Sababu za kumuunga Mkono Mwenyekiti Dkt Kikwete uchaguzi ujao wa CCM taifa

igwana123

Senior Member
Nov 8, 2010
175
25
Wana CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti Taifa katika uchaguzi wa Mwenyekiti mwezi ujao.
Sababu za kumuunga mkono Mwenyekiti Dkt. Kikwete ni pamoja na umahiri wake katika uongozi, busara na hekima katika kutoa maamuzi, sera zenye tija na kuongoza nchi kwa Amani na utulivu kwa kufuata haki za bianaadam. Kilikuwa kipindi kigumu kutokana na hali ngumu ya kiuchumi duniani, mabadiliko ya tabia nchi, majanga asilia na kadhalika...lakini bado alikuwa mstari wa kwa kukabiliana na changamoto hizi bila kuathiri mambo ya kiusalama wa raia wema. Pongezi Mwenyekiti na tusonge mbele Kikwete CCM.jpg
 
Mh!!!!!!!!!!!!!!Baada ya kusafiri sana na kumaliza kile kidogo kwa ajili ya watu wake lazima tupongeze!:confused:
 
Wakati akipongezwa kwa miaka hii saba aliyotumikia chama kama mwenyekiti na pia kama rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania,pia tungependa kujua ktk safari 337 alizosafiri kwenda nje ya nchi ametumia kiasi gani cha walipakodi kwa safari,wasaidizi wake posho n.k then ni kiasi gani tumepata kutokana na safari hizo.ili tuone tumefanikiwa kwa kiasi gani then tumpe pongezi na ridhaa ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama kwa kipindi kilichobakia.
 
Hakuna yeyote atakayejitokeza kugombea kiti pamoja naye, kwa hiyo usiwe na wasi wasi atashinda tu maana zitakuwa zile kura za Ndio au Hapana !!!
 
na tujue katika hizo safari 337 alitumia kiasi gani alikopa kiasi gani zimetumika ngapi na tunadaiwa ngapi?
kwenye haki za binadamu tuangalie je hakuna mtu hata mmoja aliyeko gerezani kwa ajili yake na je hakuna mtanzania aliyeteswa na kutupwa mabwepande na serikali yake?
 
Mh, binafsi nampongeza kwa kutufikisha hapa tulipo!! saaaaaaaaaaaaaafi sana Mr. President.
 
Ushindi wa Lowasa kugombea kwa ticket ya CCM 2015 utakuwa wa uhakika endapo JK ataondolewa kwenye post ya uenyekiti wa CCM kwenye kikao kijacho.
 
Wana CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti Taifa katika uchaguzi wa Mwenyekiti mwezi ujao.
Sababu za kumuunga mkono Mwenyekiti Dkt. Kikwete ni pamoja na umahiri wake katika uongozi, busara na hekima katika kutoa maamuzi, sera zenye tija na kuongoza nchi kwa Amani na utulivu kwa kufuata haki za bianaadam. Kilikuwa kipindi kigumu kutokana na hali ngumu ya kiuchumi duniani, mabadiliko ya tabia nchi, majanga asilia na kadhalika...lakini bado alikuwa mstari wa kwa kukabiliana na changamoto hizi bila kuathiri mambo ya kiusalama wa raia wema. Pongezi Mwenyekiti na tusonge mbeleView attachment 69754

Sitaki kuamini kuwa mleta mada uwezo wako wa kuelewa, kuchambua, kupambanua na kuwasilisha hoja zako ni mdogo.
Sitaki kabisa kuamini hivyo. Hivyo basi ungeleta hoja kamili kwa kuelezea na kutoa mifano kwa hizo sehemu nilizo highlight. Vinginevyo zichukuliwe kuwa polojo tu!
 
Mie pia namuunga mkono mh. J.K amejitahidi sana kukiongoza chama kwa ufanisi mkubwa hivyo ni vema akaendelea kuwa M/kiti na naomba apate kura zote (100%) ktk uchaguzi ujao ndani ya chama.
jku.jpg

CCM OYEEEEE.........!
 
Wana CCM tunamuunga mkono Mwenyekiti Taifa katika uchaguzi wa Mwenyekiti mwezi ujao.
Sababu za kumuunga mkono Mwenyekiti Dkt. Kikwete ni pamoja na umahiri wake katika uongozi, busara na hekima katika kutoa maamuzi, sera zenye tija na kuongoza nchi kwa Amani na utulivu kwa kufuata haki za bianaadam. Kilikuwa kipindi kigumu kutokana na hali ngumu ya kiuchumi duniani, mabadiliko ya tabia nchi, majanga asilia na kadhalika...lakini bado alikuwa mstari wa kwa kukabiliana na changamoto hizi bila kuathiri mambo ya kiusalama wa raia wema. Pongezi Mwenyekiti na tusonge mbeleView attachment 69754

Ebu nikuulize kidogo hivi ndani ya chama chenu kuna uwezekano wa kubadilisha mwenyekiti tofauti na ambaye ni Rais au mnataka kuudanganya umma kwamba mnafanya uchaguzi? kwa sababu CCM tangu iumbwe haijawahi kutokea mwenyekiti ambaye sio Rais.
 
Imewahi kutokea. Mwaka 1985-1987 mwenyekiti wa CCM alikuwa Julius Nyerere wakati Rais wa Tanzania alikuwa Ally Hassan Mwingi. Ilidumu kwa muda huo tu then back to square one
 
na tujue katika hizo safari 337 alitumia kiasi gani alikopa kiasi gani zimetumika ngapi na tunadaiwa ngapi?
kwenye haki za binadamu tuangalie je hakuna mtu hata mmoja aliyeko gerezani kwa ajili yake na je hakuna mtanzania aliyeteswa na kutupwa mabwepande na serikali yake?

Ongeze na ile ya tarehe 02/07/2012 kwenda china night.
 
CHOMA; mwenye macho haambiwi tazama, tusiwe vipofu wa kutoona mambo mazuri. Tunatakiwa penye jema tunalisifia na kulienzi palipo potosha tunashauri. 'umahiri wake katika uongozi, busara na hekima katika kutoa maamuzi, sera zenye tija na kuongoza nchi kwa Amani na utulivu kwa kufuata haki za bianaadam'
1. Shule za sekondari hadi kata - alipofika madarakani idadi ya vijana wanaoingia sekondari zaidi milioni moja kutoka chini lakita tatu. 2. Mtandao wa Barabara nchi nzima. 3. alipoingia madakani tulikuwa na vyuo vikuu chini ya 10 sasa zaidi ya 20 ikiwemo his legacy of Udom. 4.. safari za nje: a. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tatu barani Afrika kuwa pilot program ya kuzalisha chakula mpango wa World Food Program $900m maana hiyo tutakuwa tuna export chakula East Africa yote na beyond that. b. Mayor Bloomberg ametoa fund $15m more kwa ajili kupunguza vifo vya kina mama wanapojifungua. 5. Upanuaji wa Bandari zetu zote Tanga, Mtwara na Lindi. 6. Hapendi udini, ukabila au ubaguzi wa aina yoyote. Naweza kushuka hapa hadi asubuhi... sasa nikuulize Upinzani Chadema wanapata zaidi ya Tsh.300m kwa mwezi, CUF wanapata zaidi ya Tsh. 300m kwa mwezi wamefanyanini kwa wananchi, kitu gani hata kimoja cha mfano pesa hizo zaidi ya kujinufaisha wao wenyewe na familia zao?
 
Last edited by a moderator:
kibogo; Soma historia ya nchi, Mwalimu alikuwa Mwenyekiti wakati Raisi Mwinyi akiwa rais. Na pia kila Rais anapoingia madarakani huwa sio Mwenyekiti mpaka baadae
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom