Saed Kubenea na gazeti la MwanaHalisi

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Ni mwandishi pekee aliyekwenda kwa hiyari yake mwenyewe kutoa ushahidi kwenye tume ya mwakyembe na amekuwa akisakamwa na mafisadi kila kukicha lakini ametoa maisha yake kwa nchi yake
 
Habari zilizonifika zinathibitisha kuwa kubenea anatoka na gazeti linaloitwa HALIHALISI ambalo lilikuwa ni mali Ahmad Rashid wa chama cha CUF.bado haijajulikana kama ameuziwa au ameajiliwa huko
 
Habari zilizonifika zinathibitisha kuwa kubenea anatoka na gazeti linaloitwa HALIHALISI ambalo lilikuwa ni mali Ahmad Rashid wa chama cha CUF.bado haijajulikana kama ameuziwa au ameajiliwa huko

HaliHalisi ni gazeti la Saed Kubenea, ambalo Hamad Rashid alilizuia na Kubenea akaenda Mahakamani, kuna hati za kiapo zinazoonyesha kwamba ni la Kubenea na hata katika ubao wa "HaliHalisi Publisher utaona ni wachapishaji wa MwanaHalisi, HaliHalisi na Mseto" .

Bahati mbaya ama nzuri, malalamiko yaliwahi kuwasilishwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na Kubenea alikwenda kulalamika kwa Lowassa kwamba hilo ni gazeti lake ambalo limezuiwa kimakosa na Hamad Rashid. Lakini kwa mazingira ya sasa, Hamad Rashid hawezi tena kumzuia Kubenea kuchapisha gazeti hilo, ila Mheshimiwa Hamad anaelezwa kuwa alikuwa katika matibabu nje ya nchi. Gazeti la HaliHalisi lilianzishwa kwa mara ya kwanza na kambi ya upinzani bungeni kabla ya kambi hiyo kushindwa kuliendesha na Kubenea kuliomba na kukabidhiwa kuliendesha kama lake. Lilipoingia mizengwe hasa baada ya Hamad Rashid kuwa Kiongozi wa Upinzani, Kubenea ndipo kwa haraka akaanzisha MwanaHalisi, kwa hiyo "HaliHalisi si jipya."
 
sasa huo ugomvi kati Kubenea na hamad rashid uliishaje? Maana si vema kuchukulia for granted kwamba hamad Rashid hawezi kuzuia Kubenea kuchapisha hilo gazeti.
Tena, usajili wa gazeti hilo upo hai?
 
kumbe hata kubenea hakufungiwa alitakiwa hata yeye afungiwe kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya uandishi
 
kumbe hata kubenea hakufungiwa alitakiwa hata yeye afungiwe kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya uandishi

.. hapo ndipo ujue kuwa waziri wako hakutumia akili bali maguvu! Utawala huu ni wa "hisia" na "visasi" zaidi kuliko sheria!
 
kumbe hata kubenea hakufungiwa alitakiwa hata yeye afungiwe kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya uandishi
that is the technical party of the penalty/sentence!!!
 
kumbe hata kubenea hakufungiwa alitakiwa hata yeye afungiwe kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya uandishi

Shy uko nchi gani? ukijibu nitajua, maana inawezekana unaota au umetoka usingizini. Kama uko sawa fafanua watu wachangie, ama unatania?
 
kumbe hata kubenea hakufungiwa alitakiwa hata yeye afungiwe kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya uandishi
Shy sasa hilo ndilo linaitwa bao la kisigino, mwendo mdundo!
 
kwa kawaida watu huwa hatuamini ukweli,Big up KUBENEA tunaona vitu vyako,ipo siku watakubeba na kukushangilia
 
tunashukuru Kubenea endeleza juhudi zako za kufichua uovu na uozo ndani na nje ya chama, wamezidi hao walidhani wamekukomoa kumbe wamejikomoa moto ule ule hakuna kulala wakoboe tu..
 
kumbe hata kubenea hakufungiwa alitakiwa hata yeye afungiwe kujihusisha kwa namna yoyote ile na mambo ya uandishi

Unajua hata mimi nilifikiria ikiwa Kubenea ataanzisha gazeti klake,watafanya nini? Maankae walilifungia gazeti.Ama kweli tuna vilaza,sasa kwenye kutoa adhabu kwa mtu mchochezi tunafanya hivi,Je kwenye mikataba ya madini,kununua shehena za kijeshi,kuanzisha au kusaini mikataba mikubwa ya kujenga na kuendesha viwanda?

Kaazi kwelikweli,hapo ndipo gap liakoanzia!
 
kama inawezekana atoe mwanahalisi in his website sisi tutalisoma huko!!! mafisadi walie tuu
 
Big Up Kubenea. Receive my hi10. Tena fanya haraka, leta utamu na midundo ya mafisadiz. Kufungia gazeti si kufungia taaluma yako ya uandishi.

Waziri mchemfu huyo. Ati Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa miezi mitatu!!!! Kwani miezi mitatu mbali??? Mbona Tume ya Kuchunguza mafisadi walichukua miezi almost nane na hawakuja na issue???? Na bado tukauona muda huo mfupi wa kusubiri kitu kumbe mbofu tu. Miezi mitatu isikutishe bro. Songa mbele tuko nyuma yako. Wewe ni kirongora wetu katika hii vita ya mafisadiz.

Ikiwezekana achana na Halihalisi leta mdundo mwingine. Keep it up followers and supporters of Kubenea!!! Shame to Mafisadiz and their relatives, family, followers, and their supporters, including those who misdirect threads on Fisadiz.
 
Habari zilizonifika zinathibitisha kuwa kubenea anatoka na gazeti linaloitwa HALIHALISI ambalo lilikuwa ni mali Ahmad Rashid wa chama cha CUF.bado haijajulikana kama ameuziwa au ameajiliwa huko

Hili ni tatizo kubwa sana hivi sasa Tanzania watu wengi kwenye R wanaweka L hawa ndio waliosoma enzi zile hakina migomo baridi wala moto hawa wanaosoma sasa kwenye Z si wataweka A?, hivi kiingereza pia huwa mnakosea hivi?si maana inapotea? Kazi ipo!
 
Back
Top Bottom