Hizi ni hisia zako tu; maana bila kufanya utafiti huna haki ya kuzungumza! Je wewe umetumia vigezo gani kutufanya tuamini sensa imefeli?!
Ni kweli kumekuwa na mapungufu ya hapa na pale na wameweka margin of error kwa sababu kazi hii inafanywa na binadamu sio malaika! lakini sidhani kama mapungufu hayo na changamoto zake zinakidhi kutoa "hukumu ya kifo" kufeili jumla!
Wewe itakuwa ni gamba unashabikia Hata visivo takiwa kushabikiwa unashabikia kisa ccm, zoezi lime fail na huo ndio ukweli Kama Mimi mpaka Leo sijahesabiwa na sijagoma na sio Mimi tuu watu kibao utasema limefanikiwa? Wacha kuwa mamluki kutoka pilau mpaka vitumbua huoni ndio mwisho wewe bado una ngangania tuu? Kweli ngombe wa shirika hufa na ngozi yake nimeamini kupitia wewe na wenzako
Wakati mwingine hujahesabiwa kwa matatizo yako mwenyewe. Toka jumatatu ktk mizunguko yangu nimekua nikipita mitaani naangalia kama geti ama milango ya nyumba imewekewa tick,maeneo mengi hapa Dar yametikiwa kwamba tayari kumeisha hesabiwa. Malalamiko kama yako,peleka ktk Serikali ya Mtaa wako. Hata hivyo sitashangaa ukidai hujui ofisi ilipo!
Jamani mie kulingana na kazi yangu natoka asubuhi na kurudi jioni na naishi pekeyangu so alipokuja karani wa sensa akanikosa. Wakaacha maswali matatu tu kwa jirani;
1. Jina kamili
2. Tarehe ya kuzaliwa
3. Kiwango cha elimu
Hii imekaa vizuri kweli, kwani kulingana na mkurugenzi wa Takwimu alisema kuna aina mbili ya dodoso;
1. Fupi, yenye maswali 32 na
2. Dodoso ya pili ina maswali zaidi ya 60