Sabena coach iliyochinja 17 hii hapa!

Kassim Awadh

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
884
187
KAMANDA[1].png AJALIYASABENA[1].png

Basi la Sabena lililokuwa likitokea Tabora kuelekea Mbeya limeanguka eneo la Kitunda wilayana Sikonge na kuua abiria 17 na kujeruhi 78. Kamanda wa Polisi afande Rutta akiongea na wanahabari akiwa eneo la tukio
 
kuna waliopona? waliponaje jamani? lol so sad ,,hii ajali hapa lazima kuna uzembe wa hali ya juu sana
 
kuna waliopona? waliponaje jamani? lol so sad ,,hii ajali hapa lazima kuna uzembe wa hali ya juu sana

Hiyo basi ilipakia zaidi ya abiria tisini na ikapita humohumo barabarani ambamo polisi wanasimama na kukagua lakini policcm utawasikia wakisema ilikuwa kwenye mwendo kasi
 
kwa mujibu wa taarifa ambazo zilitolewa na Polisi chanzo ni kushindwa kufanya kazi kwa kidhibiti usukani(staring rod) ikapelekea gari kukosa muongozo
 
Picha za ajali hiyo
 
Attachments

  • 1408470388070.jpg
    1408470388070.jpg
    12.9 KB · Views: 698
  • 1408470406147.jpg
    1408470406147.jpg
    21.5 KB · Views: 637
  • 1408470422348.jpg
    1408470422348.jpg
    18.8 KB · Views: 639
Jamani punguzeni kufanya biashara na uchawi munawamaliza WaTz

Tajiri analoga gari lake lipate abiria, madereva na makonda nao ni wachawi wanataka waendelee kufanya kazi duh tutapona kweli?
 
Jamani punguzeni kufanya biashara na uchawi munawamaliza WaTz

Tajiri analoga gari lake lipate abiria, madereva na makonda nao ni wachawi wanataka waendelee kufanya kazi duh tutapona kweli?

Sio uchawi wala nini ni uzembe tu wamadereva wanaendesha mwendo mkali mno bila kuchukua tahadhali wala kufuata sheria za barabarani!mara nyingi ajali za uso kwa uso ni uzembe tu!RIP marehemu
 
Sio uchawi wala nini ni uzembe tu wamadereva wanaendesha mwendo mkali mno bila kuchukua tahadhali wala kufuata sheria za barabarani!mara nyingi ajali za uso kwa uso ni uzembe tu!RIP marehemu

Mwendo wa kasi sana, kutofuata sheria za barabarani na kubwa ni uchakavu wa magari yenyewe. Hayo malori yaliyowekwa body za mabasi ni majanga.

Jaribu kuangalia number ya ajali zikizokuwa zinatokea Dar - Arusha na Dar - Songea. Utagundua kwamba zilikuwa nyingi sana hapo kipindi cha nyuma. Sasa hivi wamiliki wengi wameuza yale magari ya kizamani ambayo yalikuwa malori machakavu yaliyowekewa body ya bus. Sasa hivi wanamiliki Macopolo, benzi na mabasi ya kichina ambayo ni mabasi halisi kwa specification za kitaalam.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom