sababu zilivoanzisha vurugu katika kijiji cha Ndago jimbo la Iramba magharibi mkoani Singida

Asubuhi naamka na kwenda kazini na kukuta Hiace inayomilikiwa na mtu anayeitwa California ikiwa imepaki.

Mara naona vijana wanaofanya kazi katika shimo la dhahabu la mtu aitwaye Omary wakielekea kwenye Hiace hiyo na kupanda.

Niliposogea, niliona vijana hao wakiwa wanavuta Bangi huku wakiwa wamewasha udi.

Mara gari liliondoka na lilipofika Misigiri likapaki kwenye Bar/Grocery moja iitwayo Manka. Hapa vijana walianza kunywa pombe aina ya Konyagi. Na baada ya muda gari liliondoka na kuelekea Ndago.

Punde nitawaletea picha za gari, eneo lao la kazi, vijana na Bar waliyokuwa wanakunywa Konyagi.

Source: nilikuwepo eneo la mgodini.
Taarifa hii inatia shaka hasa pale unaposema ulikuwepo mgodini. Huu mgodi uko mbali sana na Misigiri......wewe ulijuaje kama gari ilisismama Misigiri na hao vijana kunywa konyagi? inawezekana wewe ni mmoja wa wale walioshiriki tukio hili maana ni vigumu kwa mtu aliye kilometa karibu 40 kujua details za safari hiyo.. Wewe lazima ni mmoja wa wale
 
Mkutano umeandaliwa na Chadema laikini wasikilizaji ni wananchi wote. CUF,CCM,TLP,NCCR Na wasio na vyama lazima waende kwenye mkutano wa chama chochote kinachotaka kutwaa madaraka. hivyo siyo sahihi kuhoji CCM wamefuata nini kwenye mkutano wa CHADEMA. ingekuwa chadema wanajihutubia wenyewe tu then hakuna haja hata ya kuzunguka kufanya mikutano. maana lengo mojawapo la mikutano ya siasa ni kushawishi watu wa vyama vingine na wasio na vyama waunge mkono chama husika katika kusaka madaraka. so wanapopata wasikilizaji wengi toka vyama vingine ndiyo mafanikio ya mkutano.
 
Asubuhi naamka na kwenda kazini na kukuta Hiace inayomilikiwa na mtu anayeitwa California ikiwa imepaki.

Mara naona vijana wanaofanya kazi katika shimo la dhahabu la mtu aitwaye Omary wakielekea kwenye Hiace hiyo na kupanda.

Niliposogea, niliona vijana hao wakiwa wanavuta Bangi huku wakiwa wamewasha udi.

Mara gari liliondoka na lilipofika Misigiri likapaki kwenye Bar/Grocery moja iitwayo Manka. Hapa vijana walianza kunywa pombe aina ya Konyagi. Na baada ya muda gari liliondoka na kuelekea Ndago.

MAHUSIANO YA WACHIMBAJI HAO NA MH. MWIGULU.

Itakumbukwa kuwa eneo la Mgodi wa Mgongo/Sekenke lilikuwa na mgogoro kati ya wachimbaji hao na mtu mmoja anayeitwa John Binna. Huu mgogoro ulirushwa kwenye Media mbalimbali ikiwemo TBC kama mtakumbuka.

Mgogoro huu uliingiliwa Mh. Mwigulu na kuamuru Mgodi hao wa dhahabu uchimbwe na WAPIGA KURA WAKE.

Hivyo hata leo Mh. Mwigulu akija na kuwaambia twendeni Ndago mkafanye fujo, sidhani kama wachimbaji watakataa.

Punde nitawaletea picha za gari, eneo lao la kazi, vijana na Bar waliyokuwa wanakunywa Konyagi.

Source: nilikuwepo eneo la mgodini.

Mnaweweseka sana ila ni lazima mtambue hiyo ni damu ya mwanaadamu haiwezi kwende bure hata mtumie njia gani kupotosha ukweli BWANA WA MAJESHI atawaumbua tu
 
Magamba hawana jipya zaidi ya kufanya uharamia kwa maisha ya watanganyika then kusingizia cdm.Hawa ni vilaza wameishiwa na sera
 
califonia yule pale kiomboi?
yule mwenye malandrover?
kwa manka hii grocery karibu na mirimo duu.
 
Mhhh! itakuwa ngumu kuwaaminisha akina Burn Karudi, Ritz, masopakyindi, Tume ya Katiba, MAFILILI, Mwigulu LM Nchemba.
hebu iweke hii taarifa yako kama ushahidi

Mkuu mimi najaribu kuwa fair kwa nafsi yangu katika mambo yote humu JF, na si mnazi bila kuyapima mambo.

Suala la Ndago huko Singida pamoja na utata wa mazingira yake , ni la kulaaniwa na Mtanzania yeyote kutokana na mauaji ambayo sasa yanaonekan dhahiri kuwa ya kisiasa.

Kitu cha kunote hapa ni kuwa kuna vijana(wa UVCCM inavyoonekana, sina uhakika) walikodiwa kuelekea uwanja wa mkutano wa CHADEMA kwa nia ya kufanya fujo.
Hili si suala la kistaarabu katika miaka hii ya vyama vingi.

Na bado tutabaki tukijiuliza kuwa wauaji haswa walikuwa nani, ni wale waliowapeleka hao vijana wakdhurike? au wale waliowadhuru kwa kuwaua?
Polisi wachunguze na wote watiwe hatiani kwa mauaji.
 
Asubuhi naamka na kwenda kazini na kukuta Hiace inayomilikiwa na mtu anayeitwa California ikiwa imepaki.

Mara naona vijana wanaofanya kazi katika shimo la dhahabu la mtu aitwaye Omary wakielekea kwenye Hiace hiyo na kupanda.

Niliposogea, niliona vijana hao wakiwa wanavuta Bangi huku wakiwa wamewasha udi.

Mara gari liliondoka na lilipofika Misigiri likapaki kwenye Bar/Grocery moja iitwayo Manka. Hapa vijana walianza kunywa pombe aina ya Konyagi. Na baada ya muda gari liliondoka na kuelekea Ndago.

MAHUSIANO YA WACHIMBAJI HAO NA MH. MWIGULU.

Itakumbukwa kuwa eneo la Mgodi wa Mgongo/Sekenke lilikuwa na mgogoro kati ya wachimbaji hao na mtu mmoja anayeitwa John Binna. Huu mgogoro ulirushwa kwenye Media mbalimbali ikiwemo TBC kama mtakumbuka.

Mgogoro huu uliingiliwa Mh. Mwigulu na kuamuru Mgodi hao wa dhahabu uchimbwe na WAPIGA KURA WAKE.

Hivyo hata leo Mh. Mwigulu akija na kuwaambia twendeni Ndago mkafanye fujo, sidhani kama wachimbaji watakataa.

Punde nitawaletea picha za gari, eneo lao la kazi, vijana na Bar waliyokuwa wanakunywa Konyagi.

Source: nilikuwepo eneo la mgodini.
tunasubiri picha mkuu!
 
Mkutano umeandaliwa na Chadema laikini wasikilizaji ni wananchi wote. CUF,CCM,TLP,NCCR Na wasio na vyama lazima waende kwenye mkutano wa chama chochote kinachotaka kutwaa madaraka. hivyo siyo sahihi kuhoji CCM wamefuata nini kwenye mkutano wa CHADEMA. ingekuwa chadema wanajihutubia wenyewe tu then hakuna haja hata ya kuzunguka kufanya mikutano. maana lengo mojawapo la mikutano ya siasa ni kushawishi watu wa vyama vingine na wasio na vyama waunge mkono chama husika katika kusaka madaraka. so wanapopata wasikilizaji wengi toka vyama vingine ndiyo mafanikio ya mkutano.

sawa ila kama hao wa ccm wametumwa kufanya vurugu je unategemea ni kitatokea mkuu??
 
ukiona baba anaiba mayai nyumbani na kuiba mboga ya ugali wa familia jioni jua mama karibia atapata mume mwingine.
haivumiliki.
 
*NI KATIKA MKUTANO WA MNYIKA,MWENYEKITI WA KATA UVCCM AUAWA,18 WAJERUHIWA

Raymond Kaminyoge, Dar na Gasper Andrew, Singida VURUGU kubwa zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara zikiwahusisha wafuasi wa Chadema na CCM zimesababisha kifo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wa Kata ya Ndago, wilayani Iramba, Yohana Mpinga (30) na majeruhi mmoja.Wafuasi hao wa Chadema na CCM walishambuliana kwa kutumia silaha za jadi ikiwamo mawe, wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa unahutubiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kifo cha mwenyekiti huyo baada ya kupigwa kwa silaha za jadi.Kamanda Sinzumwa alifafanua kwamba, kutokana na tukio hilo, jeshi hilo linawashikilia watu 18 wa kata hiyo kwa mahojiano zaidi na watakapobainika kuhusika na ghasia hizo watafikishwa mahakamani.Alisema majeruhi huyo wa vurugu hizo anayejulikana kwa jina la Ramadhani Hussein (27), amelazwa katika Kituo cha Afya cha Ndago baada ya kujeruhiwa vibaya.

"Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Julai 14 mwaka huu saa 10 alasiri katika Kijiji cha Ndago," alisema Kamanda.Alisema siku ya tukio, Chadema kilikuwa na kibali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho na mgeni rasmi alikuwa Mbunge Mnyika.Kamanda Sinzumwa alisema kuwa, baada ya Chadema kuanza mkutano huo, viongozi wake walianza kutoa kashfa mbalimbali dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwingulu Nchemba.

Alisema kitendo hicho kiliwaudhi baadhi ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo."Wananchi hao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao na walianza kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala yake, wakawataka Chadema wawe wanaeleza sera zao na si vinginevyo," alisema.Kamanda huyo alisema licha ya tahadhari hiyo, viongozi hao waliendelea kueleza kashfa za Mbunge Nchemba na ndipo vurugu zilipoanza.

Alifafanua kwamba, vurugu hizo zilianza baada ya wafuasi wa CCM waliokasirishwa na kashfa zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Chadema kuanza kuwarushia mawe wafuasi wa Chadema. Kamanda Sinzumwa alisema askari polisi wachache waliokuwapo, walizidiwa nguvu na makundi hayo."Huyu Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, Yohana alikimbilia kwenye nyumba ya Mwalimu Shume Manase ili kuokoa maisha yake, lakini kundi la wafuasi wa Chadema wakiwa wamebeba fimbo na mawe, walimpiga sehemu mbalimbali mwilini na kusababisha kifo chake papo hapo," alisema.

Kamanda huyo alisema licha ya watuhumiwa 18 kukamatwa, polisi bado inaendelea na msako wa kuwatafuta watu wengine waliohusika katika tukio hilo ili wafikishwe mahakamani.Kauli ya MnyikaAkizungumzia vurugu hizo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema mbinu chafu zinazotumiwa na CCM za kupiga mawe mikutano yao ya hadhara kamwe haitakidhoofisha chama chao katika harakati zake za kuwakomboa wananchi kutoka katika maisha magumu.

Mnyika alisema amefurahi kufika katika jimbo hilo la Mbunge Nchemba kwa sababu ya propaganda zake, ambazo amekuwa akizitoa bungeni na alivyofanya ziara kwenye jimbo lake la Ubungo na kuwahutubia watu wa Manzese.Mnyika alisema wakati wowote kuanzia sasa viongozi wa juu wa chama hicho watafanya ziara kwenye kata zote za Mkoa wa Singida ili, kuwafahamisha wananchi hatua za kuchukua katika uchaguzi ujazo

Mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam,John Mnyika,kizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika juzi katika kijiji cha Ndago jimbo la Iramba magharibi mkoani Singida
 
Masopakyindi! Sasa polisi wafanye uchunguzi au wachukuliwe hatua? C walikuwepo mkutanoni? Walifanya nn?
 
Polisi inabidi wasimshikilie yeyote, inaokekana walikuwa mashabiki wa mambo yaliyokuwa yanaelea ie vurugu! Picha tafadh
 
Mwananchi siku izi wanacopy and paste,,hakuna kuinvestgate chanzo cha habari.HAPA WANAWAFURAHISHA serikali.na pia it seem kwamba hata RPC alikuwa anajua hii movie kabla..
 
Mwananchi siku izi wanacopy and paste,,hakuna kuinvestgate chanzo cha habari.HAPA WANAWAFURAHISHA serikali.na pia it seem kwamba hata RPC alikuwa anajua hii movie kabla..matusi yaanikwe ambayo MWIGURU katukanwa
 
Kamanda wa Polisi kwa maelezo yaliyoletwa na mleta mada, ni kwamba anathibitisha wafuasi wa CCM ndio walioanza kurusha mawe kwenye mkutano wa CHADEMA, jambo lililopelekea CHADEMA kujibu mashambulizi vikali hadi kusababisha kifo. Nina maswali machache kwa Kamanda, naomba watu wa Singida mumfowadie maswali haya:-

1) CCM walienda kufanya nini kwenye mkutano rasmi wa CHADEMA?

2) CCM wasingerusha jiwe hata moja, mauaji yangetokea?

3) Ni wafuasi wangapi wa CCM waliokamatwa hadi sasa kwa kosa la kuanzisha vurugu (kurusha mawe)?

4) Anayetakiwa kushughulikiwa wa kwanza kisheria ni yupi, aliyechokoza kwa kurusha mawe au aliyejibu mashambulizi ya mawe kwa kutoa kichapo?

5) Matusi yanayodaiwa kutukanwa Nchemba suluhu yake ni mawe au kumshitaki Mahakamani mtukanaji?

6) Walichokifanya CCM (kurusha mawe) ni hatua sahihi kisheria dhidi ya mtukanaji (if any)?
 
Back
Top Bottom