Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,452
Wanabodi,
Leo ndio siku ya Interview ya kujiunga na Shule ya Sekondary ya St. Marrian Girls Sec. School iliyopo Bagamoyo.
Interview hiyo inahusisha mtihani wa masomo matatu ya Hisabati, Kiingereza na Maarifa ambayo wataifanya kwa masaa 4 mfululizo. Imeelezwa mtihani huo ni mgumu mara 10 kumi zaidi ya mtihani wa taifa wa darasa la 7 uliofanyika wiki mbili zilizopita ili watakaofaulu ndio watakao chaguliwa kujiunga na shule hiyo.
Jumla ya waombaji ni 3000 wakigombea nafasi 150 tuu!. Kila muombaji amelipia fomu ya kujiunga kwa Sh. 15,000/= hivyo kwa zoezi hilo la interview pekee, shule hiyo imeshajiingizia Shilingi Miilioni 45 ya chap chap!.
Kufuatia interview hiyo, asubuhi ya leo imeanza kwa mashindano ya magari kuelekea Bagamoyo na mjini Bagamoyo penyewe ndio hapafai kabisa kwa makundi ya watu. Ziko familia zenye uwezo wamekuja na magari mawili kuanzia baba, mama, bibi, babu, mjomba, shangazi, na watoto wa familia wakimsindikiza mtoto kufanya interview as if wakiwa wengi basi mtoto wao ataongezewa maksi!.
Magari zaidi ya 1000 kuizunguka Marrian Girls ni kizungumkuti, hivyo Traffic police wametanda kuyaongoza magari kwa kuyazuia kukaribia eneo la shule hivyo wanafunzi kulazimika kutembea nusu maili kuifikia shule. Hao traffic wakiona gari za kipesa pesa ziliruhusiwa kupita ndani kwa kihisiwa ni waheshimiwa!.
Na tukirudi mitaani Bagamoyo leo, kila hoteli, kila mgahawa, kila kioski, kila chini ya mti kwenye kivuli ni parking za magari!. Waliokuja ki-pikiniki pikiniki, wamekuja,waliokuja ki beach beach wamekuja na mahotelini hakuna chochote watu wameshakomba kila kitu!.
Kwa wale watoto wa familia za kula kuku sio mpaka siku ya sikukuu au soda sio mpaka wakija wageni au mayai mpaka wakiugua na matunda mpaka waambiwe na dakitari, ile kutembezwa tuu nusu maili kabla ya kuingia chumba cha mtihani ndio elimination test yao ya kwanza kwa wanafunzi wenye uwezo wa wastani kufanya mtihani wakiwa huku wakiwa wamechoka na kutembes hivyo kupata uwezekano wa kufanya vibaya!.
Kwa idadi hiyo ya wanafunzi 3000 kugombea nafasi 150 inamaanisha watakaofaulu ndio top most cream hivyo wanakuwa ni wepesi kufundishika ukijumlisha na spoon feeding ya kutafuniwa kila kitu na wao kupewa kumeza tuu, then no wonder ni kwa nini St. Marrian Girls wanatoa Div 1 za darasa zima na kuongoza kwenye ufaulu kitaifa kipindi cha miaka kumi mfululizo!.
Swali kwa nyie wanafunzi wa kisasa ambao mmekutana na hivi vichwa vya Marrian Girls huko mavyuoni, jee ni vichwa kiukweli mpaka huko mavyuoni?.
Nakumbuka tukiwa UD shule zilizokuwa zikiongoza wakati huo zilileta nusu ya darasa kupiga Law. Tangu registration pale chini ya Mdigrii hadi faculty walikuwa wakipiga ung'eng'e tuu as if Kiswahili hawajui yaani hadi kucheka walikuwa wakicheka kizungu!. Hata ukimuuliza kitu kwa Kiswahili kwanza atakuuliza " what?" ili swali lako uliulize kwa Kiingereza na ukisisitiza kwa Kiswahili ndipo atajilazimisha kwa "you mean" nyingi na ma "what na what not" kibao ili mradi ni kiswanglish kwa kwenda mbele!. Sie wengine tukajisemea kimoyo moyo kumbe wenzetu wanaakili!. Kufika matokeo ya mwisho ya mwaka wa kwanza tuu, wanafunzi kumi naa wakapigwa Disco!, na wachache waliobakia nao wakalabwa disco mwaka wa pili, na sikumbuki hata ni wangapi walifanikiwa kumaliza ila tukikutana nao mitaani kwa sasa ni Kiswahili safi kwa kwenda mbele!.
UPDATE
Matokeo ya mtihani wa kujiunga Marrian Girls ya Bagamoyo yalitoka kesho yake Jumapili jioni kwa wazazi wa watoto wao walioshinda kujulishwa kwa simu na kesho yake Jumatatu asubuhi yalibandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa shule na kwenye ile ofisi yao iliyopo Msimbazi Center.
Jumla ya wanafunzi 120 ndio waliochaguliwa cut off point ni wastani wa marks 35 chini ya 50.
Nimeishuhudia marking scheme yao, mtihani wao sio tuu ulikuwa mgumu bali pia ulikuwa a bit tricky ili wanafunzi wale tuu wenye IQ above average ndio waliofaulu.
Nimethibitisha beyond reasonable doubt kuwa mchakato wa kuipata Marrian Girls ya Bagamoyo ni mchakato wa haki wenye maximum transparency na waliochaguliwa wote walistahili, hakuna upendeleo wa aina yoyote na hakuna deals.
Ila pia niliposoma majina ya ubini ya wengi walioshinda idadi kubwa ni majina ya watu kutoka makabila fulani fulani ambayo yanatambulika kirahisi. Lazima tukubali, tukatae, huu ni ukweli isiopingika kuwa japo Watanzania ni wamoja na hatuna ukabila, ila pia yapo makabila ambayo yamebarikiwa kwa wengi wao kuwa na akili kuliko makabila mengine.
Pia mtihani wa kujiunga na shule hii haukubagua dini, yaani watu wa dini zote wamefanya interview ila kwenye matokeo very very unfortunately majina mengi ni ya dini fulani na sikubahatika kuyaona majina ya dini nyingine!.
Mwalimu alipofanya affimative action ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za elimu, pia alitakiwa afanye vivyo hivyo kwa affimative actions ili watu wa dini wapate fursa sawa kupata elimu bora!
Naomba Kuwakilisha.
Pasco.