Sababu za kung'atuka uenyekiti jimbo la ubungo.

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Kuna watu wameandika thead ihusuyo kujiuzulu kwangu, ndani yake kuna ukweli lakini pia kuna upotoshaji wa baadhi ya mambo. Naomba nitoe maelezo sahihi.

Mimi nimekuwa mwenyekiti wa Chadema ubungo na mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni mwanachama ni nayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote.

Nilipoingia Ubungo baadhi ya viogozi waliokuwepo walikuwa wanakaimu nafasi zao ktk baadhi ya ngzi, nikamilisha chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba. Shahidi wa Yote haya Mbunge mwenyewe. Nilifanya naye kazi kwa karibu sana.
Kabla sijaja ubungo, ubungo kulikuwa na vurugu nyingi sana. Nilipochaguliwa kuwa Mkiti na baada ya waleta vurugu kutimuliwa na makao makuu. Ubungo tumekuwa moja hadi tukashinda chaguzi zote hizo za madiwani na ubunge chini ya Uongozi wangu.

MCHAKATO WA KUNG’ATUKA.
Nimewashirikisha wazee wa ubungo na secretariet ya jimbo chini ya Katibu wa Jimbo la Ubungo.
Baadaye nikakaa na viongozi wa kata zote. Wote wamenielewa.

Kuhusu kujiuzulu ubungo.
Mimi nimejiuzulu uenyekiti wa Ubungo 1/7/2011. Nakala nimempa katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na Katibu mkuu Taifa. Barua nilimwandikia katibu wa Jimbo la Ubungo.

Kwanini nimjizulu?
A)Nimehama kimakazi kutoka Ubungo, mtaa wa Kisiwani manisipaa ya Kinondoni hadi Manisipaa ya Ilala. Makazi yangu ya kudumu yatakuwa Kitunda. Sidhani kama ni busara nichome mafuta kutoka Ilala kwenda ubungo. It is a waste of Time and Money unnecessarily.
On the other hand, katiba ya Chadema inaniruhusu mimi kupima mwenyewe baada ya kuhama kimakazi-haisemi lazima nijiuzulu au lazima nibaki. Kwa hiyo, mimi nikaongea na wazee wa Jimbo la ubungo, wakanielewa.

B)Ubungo ni Imara kimtandao na kiungozi. Jimbo la ubungo lina Mbunge Mnyika na Madiwani wa kutosha (7) bila kutaja wabunge wawili ambao nao ni madiwani. Kamati ya utendaji Ubungo ina wajumbe kama Dr Kitila, Mbunge na Suzana Lymo. Si Busara kuacha jimbo la Ukonga ambako ndiko ninakotumia muda wangu mwingi na kuendelea kuja ubungo ambayo ni imara. Nimezunguka kata zote, za ukonga na nimegundua inahitajika uimarishaji. Baadhi ya viongozi waliopo (wakiwepo viongozi wa jimbo) wanakaimu nafasi zao. Busara ni mimi kuongeza nguvu ktk jimbo kama hilo.

C) Ubungo ina ruzuku ya zaidi ya Sh mil moja kwa Mwezi ( Ruzuku ya Chama na mchango wa Mbunge). Ukonga wana ruzuku ndogo sana – around laki mbili na kidogo. Kwa hiyo, Uongozi uliopo unaweza kujenga chama Ubungo wakishirikiana na madiwani na Mbunge bila mimi. Busara yangu ni kwamba sasa niende nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku ( kabla ya uchaguzi 2010) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya mwaka jana. Kwangu mimi huu ndio uamuzi wa Busara. Sitakiwi kung’ang’ania ubungo tena imara.

D) Viongozi na wanachama wa ukonga wameniomba nigombee ukonga,
Viongozi wengi na wanachama wa ukonga, baada ya kuona utendaji wangu walioniomba nigombee nafasi mojawapo ktk uchaguzi unaokuja hivi karibuni. Nikawakubalia. Hiyo nayo ni sababu mojawapo.

Mwisho;
Ni matumaini yangu kwamba yale mazuri tuliyoyafanya pamoja mimi na viongozi wenzangu watayaendeleza wenzangu wanaobaki.

ALUTA CONITINUA.

MIKAEL P AWEDA
 
Safi sana, lakini bora hili ungelijibu kule ambako wamekushutumu au walikotuma ile post ya kukutuhumu
 
Safi sana kijana , tunataka na viongozi wa CCm wanaposhutumiwa wawe wanakuja hapa kukana au kukubali. safi sana kaka
 
Kaka tumekuelewa sana na pia tunakutakia kila ka heri maana tulikuwa wote kipindi chote katika Ubungo Kibangu na pia haya yote ni makini kuja na kuongea ndani humo. Kweli kabisa umekuwa na Mnyika karibu sana katika harakati hizi umekuwa karibu sana katika kuhakikisha kuwa ubungo imekuwa imara sana
 
Safi sana, lakini bora hili ungelijibu kule ambako wamekushutumu au walikotuma ile post ya kukutuhumu

Asante, kule nako nimetoa maelezo haya haya, lakini nimeona mods wameyaondoa haraka sana.
 
Wwambie kuwa ubungo yupo mnyika na sio vibaya ukajipanga ukonga kwani 2015 sio mbali.
 
songa mbele, kumng'oa Mnyika ubungo ni kazi sana, nenda kajaribu bahati yako huko tuongeze majimbo, umesoma vizuri alama za nyakati
 
Vizuri sana. Chama hujengwa na wanachama. Kama unafanya haya yote kwa nia thabiti na wala si kwa sababu ya maslahi yako basi Mungu anaonajitihada zako. Na akujalie moyo wa kuenenda ktk njia iliyo njema ya kuijenga CHADEMA.

Big up Aweda. Mapambano bado yanaendelea na ndio yamepamba moto.
 
kaka songa mbele wala usitereke kwani si wote wanaoweza kukutakea meema katika hizi harakati za ukombozi
 
Safi sanna brother, chadema tunaitaji viongozi kama wewe.
Alafu napenda nidhungumze na ili kidogo, ni kweli sisi viongozi tumekuomba ugombee nafac ya M/Kiti coz Binagi anapwaya sanna. Tunakukubali sana hasa utendaji wako, unavyoweza kujenga hoja, uzoefu na ushawishi pia.

Katibu chadema tawi la Pugu Bombani
Godlisten Masawe.
 
hii iko powa mkuu.
sababu ya wewe kuhama kimakazi na kuwa na makazi ya kudumu kitunda ni ya msingi sana ambayo mimi naiunga mkono.
endeleza mapambano tupo pamoja saaaaaaaaaaaana. nimeambiwa hata segerea haina uongozi wa kudumu, saidia kote huko ikiwezekana.
 
Kila la kheri kwenye makao Mapya,na Mungu akujaalie afya njema na ushinde Uenyekiti na maanslizi mazuri ya 2015
 
Back
Top Bottom