Sabodo atunukiwa Medali na CHADEMA: Aahidi kuchangia tena mil. 150

Mungu akuzidishe sobodo heri yako wewe unapenda maendeleo sio vigogo wetu kazi yao kuambukiza dada zetu ukimwi kwa kodi zetu
 
Chama cha demokrasia na maendeleo kimetunuku Medali ya heshima na ujasili Mzee sabodo kwa kukichangia chama hicho waziwazi.

Pia ameahidi kukichangia tena chama hicho Milioni 150.

ITV.


Ujasiri wa huyu kada wa ccm (kama alivyojitambulisha) ni wakuigwa. Kwasababu watu wengi wanaotoa michango kwenye vyama huwa na tabia ya kujificha mbele ya jamii na hii upelekea kufaidika na michango yao hiyo bila jamii kuhoji. Leo hii tukionyeshwa mabilioni ya vyama yalichangwa na akina nani (2000/2005/2010) si ajabu tukakuta ndio hao hao wananufaika na kandarasi mbalimbali za serikali!
 
Ujasiri wa huyu kada wa ccm (kama alivyojitambulisha) ni wakuigwa. Kwasababu watu wengi wanaotoa michango kwenye vyama huwa na tabia ya kujificha mbele ya jamii na hii upelekea kufaidika na michango yao hiyo bila jamii kuhoji. Leo hii tukionyeshwa mabilioni ya vyama yalichangwa na akina nani (2000/2005/2010) si ajabu tukakuta ndio hao hao wananufaika na kandarasi mbalimbali za serikali!

Hapo umenena Mkuu!
 
Wandugu zetu CHADEMA yule muhindi ni Mtanzania? mbona hata Kiswahili hajuwi? Nimekuwa nikishuhudia mara nyingi mkiwabatiza wahindi (ma*********) wote si wazalendo ,leo kiwapi na kumtunukia juu! Ama kweli usitukane wakunga na >>>>>>>>>>>>!
 
Hongera sabodo tunakubali mchango wako. Manake ccm wametengeneza umaskini ili kutumia kama fimbo kuwasamabaratisha si unaona zitto. Nakushukuru sabodo kwa mfano bora mungu akupe uhai kwa kuonesha njia na uzalendo kwa taifa lako hongera saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana.
 
Kwa Mtanzania yeyote kuchangia Chama cha upinzani kwa uwazi ni lazima uwe na uhakika kuwa wewe ni safi - hukwepi kodi na huna kosa lolote la jinai. Kama kuna mahali popote umekiuka taratibu au mambo yako yamekaa kuweza kuwa na mazingira ya kuweza kusingiziwa kesi, CCM kwa kutumia serikali yake watafanya hivyo. Mzee Sabodo kufanya hiki anachokifanya ni dhahiri ni mtu safi ambaye anajua hawana pa kumkamata au kumsingizia kesi.

Mzee huyu, alikuwa mwumini mkubwa wa siasa za mwalimu, naambiwa kazi yake kubwa ni kilimo cha mashamba makubwa. Huyu ni haki yake kupewa nishani hii maana ni mwezeshaji wa mabadiliko.
 
Huyu mzee amenifurahisha sana kwa kuamua kukipa Chadema Tshs. 150,000,000 kwa ajili ya kujenga chuo cha maadili ya uongozi kwa wanachama wa CHADEMA ambapo chadema wamesema kitaitwa "Mustafa Sabodo Accademy". Nadhani huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuwafunda viongozi vijana wa CHADEMA. Pia wana JF mnaonaje tukio la jana la Mzee Sabodo kupewa Medal ya "Courage and Goodwill". Kwangu mimi naona Chadema wana watu vichwa sana kwani CCM haijawahi kufanya kitu kama hicho tangu kuanzishwa kwake na si ajabu punde mkasikia wanawatunuku watu wao Medal maana wamezoea kuiga!
 
Kweli kabisa iyo imedhiirisha CHADEMA walivyo makini katika mambo yao. Wanafanya kwa uwazi na ukweli. Iyo academy pia itakua msingi mzuri wa kujenga viongozi imara,wazalendo na wenye kuweka maslahi ya taifa mbele ya maslahi binafsi na ya chama. Jambo la msingi wakufunzi wa iyo academy wawe ni watu waliotukuka na kubobea katika masuala ya uongozi. Si vibaya wakufunzi wakiwa wakongwe kama Jaji Warioba, Salim Ahmed Salim n.k.
 
dr.slaa alisema kwenye kampeni (kama si sikosei) "kikwete mambo mengi anafanya kutokana na maagizo yangu" (sijui kama nimekosea kumnukuu).
kwa maana hiyo kila ambacho kitafanyika chini ya uongozi wa slaa lazima wataiga tu!
ni vizuri lakini kwa maendeleo ya Tanzania
 
RIP CHADEMA

coffin_lg.gif
 

Kama vile mlivyowatengeneza lukuki katika chama chenu?

Wakutumwa bado mpo tu?

Unafikiri chadema ni kama nyie!

mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu...kweli ww ni mwana fisadi damu mana kuona mtu kachangia tu ukahisi ni kama mfanyavyo uko kwenu,kwanza nachefuka ona iyo rangi ya profile yako na iyo nyundo na yako ambayo soon itakumaliza mwenyewe.....ila kwa leo nmekusamehe sio kosa lako

Mafisadi ni kwenu huko mbona wanaochangiaga huko watuwasikii! kwa nini wanakosa ujasiri au kwa nini chama chenu (CCM) hakiwasemi/hakiwaweki hadharani??

Si mnajificha kwa sababu nyie ni mafisadi......................................

Atoaye kwa uwazi na Kupongezwa hadharani hawezi kutengenezwa kuwa fisadi. Sio wale wanaokwapua 40 bil na kuipa Chama twawala 10 bil kisha wanapewa uwezo hata wa kuhakikisha wanamweka Spika wa Bunge au waziri wamtakaye wao.

Kwa usemi wako huo unakili kuwa chama chenu ni chama cha mafisadi si ndio?

Kichwa maji huyu hapa

Umezoea kutukanwa wewe.

fisadi hujificha anafanya mambo yake kwa siri, na atoaye kwa chama pinzani wakati wa mwanga ni nuru huyo!
Naona mmeshachakachua maana ya Fisadi....
 
Taratibu Chadema inaanza kutengeneza Mafisadi

Huyu bwana alianza kuichaambua serikali toka enzi za Mkapa. Na wakati ule chama kikubwa cha upinzani kilikuwa CUF na si CDM. Akaendelea wakati JK alipochukua nchi kwa kumpa ushauri namna anavyoweza kuongeza mapato ya serikali kwenye kampuni za simu. Alikuwa anajaza kurasa mbili za gazeti kuelezea namna JK na serikali inavyoweza kuongeza mapato na kutoa huduma bora(kama zilivyo sera za CHADEMA).
Kama wewe ni mfuatiliaji wasiku nyingi wa habari za siasa sidhani kama utashangaa kwa Bw. Sabodo kuchangia CDM. Huyu bwana anaweza kuwa CCM but damu yake ni nyeupe na Blue (CDM).
 
Back
Top Bottom