Sabodo atoa 100 mil, baiskeli za walemavu, visima 10, ashangazwa na Mkapa

awakabidhi chademazaidi ya tsh mil 100, baiskeli za walemavu 100 na atachimba visima 10 arusha. Mungu ambariki sana Mstapha Sebodo.
 
Huyu mzee alishasoma alama za nyakati! maana haihitaji degree kulijua hilo.
 
Ubarikiwe SABODO, Mungu akuzidishie ulipochota, akuongeze siku za kuishi mpaka uyaone mabadiriko ndani ya nchi.
 
Tuntemeke na genge la wahuni ambao walisema pesa za sabodo zimeliwa na majemedali. Nadhan saiz macho yamewatoka km mjusi kabanwa na mlango.
 
Tunashukuru kwa hilo.Namfahamu mzee huyo.Kuna wakati nilimwendea Sabodo kutaka msaada wa masomo nje ya nchi lakini nilijibiwa anasaidia vikundi na sio mtu mmoja mmoja.

Kwa hiyo ukafanyaje, si ungeenda kuwakusanya watu ambao wameshindwa kwenda shule kwa sababu ya school fees?
 
Boflo naye katoa mchango mkubwa kwa Avatar yake. Imeilemba hii thread inaonekana bomba kweli kweli. Anastahili pongezi
 
sabodo1.jpg sabodo2.jpg
 
Dar anastahili pongezi! HIVI HUYU MZEE ANAJISHUGHULISHA NA NINI? I mean nini chanzo cha utajiri wake?
 
Sabodo ni mfuasi mkubwa sana wa Mwl Nyerere.. Anasononeka sana kutokana na haya yanayofanywa sasa na Viongozi wa CCM.. Alishawahi kumjibu Kiongozi mmoja mkubwa wa Serikali ambae alimlalamikia kwa kitendo cha kutoa hela za mwanzo wakati ule wa uchaguzi.. Bila ya kumung'unya maneno alimuambia anamuenzi Mwalimu kwa maana kinatakiwa Chama imara cha kuistua CCM.. That's Sabodo.. Haogopi wala kutishwa na lolote..
 
Barikiwa sana mzee Saboro,na Mungu akuzidishie maisha marefu sana mzee wetu mpendwa
 

Wakuu mambo ya leo hayakuwa madogo, ingawa intelejensia ya chama tangu Jumatatu ilishanusa kuwa hali hiyo ingetarajiwa kutokea kama ilivyotangazwa leo mahakamani, hivyo vikalazimika kuwepo vikao na consultations hapa na pale kiasi cha kudelay hii taarifa.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Mmoja wa makada wakongwe wa CCM na mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffer Mustafa Sabodo amechangia tena harakati na vuguvugu la ukombozi wa nchi yetu kwa kutoa Sh. milioni 100, ambayo itawekwa kwenye account ya M4C, kuendeleza gurudumu la mapambano yanayoendeshwa na CHADEMA kwa ajili ya Watanzania.

Akikabidhi hundi ya fedha hizo kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Daktari Willibrod Slaa, mbele ya wanahabari, Mzee Sabodo alisema anafurahishwa sana na kazi inayofanywa na chama hicho, chini ya usimamizi makini wa Kamanda wa Anga, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Dkt. Slaa na wasaidizi wao, huku akisema 'tumechoshwa na CCM miaka 50...huyu huyu huyu'.

Mbali ya hundi hiyo ya Sh. milioni 100, Mzee Sabodo ametoa baiskeli 100 za walemavu kwa ajili ya CHADEMA, akimwambia Dkt. Slaa kuwa chama hicho kiweke utaratibu wa namna ya kuzigawa kwa wahusika. Pia amesisitiza ahadi yake ya kusaidia uchimbaji wa visima katika Jimbo la Arumeru Mashariki, ambapo ameongeza idadi ya visima hivyo badala ya vinne sasa atasaidia visima 10.

Akizungumza mapema kabla ya kukabidhi hundi hiyo na ahadi hizo zingine, Mzee Sabodo akizungumza mbele ya wanahabari wa vyombo mbalimbali, alimwambia Dkt. Slaa kuwa amekuwa akiwaombea CHADEMA na kuwatakia kila la heri, akitumaini kuwa watafanikiwa katika harakati zao za kuongoza vita dhidi ya ufisadi, kudai uwajibikaji kwa wananchi na mabadiliko ya kimfumo na utawala nchini.

"Nimeshangazwa sana na Rais Mkapa, hivi umeona wapi duniani rais akaenda kufanya kampeni katika uchaguzi au uchaguzi mdogo, umeona wapi rais anaingia kwenye uchaguzi kupiga kampeni, hakuna sehemu yoyote, nimesikitika sana. Leo nakupatia tena milioni 100. Pia nitatoa visima kumi na baiskeli mia moja za walemavu kwa ajili ya CHADEMA.

"I am praying hopefully for you, tumechoka na CCM miaka hamsini...huyu huyu huyu...nimewaambia msitazame rangi yangu tazama upendo wangu, Dokta Slaa I am proud of you. Naangalia moja ya majengo yangu pale niwapatie muweke ofisi...kwa fedha hizi mnaweza kujenga ofisi," alisema Mzee Sabodo.

Akishukuru kwa msaada huo, Katibu Mkuu Daktari Slaa alisema kuwa CHADEMA kinatambua dhamira ya dhati ya Mzee Sabodo katika kutetea haki za Watanzania kupambana na ufisadi na kudai uwajibikaji wa watawala kwa wananchi.

Alisema kuwa fedha hizo zitaingizwa katika akaunti ya M4C ili zitumike kwa kwa ajili ya kupigania mabadiliko makubwa ya kupata uongozi utakaotumikia Watanzania.

"Kwa niaba ya CHADEMA, kwa niaba ya Mwenyekiti Freeman Mbowe, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu, kwa niaba ya Nassari aliyekuwa mgombea wetu Arumeru Mashariki, nakushukuru kwa dhati kabisa kwa moyo wako daima wa kukichangia chama chetu. Umekuwa ukifanya kwa uwazi kabisa bila siri, bila kumwogopa mtu.

"Hii inatokana na ukweli kuwa dhamira yako ni safi, uadilifu wako, usafi wako na moyo wako wa dhati wa kuwatumikia Watanzania...kama ni mtu mwenye dhamira mbovu au aliye mwovu usingeweza kufanya haya. Umewakumbuka hata walemavu ambao ni marginalized group,nasi tutafanya utaratibu wa kuzikabidhi kwa wahusika. Kwa upande wa visima utaratibu utawekwa pia angalau kila kata kulingana na jiografia ipate kisima, maana ziko kata 17," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Dkt. Slaa alisema kuwa hata wao CHADEMA walishangazwa kuona rais mstaafu akienda kupigia kampeni chama cha siasa, tena akidiriki kusema uongo badala ya kuwa mlezi wa taifa, akiongeza kuwa chama hicho kinafikiria kuandaa hoja kupeleka bungeni juu ya namna ambavyo viongozi wastaafu wa serikali wanapaswa kuenenda, huku wakiishi kwa pensheni inayotokana na kodi za Watanzania wote.

"Pamoja na hayo wananchi wamemkataa, tena wamekwenda mbali hata kumkamata kiongozi wa CCM akitoa rushwa kanisani...hii inaonesha kuwa yale ambayo CCM wamekuwa wakisema juu yetu kumbe wao ndiyo wanayoyafanya ya kubebwa na madhehebu ya dini. Wananchi wengi wamewachoka sasa, miaka 50 si kwa sababu wanapendwa na watu bali kwa sababu wanatumia nguvu ya polisi, dola na serikali, lakini haki ya watu inacheleweshwa tu lakini haiwezi kuzuiwa," alisema Dkt. Slaa.
 
Back
Top Bottom