Sababu za wabunge kudai nyongeza za posho kila kukicha hizi hapa

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Sababu kuu za wabunge kudai nyongeza za posho kila kukicha ni hizi hapa;
  1. Kwanza ni uelewa mdogo wa wananchi juu ya kazi za mbunge, pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuianisha wazi kazi za mbunge, watanzania wengi hawazijui kazi za mbunge. Wantazania wengi hufananisha kazi za mbunge na zile za serikali au wafadhiri, hii hupelekea kumubebesha mbunge kazi za serikali na wafadhiri. Ukosefu wa huduma za afya maji, elimu, barabara, umeme n.k hudhani hutokana na kuwapo mbunge dhaifu katika eneo husika.
  2. Kuwapo kwa serikali dhaifu sana, kuwapo kwa serikali isiyoleta maendeleo husababisha wabunge kupata lawama kubwa kutoka kwa wananchi wake. Serikali kushindwa kuleta huduma nzuri iwe katika afya, elimu n.k husababisha wananchi kuwabebesha wabunge lawama sana.
  3. Tatu ni wananchi kukabiliwa na umaskini ulikithiri, hii husababisha watu kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya kifedha. Ili kujikwamua na matatizo hayo huhitaji ufadhiri kutoka kwa watu mbalimbali.
Kutokana na sababu nilizoeleza hapa juu, wabunge hulazimika kutafuta pesa zao binafsi ili zitumike katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kazi ambazo zingefanywa na serikali au washirika wa maendeleo. Hii husaidia kuepuka kupata lawama za wapiga kura wake. Wabunge wengi wanaosifiwa ni wale ambao maeneo yao serikali ilipeleka au inapeleka maendeleo Wabunge wenyewe wamekuwa wafadhiri. Njia kwao rahisi ya kuongeza posho ni madai ya nyongeza za posho.

Wabunge hulazimika kudai posho kubwa ili sehemu ya fedha hizo zisaidie kutatua baadhi ya matatizo binafsi yanayowakabili wananchi kama ada za shule, kughalimia matibabu, chakula n.k.

Lawama wanazopata wabunge wengi kuwa hawajafanya lolote katika maeneo yao ni matokeo ya serikali kushindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wake. Lawama inaweza kuwa kwetu sisi wenyewe wananchi kushindwa kutengeneza serikali madhubuti. Nakaribisha michango zaidi sio matusi.
 
tatizo jingine ni kuwa hatuna mifumo mzuri wa kuendesha mambo yetu. mifumo ya malipo hapa Tanzania ni kama haieleweki vema. Wabunge wanapata mwanya wa kuendelea kudai nyongeza za mishahara na posho kwa sababu hiyo. Tungekuwa na mfumo wa malipo kwa watumishi unaoeleweka na kuheshimika, wala tusiongeona matatizo kama haya.
 
hakuna kitu kama hicho ni ubinafsi wao na kumpa kazi nzito Rais ambaye bado ana kazi ya kuboresha maeneo mengi yenye mahitaji
 
WABUNGE NI WASALITI, hawafanyi kile tulichowaagiza, wapo pale kwa ajili ya matumbo yao! Kama maisha magumu sote twakabiliana nayo!
 
Tunasubiri kauli ya chadema ndio wamelivalia njuga sana suala la posho hadi hawaelewani wao kwa wao kadhalika mwenyekiti wa chadema na baadhi ya wafuasi wake
 
Tanzania bunge ni branc la serikali hivyo ni haki kulaumiwa kwa kutoleta maendeleo katika majimbo yao.
Kuna mhimili mmoja tu serikali
 
Wabunge kazi yao iwe kuwachochea wananchi waidai serikali maendeleo siyo wao kuomba posho kwa ajili ya kuwapa wananchi. huu ni ujinga mbunge hawezi kuwagawia wananchi pesa ni ujinga na ujinga wa hali ya juu. Hoja zao ni dhaifu sana wakati serikali inayopashwa kulaumiwa na kuwajibishwa iko kimya ikwasakizia wabunge.
 
Huyu selasini wa chadema amekuja na hoja dhaifu sana za kutaka kuongezwa posho. Hivi anadhani anaweza kumaliza matatizo ya wananchi kwa fedha za maendeleo kupitia mikononi mwake lakini zaidi tutajuaje kama zitawafikia
 
Bunge linatenga fedha ya maendeleo je selasini wa chadema anataka kutekeleza mambo ambayo hayamo kwenye ahadi kwa kila jimbo? kama anataka zaidi kwa nini asijenge hoja za jimbo lake kuongezwa bajeti badala ya kutaka fedha hizo zipitiye kwenye akaunti yake binafsi kwa jina la posho? Je akizitafuna yeye au bunge yeyote tutajuaje kama zimefika kwa wananchi
 
hiyo ndio hasara ya kutoa ahadi nyingi kwa wananchi hata zisizotekelezeka au nyingine ziko nje ya ahadi za vyama vyao. Mtu binafsi (mbunge) unaahidi kisha unadai kusaidiawa kwa posho.
 
Selasini na wabunge wote mnaounga mkono kuongezwa posho kwa kisingizio cha kuzipelekeka kwenye maendeleo ya wananchi rudini kwenye majimbo yenu waeleze wananchi kile kilichotekelezwa kwenye ilani za chama watawaelewa. Maendeleo ni fedha na kila jimbo lina mgao waambie mgao wenu katika bajeti ya mwaka huu na mambo ambayo hujatekeleza katika mwaka huu wa fedha utayapigania katika bajeti ijayo.
 
wabunge punguzeni kutumia fedha nyingi kuupata ubunge mnalilia posho kuziba mapengo na hasara mliyopata
 
Wabunge mkitaka wananchi watambue kuwepo kwenu acheni kutatua matatizo ya mwananchi mmoja mmoja. Tatueni matatizo ya jumla kama vile maji, umeme, elimu na afya ambayo yanatengewa bajeti yake baada ya kila mbunge kujenga hoja za kupewa mgao bungeni kupitia wizara.
 
nguvu wanayotumia wabunge kushinikiza posho wangetumia katika kudai haki za wapiga kura wao ndani ya bunge tungekuwa mbali sana
 
wabunge ndio hawafanyi kazi yao barabara kwa wananchi kusudi waeleweke sio kweli kwamba wananchi hawajui kazi za wabunge. Wanafunzi anaweza asielewe kama hamwelewi mwalimu. Wabunge wetu warudi kwa wananchi na kufanya kazi yao ipasavyo tutawelewa lakini wakichaguliwa na kisha kukimbia majimbo yao majukumu yao hayataeleweka na wananchi.
 
Wasipotumia pesa nyingi kweli wataupata?. Maoni yako mengine tunashukuru sana. Selasini atakuwa amekusikia pia.
wabunge punguzeni kutumia fedha nyingi kuupata ubunge mnalilia posho kuziba mapengo na hasara mliyopata
 
Back
Top Bottom