Sababu za wabunge kupinga na kuunga mkono hoja wasizozijua

The Worshiper

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
302
89
Ni wakati wa vikao vya Bunge hapa mjini Dodoma,mji huwa katika hekaheka na pilikapilka nyingi huku idadi ya watu ikiwa imeongezeka.Kuongezeka huku kwa idadi ya watu husababisha pia msongamano wa hapa na pale siyo tu barabarani lakini pia maeneo tulivu watu/wageni wanapofikia (Guests houses,hotels,Logdes nk)kwa ajili ya kujipumzisha ama kumalizia viporo vya shughuli zao mara baada ya zile za msingi za mchana kutwa.

Lakini jambo moja ambalo huwa limekuwa likinishangaza,kuniumiza kichwa na kujiuliza mara kwa mara ni juu ya u-seriousness wa miongoni mwa hawa wawakilishi wetu Bungeni(Wabunge).Kwa kawaida Mbunge yeyote(kama mwakilishi wa wananchi) ana wajibu na uwezo wakati wowote kwa sababu maalum wa kupata nyaraka,ripoti na mikataba mbalimbali inayohusu shughuli na maswala mbalimbali yanayoendelea nchini.Mara nyingi ni rahisi baada ya wao kuondoka katika maeneo waliyokuwa wamefikia(Guests houses,hotels,Logdes nk) kukuta nyaraka mbalimbali za vikao vya ndani(vikiwa vimetelekezwa) ambazo kwa mtazamo wangu ni highly confidential kujulikana kabla na mtu wa kawaida, lakini utakuta wakati mwingine zipo mikononi mwa wahudumu wa haya maeneo.

Nyingine ukiangalia kwa makini utagundua kabisa tangu zihifadhiwe zilikuwa hazijaguswa kabisa hali inayoonyesha kwamba wengi wa wawakilishi wetu hawa wamekuwa siyo wasomaji na wapitiaji wazuri wa nyaraka na repoti hizi (wavivu) ingawa ni wazuri katika kuzirundika,hivyo ukiangalia wakati wakupresent bungeni wengi wao huwa wanaishia kuunga mkono au kuwapinga wale wanaoonekana kuwa ni wasomaji,wachambuzi na wapitiaji wazuri.Kwa lugha rahisi unaweza kusema ni kama huwa wanasubiri kwa hamu vikao viishe waondoke.Hii inanipa picha kwamba kama ni mfuatiliaji mzuri unaweza ukawa unajuwa mambo mengi ya siri kuliko mwakilishi wako.Swali, Ni nini maana ya kuwa mwakilishi wa wananchi? Unaweza kumpima pia mwakilishi wako.


Naomba kuwasilisha.
 
Kwa wabunge wetu issue siyo hoja bali posho na mshikamano wa kifisadi na kizalendo (wapinzani). Wanawakilisha matumbo yao na si majimbo yao.
 
Sasa kama mbunge ni kilaza wa STD 7 au Form 4, unategemea atasumbua ubongo wake kuanza kuchambua hoja za kwenye vitini....
 
mkuu umenena. nakumbuka wakati wa uongozi wa mzee wa standard and speed aliandaa programu ya kila mbunge awe na laptop. wakapewa wabunge wachache kwa majaribio.

mrejesho ulivyokuja ili kuangalia ufanisi wa zoezi hilo, ikaja onekana ufanisi ni sifuri. laptot karibu zote either zilikutwa zimeharibika kwa kumwagiwa BEER,KONYAGI NA CHAI. Kwa hiyo sishangai kukuta classified documents mikononi mwa wahudumu wa baa tena nyingine zina madoa ya hivyo vinywaji tajwa hapo juu. mbunge anapitia document huku anapata beer, what do you expect? Ni ndioooo. Nadhani waliosema ndio wameshinda.
 
  • Thanks
Reactions: awp
Back
Top Bottom