Saed Kubenea: Aliyosema Mwalimu Nyerere sasa yametimia

daaa,watu bwana,wengine washaanza kuchangia thread kali hii kwa mitazamo ya kidini,anyway ni migongano tu kwani hata glasi kabatini hugongana,suala la msingi hapa ni kuwa alichosema kubenea ni ukweli mtupu na itabaki kuwa hivyohivyo,huwezi kumfananisha nyerere na raisi yeyote aliyukuja mbele yake kwani yy alichukia ufisadi na hakukumbatia matajiri,na hata madini hakuwa na haraka nayo kuyachimba na alikuwa na msimamo na kauli moja,hakuwa legelege,alikuwa na qualities za uongozi ingawaje pia alikuwa na udhaif
 
Mwanahalisi siku hizi limeishakuwa gazeti la udaku, watu wamelichoka mpaka saa 10 jioni lipo kwenye vibanda vya magazeti.

Hoja dhaifu sana hii,pengine limekua la udaku kwa nyie wenye kusoma zaidi magazeti ya Eric Shigongo,so mitazamo yenu kwa magazeti mengine kama mwanahalisi lazima yawe ni ya udaku
 
Nyerere kafanya nini cha maana? Mwinyi kaanza kuibomoa misingi mibovu aliyoiweka Nyerere iliyotufanya maskini wa mwisho duniani. Eti kila kitu cha umma! khaaa! jitu halijui hata choo cha flash ni nini unakuja unamwambia haya simamia majengo ya umma! hiyo ni akili kweli? kwanza angefundishwa namna ya kutumia choo.
Utawahadaa hao hao mazezeta,wewe ni mmoja wa wasaliti wakubwa wa nchi hii amini nakuambia kila chenye mwanzo kina mwisho hata kama sio leo
 
Kwa ufupi CCM imeshindwa kuongoza nchii, toka ilivyoacha miiko yake kwa kuvunja azimio la Arusha mambo yote yaliharibikia hapo. Kurekebisha hii hali ni kuondoa mfumo mzima kwani wote wameoza pale
 
Nani ana CV ya kilaza kubenea?naomba anyooshe mkono juu na atuwekee hapa ili tuijue kabla ya kupoteza muda kujadili maandishi yake.

Na hivi tume ya kuchunguza mauaji ya wale wafanyabiashara wa madini iliundwa na nani?
 
Mwanahalisi siku hizi limeishakuwa gazeti la udaku, watu wamelichoka mpaka saa 10 jioni lipo kwenye vibanda vya magazeti.

nakala zinatolewa za kutosha na linanuliwa sana!
Gazeti gani linakwishwa ?
 
Utawahadaa hao hao mazezeta,wewe ni mmoja wa wasaliti wakubwa wa nchi hii amini nakuambia kila chenye mwanzo kina mwisho hata kama sio leo

Wewe nishambilie mimi binafsi mpaka uchoke, mimi nashambulia rikodi zilizokuwepo. Hapo sasa!

Unga wa yanga umeshakunywa uji wake wewe? (mimi nimeshakunywa wakati wa Nyerere).
 
Tutabishana sana kwa hoja maana kila mtu anahoja zake, lakini ukweli ni kwamba kunatatizo tz, tatizo kubwa. Serikali ilipaswa kushughulikia hali hiyo na sio kubeza madai makubwa na ya msingi kama hayo aliyoweka Kubenea. Kauli mbili mbili kwenye suala moja za nini? hii ni mbaya na wala sidhani kuna MTZ anafurahia serikal kuwa kama imepalaganyika vile, tunawalipa hawa watu kufanya kazi, sio kututelekeza na matatizo kibao yasiyo na majibu sahihi.
 
Najua wengi mtanibishia lakini nimeyasema haya toka zamani kwamba adui yetu sisi sio JK bali ni chama CCM. Hii vita ya kuonyesha udhaifu wa JK ni kukosa kuona mbali kwamba chama CCM toka walipolichukua Azimio la Zanzibar ndipo ulegelege wake ulipoanza. Mbegu ilipandwa siku ile, Mkapa akaja kuiwekea mbolea na kumwagilia maji akasifiwa sana halafu sasa wakati wa JK tunavuna walichopanda..

Tatizo letu wote hapa JF tunataka kuziweka lawama kwa mtu mmoja japokuwa kiutawala JK alitakiwa kuyaona hayo na kuwaahidi wananchi ataweza kuyazuia lakini ameshindwa kwa sababu bado anaamini ktk Maazimio ya chama kuhusu Azimio lile linalowafaidhisha kundi la watu. Nimesikia habari nyingi sana kuhusu JK kuwa ni Statesman, tusubiri, sijui anapima lakini ukweli unabakia kwamba maadam ni muumini wa yale yale yalotufikisha hapa hataweza kubadilisha kitu. Amebakiza miaka yake mitatu alivue joho na hakuna atakachoweza tena..

Maneno ya mwalimu yametimia kweli maana tunavuna tulichokipanda na kwa bahati mbaya sana watu wanafikiria tatizo ni JK akiondoka na kuja sijui Lowassa au Asha Rose Migiro basi mambo yatakuwa mazuri.. Hakuna kitu tuubomoe mfumo mzima wa uongozi ktk Katiba hii mpya na kama kweli tutaweza kufanya hivyo basi yawezekana tukapata tumaini jipya..Kinyume cha hapo tunahitaji mageuzi kamili a 360 turn kurudi nyuma tulipoharibu na kurekebisha kisha tunarudi ktk mduara wetu..

Sii kazi ndogo lakini inahitaji sisi wenyewe kujitazama na sio kutegemea IMF au World bank tunasuriwa maana wao wachohitaji siku zote ni Taifa lenye shinda ya mikopo na misaada ili watengeneze faida zao ktk interest kama benki zinavyo tukopesha na kutuweka ktk madeni muda wote wa maisha yetu. Tutakopa tu pale tunahitaji kukopa na kwa mahitaji yetu sisi sio ya kupangiwa.

Soma katikati ya mistari. Imetajwa Serikali inayoongozwa na CCM ambayo Mwenyekiti wake ni JK ambaye ndiye Rais pia. Watanzania si wajinga tusijue kuwa tumeichoka CCM kwa ujumla lakini haituzuii kuita spade ni spade
 
Nyerere kafanya nini cha maana? Mwinyi kaanza kuibomoa misingi mibovu aliyoiweka Nyerere iliyotufanya maskini wa mwisho duniani. Eti kila kitu cha umma! khaaa! jitu halijui hata choo cha flash ni nini unakuja unamwambia haya simamia majengo ya umma! hiyo ni akili kweli? kwanza angefundishwa namna ya kutumia choo.


Mnatafuta visingizio kwa ujinga na upuuzi wenu mwalimu alifanya kazi yake na muda wake ukaisha!!!

Wewe na wana magamba wenzio mnatakiwa mipge hatua....

Au la semeni na kubalini wazi kuwa nchi imewashinda!!

Kagame aliichukua nchi baada kuvurugika kabisa!! lakini angalia sasa anavoenda vizuri....wala hamsingizii mtu kuwa

aliweka misingi mibaya ndiyo maana haendelei, yeye anasonga mbele!!....

Angalia usivyo na sono wala akili....!! unadhani kujua kutumia choo cha kuflashi ndiyo akili!!

Wewe na Wenzio CCM ni janga la Dunia....maana hata hao wazungu wanaotunyonya inafikia hatua wanatuonea

huruma kwa umbumbu wetu!
 
Nani ana CV ya kilaza kubenea?naomba anyooshe mkono juu na atuwekee hapa ili tuijue kabla ya kupoteza muda kujadili maandishi yake.

Na hivi tume ya kuchunguza mauaji ya wale wafanyabiashara wa madini iliundwa na nani?

Mimi naomba tuwekee CV yako hapa maana unataka kulinganisha hoja kwa CV.
 
Hicho chama wakati wake kilifanya nini zaidi ya kuiingiza hii nchi kwenye lindi la umaskini. Ni yeye aliyekianzisha na kilikuwa na misingi mibovu, imebomolewa sasa inasukwa upya. Na bado!
unatia hasira wewe!! basi tu huku kuna ban!
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom