Elections 2010 Sabodo aichangia CHADEMA Milioni 100 (tena)

Sabodo ndie nakumbuka mtu wa kwanza kufichua ukwepaji wa kodi kwa kampuni za simu!hembu tujiulize kwenye top ten large tax payers vodacom wapo nafasi ya ngapi?cha kushangaza voda eti ina wateja 10m,zain 5m lakini zain ipo kwenye top 5.sabodo keep it up!!!
 
big up mzee Sabodo kwa kuwa muwazi tofauti na wafanyabiashara wengine ambao wapo ccm kinafiki kwa ajili ya kulinda biashara zao haramu na ukwepaji wa kodi
 
Naomba mods mdhibitishe habari hii. samahani mleta hoja, nimekugongea thanks, usimindi ila habari hii ni nzito inahitaji nguvu kwani huenda zikaongezeka soon.

Kama dakika kumi zilizopita Mlimani TV wamemuonyesha Sabado akisaini hundi ya million mia moja kwa Chadema. Hii ni habari ya kweli.
 
TAARIFA HABARI YA USIKU ITV - MZEE ABDALLAH SABODO (Mwana-CCM tangu enzi za Baba wa Taifa) amekimwagia tena Chama cha Ukombozi wa Tanzania - CHADEMA mamilioni yapatayo 100 kwa ajili ya kukamilisha ukombozi wa Taifa hili.

MALAIKA WA MUNGU WANAZIDI KUJIDHIHIRISHA katika kukamilisha harakati hii ya kulikomboa taifa la Mungu lililoharibiwa kwa muda mrefu.

Mzee SABODO, anafaa kuitwa ni 'BABA MLISHI WA TAIFA HILI...Mpambanaji na kipenzi cha Ukombozi wa nchi hii'.

Mchango wake na dhamira yake nyeupe ni Baraka kamili na hii inaashiria nini?

* CCM wamepigwa na 'anguko kuu', na uchochezi wao eti CHADEMA ina mambo ya udini au ukabila ni kwamba wame-expire, maana Sabodo ni Muislam kamili, mzaliwa wa Lindi (na sio Kilimanjaro kama Mbowe au Ndesa) - na yeye ni mpinga Ukabila toka enzi za Baba wa Taifa, ndio maana yeye na Baba wa Taifa walikuwa pete na kidole. Kamwe hangeweza kutoa mchango kwa Chama chenye Ukabila au Udini!
* Wale Wafanyabiashara na Mafisadi wanaojipendekeza kwa CCM ndiyo wamepigwa na mshale wa moto kuwaonyesha kuwa Taifa litapata ukombozi kupitia gharama halali na nguvu halali ya Umma unaochangiwa na mtanzania wa kila rangi bila ufisadi.
* UCHOCHEZI SASA UMEFUNIKWA NA CHADEMA ni Chama cha Watanzania wote wenye dhamira njema, na hivyo kila mwenye Utashi mwema anapaswa kuutoa urithi au jasho lake halali kustawisha mafanikio ya Ukombozi na ujenzi wa Taifa letu na sio kupindisha ukweli, hila na unafiki.

SABODO_Mpambanaji.jpg

MUNGU IBARIKI NCHI YETU, MBARIKI MKOMBOZI - DR SLAA, MJALIE MZEE SABODO NGUVU TELE, APATE KUFURAHIA UTAWALA MPYA UJAO ULIOJAA UMAKINI, AMANI NA USTAWI.
 
Mungu mbariki kizee huyu aendelee kupata afya njema audhurie ubarikio wa rais mpya. Amen
 
Duh, Ama kweli za wizi 40. Mimba ni miezi 9 tu. Maana TZ ilikuwa mjamzito inapata uchungu. Mtoto anapatikana 31.10.2010
 
Mzee huyu anaonekana ni kati ya wafanya biashara wasafi kwani huwezi kuthubutu kutoa mchango kwa upinzani ukiwa na madoa.
Yashindikana hata wasafi wanatafutiwa madoa kama wakionekana wako karibu na upinzani. Itakuwaje wanaosaidia upinzani kwa wazi? Hongera baba yetu.
Mfano wa kuigwa hakuna udini hakuna ukabila wakristo na waislamu tumekuwa ndugu na kitu kimoja. Siasa za makabila na dini zimetokea kipindi hiki tu kwa sababu ya kutafuta hoja nyepesi.
 
Habari nilizosikia hivi punde ni kuwa Mustafa Sabodo amekipatia tena Chama cha Chadema Tsh milioni 100. Hii inaonyesha jinsi gani Chadema inakubalika. Sijui ingekuwaje kama mtu mwingine angetoa hii.
 
Hakua na haja ya kwenda kwenye vyombo vya habari... Huyu mzee anazeeka vibaya
 
Mzee huyu anaonekana ni kati ya wafanya biashara wasafi kwani huwezi kuthubutu kutoa mchango kwa upinzani ukiwa na madoa.
Yashindikana hata wasafi wanatafutiwa madoa kama wakionekana wako karibu na upinzani. Itakuwaje wanaosaidia upinzani kwa wazi? Hongera baba yetu.
Mfano wa kuigwa hakuna udini hakuna ukabila wakristo na waislamu tumekuwa ndugu na kitu kimoja. Siasa za makabila na dini zimetokea kipindi hiki tu kwa sababu ya kutafuta hoja nyepesi.

Mungu anamleta malaika wake toka katika upande wowote...
Ndio maana tunasema CCM miti yote inateleza kwa sasa
Sera zao kusambaza uchochezi eti udini na ukabila, mwenyezi Mungu anazidi kuwapiga kofi la mdomo...

Na muda unafika pale watakapoomba utulivu na amani watakaposhindwa ili uchochezi wao usichukuliwe hatua...ICC itakuwa palepale, watafikishwa tu kama amani itavurugika...
 
Angechangia CCM usingemwita GABACHORI!! Magabachori unawajua KIBUNANGO ni wakina Manji, Subash Patel,,Dewjis na Rostam bana !!Huyu babu ni mzalendo wa kweli mambo yake hafichi wala sio mnafiki na ndio maana hamumpendi!!

hii ni ishara njema: masikitiko yangu ni kuwa hivi vijisenti vinaishi mashavuni mwa MAFISADI WACHACHE wa chadema kwani hata wagombea ubunge hawapati kitu.
 
Habari hizo ni kweli kabisa.


Kutangaza n muhimu sana, inahamasisha watu wengine kuchangia zaidi, pia ni sehemu mojawapo ya Transparency. Ningependekeza zielekezwe kwenye uhamasishaji wa wapiga kura na ulinzi/uangalizi wa kura
 
hakuna mtu asiyeona mchango wa huyu mzee wetu ktk kuelekea uhuru kamili wa taifa letu baada ya mateso ya miaka 50 ya uhuru wa bendera chini ya serikali ya chama kizee,tupendekeze aina ya title ya tunzo ya kumpa huyu mzee wetu watanzania
 
Tumuenzi kwa kumweka kwenye orodha ya mashujaa wa Nchi hii kwa mchango wake wa kijasiri wa kukuza demokrasia ya vyama vingi ndani ya nchi yake...........
 
Back
Top Bottom