Sababu za polisi kuiba maiti usiku mochwari na kukamatwa Lissu Tarime

Hawa kina Mwema ni suala la muda tu, lakini lazima siku moja nguvu ya umma itawasimamisha kizimbani. Na tuzo kwa utumishi wao shurti iwe kifungo.
 
Kuzisumbua maiti ni dhambi kubwa sana,wanaitajika kustiriwa jamani!kwanin wanadhalilishwa?subhanallah
 
Picha hii ni kielelezo kizuri cha taarifa.

Najiuliza; kwani polisi huwa na kawaida ya kuhakikisha ndugu wa marehemu wanaichukua miili na kuizika kwa wakati? Au hilo nalo ni jukumu jipya la kisheria kwa jesji la wahalifu (polisi)?

Kwa vyoyote vile, hakuna namna wala lugha ya kuspin unyama huu, ccm na serikali yake wanapaswa kujua hilo kabla mambo hayajazidi kuwa mabaya na hatari nchini Tz.

Hivyo napendekeza yafuatayo miongoni mwa mengine:-

1. Ufanyike uchunguzi huru na wa haraka juu ya mauji yote hapo Tarime.
2. Polisi na viongozi wote waliohusika wanajulikana (hata kama wamehamishwa au kustaafu), wakamatwe na kufunguliwe mashtaka ya mauaji mara moja.
3. Mahakama iwaachie huru wote waliokamatwa bila masharti yoyote na kufuta kesi hizo dhalili.
4. Shuguli katika eneo tata la mgodi zisimamishwe mara moja hadi hapo muafaka na haki itakapopatikana.
5. Serikali iombe radhi kwa umma wa Tarime na Tz kwa ujumla na pia ilipe fidia za madhila ya mauaji, hasara za kiuchumi, matibabu kwa walioathiriwa na sumu itokayo mgodini nk
6. Mikataba yote ya madini iandikwe upya, na iwe kwa lengo na maslahi ya MTz kwanza na pili Taifa kwa ujumla.
 
kwani msaada si waweza kuishia mhusika anapofika aendako?Hapa inaonekana Polisi walikuwa na root nyingine ikabidi wawashushe hapo karibu na kituo ambapo wangepata usafiri mwingine.Huo si ndio uzalendo jamani?wa kusaidiana kadri ya uwezo?Kwani hamkuridhika na msaada walioutoa Polisi?
 
Massawe kanywe kikombe wakurya huwawezi afya yenyewe mgogoro na uongo wote huo unaotunga loh
 
tatizo igp yupo kama picha...maagizo yote kuhusu polisi yanatolewa na ccm...to hell

Kwa kweli IGP alikuwa anakwenda vizuri na jeshi la polisi, tatizo ni hizo interferences za Magamba. As it is now hawezi tena kuwa objective na kufanya kazi professionally kama ilivyokuwa nia yake ya dhati. Ameshaona lesson nzuri tu kutoka kwa Tido Mhando. My take ni kwamba IGP hayuko tayari kupoteza menu kwa ajili watu kunyimwa haki zao, as long as anapata chake basi maisha yanaendelea. Poor leaders.
 
napata shida kidogo na kujiuliza KWANINI NDUGU WACHUKUE MAITI USIKU? Na vipi ndugu hao waliochukua maiti na kusindikizwa na polisi vipi wazishushe maiti hizo barabarani?

kazi ipo Tarime.
 
Jamani.....
1. mimi sijawahi kuona maiti inachukuliwa Mochwari usiku... tena wa saa 4
2. Kamanda wa polisi anadai akina Mh. Lissu walienda kuzuia ndugu wa marehemu kuchukua miili, inakuwaje miili ichukuliwe saa 2 usiku? na kama ni kweli (wao Polisi wakaenda kutoa usaidizi) inakuwaje wakawakamata tena relatives wa marehemu?? Nao walizuia miili isiende kuzikwa?
3. Kama walishatoa usaidizi wa kutoa miili mochwari, kwa nini waliitelekeza barabarani? Ni kwa sababu ndugu wa marehemu walikuwa rumande na wao polisi hawakujua pa kuzipeleka hizo maiti

Hii ni dharau sana kwa marehemu wetu, lakini Mungu siku zote husikiliza kilio cha wanyonge, yote yana mwisho na huo mwisho hauko mbali...

Wananchi tumekosa imani na jeshi la polisi, juzi tu wamemuua yule dada askari eti kwa sababu kapoteza msafara wa rais. Askari wa Tarime ni Ma-Israeli, watoa roho za watu....

Amaaaaaaaaaaaaaaaaaaandla.......
 
napata shida kidogo na kujiuliza KWANINI NDUGU WACHUKUE MAITI USIKU? Na vipi ndugu hao waliochukua maiti na kusindikizwa na polisi vipi wazishushe maiti hizo barabarani?

kazi ipo Tarime.

Ndugu hawakuchukua maiti, Ndugu walienda Mochwari kuzuia polisi wasichukue miili ya ndugu zao. Polisi ndio walichukua Maiti na baadhi ya ndugu pia walikamatwa during the process wakawekwa lupango. Since polisi walikuwa hawajui pa kuzipeleka hizo maiti, then wakaamua kudi-dump
 
Je,makamanda wameshaachiwa kwa dhamana au? Sasa baada ya miili hiyo kutelekezwa na polisi wa magamba nini kilichofuata? wamezikwa? kuna siku watu wataanza kujitoa muhanga katikati ya maposi ndipo watakapojua watu sasa wamechoka na tabia chafu ya ukandamizwaji.Let us have the current news please!!!
 
Tanzania hakuna kiongozi mwenye akili katika Jeshi la Polisi.

Tangia lini Polisi kuwa na watu wenye akili! au umesahau kuwa watu wengi wanaoingia jeshi hilo ni wale walio feli FORM FOUR au wamechukua cheti cha mtu ili waweze kwenda MOSHI kujifunza upolisi!! si watukani lakini ukweli ndo huo. Watanzania hatupendi kuambizana ukweli najua kunawatu watakuja juu nitetee hoja yangu.
Ni kipindi hiki tu ndio tunaanza kuona vijana wakienda jeshi la Polisi wakitoka vyuo vikuu ila nao wanapigwa vita kama nini ili wasichukue nafasi za akina fulani na watoto zao.
 
constantine massawe ni muislamu?

Anaweza kuwa Muislam au Mkristu lakini nachojua asingeweza kutelekeza maiti barabarani bila IGP Said kujua pamoja na Mrisho maana ndio mabosi wake naye ni mtumishi tu anayetekeleza amri za mabosi wake ambapo kanuni za jeshi haziruhusi kupinga amri za bosi wako
 
SHAME ON YOU, Jeshi la Polisi.

It doesn't make sense at all, kuiba (hata ukiita kuchukua) maiti usiku, na kwenda kutupa/kutelekeza barabarani.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom