Sabodo kumchangia mgombea wa CHADEMA milioni 500

nina mashaka na usafi wa pesa za Sabodo

Kama Sabodo asingekuwa msafi unafikiri angekuwa na jeuri ya kuchangia CDM, tena kwa uwazi hivyo? Waulizeni wafanyabiashara, wako wengi sana wanaipenda CDM lakini hawadhubutu hata kwa usiri kuichangia kwa sababu wanasema siku wakijulikana ndio mwisho wao. Hivi mnafikiri Sabodo halijui hilo? Hivi Mnafikiri TRA hawajapewa maagizo ya kumfuatilia Sabodo?
 
Nimafurahi sana Sabodo kuichangia CDM. Na wengi hawajui kwa nini Sabodo anaichangia CDM, habari za ndani kabisa Sabodo anaichangia CDM kwa sababu ni vision ya rafiki yake Nyerere kwa CHADEMA itakuwa chama kikubwa mbele ya safari. Lakini pia wazee wa Mwalimu Nyerere Foundation hawaikubali CCM kwa sasa na wengi wao chini chini wanaisadia CDM mawazo na kuwaonyesha njia ya kupitia. Ukiweza kumtenganisha Arcado Ntagazwa na MNF unaweza kunibishia.

Lakini tafakuri yangu iko kwenye kiwango cha mwisho kwa mtu mmoja kukichangia chama cha siasa. Sabodo keshaichangia CDM Shilingi Milioni 700 mpaka sasa. kweli visima ni vitu vya msingi lakini kwa nini chama kisihamasishe watu wengi wachangie kuliko mtu mmoja kutoa hela zote hizo. Tamiri alipotoa milioni 400 kuisaidia UVCCM wengine tulipiga sana kelele kwamba hela zote hizo anatoa kama sadaka ,analipa kodi huyu? Rekodi ya wanaotuchangia katika kulipa kodi ni muhimu kupitiwa.
 
Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafuteni vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.

Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.

Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao pia wako katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Kama chadema ni makini Watch Out.

Kutoka kwa sabodo kuliko zenu mlizowaibia wananchi- Kagoda, deep green meremeta etc
 
Acha wivu wa kike, alichopinga Sobodo na suala la kuulizia asili ya wapangaji! Huo ni ubaguzi!

Haya Mkuu wivu wa kike huoooooooooooooooooooooooooo Ya Sabodo hayo.Kumekuchaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa na Makuchaaaaaaaaaaaaaaa yakeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.Chademaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Mpoooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Acha wivu wa kike, alichopinga Sobodo na suala la kuulizia asili ya wapangaji! Huo ni ubaguzi!


THURSDAY, 20 OCTOBER 2011 19:27 NEWSROOM


* Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffer Sabodo, amesema hajahama na wala hana mpango wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho amekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40.

Sabodo alisema baadhi ya kauli kali ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya CCM, hazina maana kuwa anaichukia, isipokuwa zinalenga kukikosoa Chama ili kiendelee kuwa imara katika kuwaongoza Watanzania na kuharakisha maendeleo yao. Hayo aliyasema jana alipozungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati nyumbani kwake, Upanga, Dar es Salaam na kuwataka wana CCM na wananchi kwa jumla wasimwelewe vibaya.

"Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, "Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi."

Alitoa toa wito kwa wananchi kutofanya makosa ya kufanya majaribio ya kuwapa ridhaa wapinzani kuunda serikali. "Nawaomba Watanzania wenzangu, tusifanye majaribio ya kuwapa CHADEMA au chama kingine chochote zaidi ya CCM kuongoza serikali kwa kuwa havina uzoefu, hatuwezi kufanya majaribio ya kuliweka rehani Taifa," alisema mfanyabiashara huyo.

Kuhusu msaada wa sh. milioni 100 alizotoa hivi karibuni kwa CHADEMA za kuchimba visima vya maji, alisema ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kuwa visima vitakavyochimbwa vitasaidia wananchi wote bila kujali itikadi zao za siasa.

Alisema amepanga kuchimba visima 200 katika majimbo yote nchini, bila kujali wabunge wa majimbo hayo wanatoka vyama gani kwa kuwa lengo lake ni kuwasaidia Watanzania na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya CCM.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Chiligati alimshukuru Sabodo kwa kutoa msimamo wake huo kwa kuwa unamaliza minong'ono ya baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla juu ya msimamo wa mfanyabiashara huyo ndani ya Chama.

"Nitawajulisha wanachama wenzako wa CCM na wananchi kwa jumla, kwamba bado uko nao kwa hali na mali ndani ya Chama chetu kwa ajili ya ustawi wa taifa letu, kauli yako imemaliza minong'ono kwamba umehama au una mpango wa kuhama CCM," alisema.
.

Inainuma sana kila nikifikilia uwaga nilalia..........wimbo wa juma nature !!!Wiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiivuuuuuu huo jamani wivuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu na bado.
 
Back
Top Bottom