JK alikwenda Muhimbili kumuona baada tu ya tukio la tindikali na kumuahidi serikali kumgharamia gharama za matibabu, lakini ilikuwa ni usanii tu wa JK kama kawaida yake.

gharama zote amekuwa akitoa Mzee Mengi na waziri mmoja ambaye sitaki kumtaja.

Ukweli ndiyo huo.

Jk alipita India kumuangalia Kubenea.
 
Jk alipita India kumuangalia Kubenea.

kama alipita kumuangalia basi maisha yake yako hatarini zaidi,kubenea alimwagiwa acid baada kuchapisha taarifa za kibenki za mabilioni ya jk na riz1 kwenye benki ya nbc,..jk spare kubenea's life
 
Jambo usilolijua ni sawa nausiku wa giza,jamaa yuko fiti kutujuza uozo wa hili liserikali,kwangu mimi hiyo yatosha kumpa heshima ya udaktari,sio hii mijamaa yenu inayotunukiwa heshima za uizi wa mali za umma. Hatuhitaji kujua elimu yake anayofanya yatosha kuliko hiyo mijitu yenye PHD za uizi.
 
Jamani kusoma diploma siyo lazima iwe "ORDINARY DIP" Post Grad. Dip ambayo hata mwenye PhD anaweza kuichukuwa hasa hizo za nje ya nchi.
 
Usemayo sio kweli. Ni kweli JK alikwenda Muhimbili kumuona baada tu ya tukio la tindikali na kumuahidi serikali kumgharamia gharama za matibabu, lakini ilikuwa ni usanii tu wa JK kama kawaida yake.

gharama zote amekuwa akitoa Mzee Mengi na waziri mmoja ambaye sitaki kumtaja.

Ukweli ndiyo huo.

Ni kweli uliyosema lakini chumvi nyingi! Ni kweli serikali iliahidi kumgharamia lakini haikutekeleza.
Lakini una ushahidi gani Kubenea kusaidiwa na Mengi na huyo waziri? Kama ni kweli mbona umemtaja Mengi lakini mzito kumtamka huyo mwingine? Tujifunze kusema Kama great
thinkers, tuache soga na ngonjera za uani! Kubenea naamini atatushuhudia ni nano anagharamia mahitaji yake! Nahofu unajenga picha kwamba shujaa anatumiwa na wafadhili, sio kweli, na mfahamu ni Mtu huru sana
 
Mwenye taarifa kuhusu alipo Saed Kubenea ambaye amekuwa mwandishi wa gazeti la Mwanahalisi kwa muda mrefu tafadhali anijulishe. Mimi ni mpenzi sana wa articles zake za kisiasa katika Gazeti hilo. Kama anafanya na gazeti lingine tafadhali naombe Kujuzwa ili nifuatilie habari anazoziandika.

Kashalishwa tamu ya chama tawala akirudi masomoni si yeye tena mtamwona ..unacheza na sumu ya mwakyembe nini hata wewe ungesepa zako fasta
 
Laiti wanaomsifia Kubenea wangemjua Kubenea wa kweli ambaye aliwahi kufanya kazi Habari Corp wasingepoteza sifa zao bure. Anyway Kubenea bila Ndimara Tegambwage hayupo you know what I mean. Kubenea ni kihiyo wa kawaida anayeanza kuitafuta elimu kwa sasa huu ukiwa ushahidi kuwa Kubenea aliyejulikana siyo yule wa kweli. Makala zake nyingi alikuwa akiandikiwa na watu kiasi cha wakati mwingine hata kusahau emails zao mmojawapo akiwa Paschary Mayega. Kubenea ni mission to town wa kawaida kama meya wa jiji la Dar Didas Massaburi aneyeitwa dokta bila kusomea. Kubenea bila watu kama Ansbert Ngurumo kumuandikia nyuma ya pazia asingekuwapo so to speak. Heri ameamua kwenda kuondoa ujinga wake.
 
Mkuu mpayukaji umenikumbusha wakati Kubenea yupo Habari Corporation aliwahi kuandika habari za kizushi kwenye Gazeti la Rai waakati huo hilo gazeti lilikuwa linaheshimika sana. Aliandika habari za kumsingizia Mzee Ngeze aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Kagera. Kubenea alisema amekutana na Ngeze na kumhoji masuala kadhaa kitu ambacho hakikuwa kweli. Wakati huo Mzee Ngeze alikuwa na msuguano na Masilingi (wakati huo waziri). Baada ya uchunguzi ilibainika kwamba si kweli hakukuwa na mahojiano yoyote bali Kubenea alitunga stori na kumwekea mzee Ngeze maneno kinywani! Ilibidi Rai limuombe radhi Mzee Ngeze na nadhani Kubenea alifutwa kazi. Iligundulika kwamba hana weledi wala vyeti!
 
Last edited by a moderator:
Mchuzi wa bata bwana yaani Mwanahalisi limefikia hali hiyo kweli?

Mkuu Kimbunga,
mbona simple tu....kama upo Dar basi jaribu kupita kwenye meza za magazeti.....leo hii ni Ijumaa na Mwanahalisi linatoka Jumatano. Kama utalikuta, basi maelezo ya Mchuzi wa bata hata kama sio sahihi lakini yanaelekea kwenye ukweli wa kuchukiza! Na kama haupo TZ, mbona simple, mpigie nduguyo simu mwambie akuchekie hilo gazeti kv kuna kitu umesikia wameandika!
 
Mimi mwenyewe kaka nimestuka kusikia jamaa anatafuta diploma! wakati kuna vijana kama 500 kila mwaka wanamaliza BA Journalism na BA Mass Com bongo! Kweli ukistaajabu ya Musa

hiyo shule yenu ya vyeti tu pasipo kuwa na uwezo ndio yale tuliyoyaona kwenye bunge la AFRIKA MASHARIKI wagombea wenye vyeti vizuri na madigree kibao kujieleza ni %O Sasa Huyu Kubenea hata kama hana vyeti vya digree but uwezo wake ni bora mara 100 zaidi ya hao mnaowaona wana elimu safi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom