Sababu za kufeli kwa zoezi sensa

Pia mimi hadi leo hii sijahesabiwa pamoja na rafiki zangu tunaoishi pamoja.
 
Hivi unaposema zoezi la sensa halijafanikiwa,unazungumza kwa furaha au kwa uchungu. Kumbuka kuwa hizi takwimu hazitatumiwa na serikali iliyopo madarakani tu,hata kama ikiingia serikali nyingine hapo 2015 mf. Chadema,TLP au NCCR bado hiyo serikali itatumia hizo takwimu. Kwa hiyo tuache chuki za kisiasa ambazo hazina msingi.
Siamini kama kila ambacho kinafanywa na serikali ya CCM ni kibaya. Watanzania sisi ambao tunajiita ni wapinzani tukiwa katika majukwaa au vijiweni ndio ambao tunasema serikali ya CCM haijafanya kitu kwa miaka 50 wakati huo tunampa sifa Mwl Nyerere kuwa alikuwa ni kiongozi aliyetukuka wakati wa kipindi chake. Ndugu wananchi tusiwe tunabeba tu kila ambalo tunaambiwa na wanasiasa,Tupime kauli zao. Mimi sio mwanaccm wala Chadema wala chama chochote cha siasa. Nimeongea kwa mtazamo wangu.
''TUACHE KUWEKA MASLAHI YA VYAMA VYETU MBELE,BALI TUWEKE MASLAHI YA TAIFA LETU MBELE''

Basi ngoja tukuridhishe kaka
La kwanza: Walimu hawajagoma
La pili: Madaktari hawajagoma
La tatu: Zoezi la sensa limefanikiwa kwa asilimia 100%.

Kwa mtindo huu utakuwa umewadanganya watakaokuja kuchukua nchi. pmbf we
 
zoezi limefeli nadhani wanafanya makadilio sasa


Hatimaye nilihesabiwa kwenye siku ya kwanza ya 'nyongeza'. Niligundua nimehesabiwa baada ya kupigiwa simu na wife kuomba kaufafanuzi fulani.
 
Back
Top Bottom