Sababu za CCM kukataa midahalo hizi hapa

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,100
6,022
Habari za ndani toka katika vyanzo vyao vya fedha za kifisadi za kampeni zinasema kwamba sababu kubwa iliyopelekea kwa katibu mkuu wa sisiem kukataa midahalo ni kwamba kutokana na ubovu na uelewa mdogo kwenye mikutano mikubwa.

Itawachukua muda mrefu na fedha nyingi kumsafisha mgombea ambae atachemka kipindi cha mdahalo, rejea yule dada HAWA NG'UMBI.... CCM haijui ianzie wapi kumsafisha huyu mama....hii ndio hasa sababu ya kukataa mdahalo, sasa tuwaulize bila mdahalo watatekeleza vp sera zao na upeo wao tutaujuaje

Mi nadhani ifike kipindi nasi tuseme kwamba mgombea asiyehudhuria mdahalo hatumchagui katu!!!!!
 
Nakuunga mkono mkuu. Kama wanaogopa kuongea na wananchi wanaotegemea kuwaongoza tutategemeaje uongozi shirikishi kutoka kwa maendeleo ya taifa letu.

Ni jambo moja Makamba kurupoka kama kawaida yake, lakini ni jambo lingine kama hao wagombea wa ccm wako tayari kushiriki midahalo hata kama wasingekatazwa. Nadhani ccm sio ya makamba, inapaswa kuwa na washauri ili katika jambo jema kama hilo huyo mropokaji asisikilizwe.

Any way, nadhani ni wakati sasa wa watanzania kufungua macho na kutoa kura kwa wagombea ambao watatoa sera zao katika midahalo hiyo, pamoja na katika kampeni. Hao ambao wanatawaliwa na huyo mropokaji wao na kukubali kujificha nyuma ya pazia, na wabakie huko huko, hawatafaa kuleta maendeleo katika nchi yetu. Na hawakuweza kuleta kwa sababu daima walijificha nyumba ya pazia. Labda wataweza kuongoza kutoka nyuma ya pazia kwa kutumia 'kitawalambali'. Hata wakichaguliwa hawatakuwa viongozi bora. Makamba akikohoa, watafyata mikia yao. Kama wanachaguliwa kwa maslahi ya makamba na sio ya watanzania, shauri yao hao wanaowapa kura zao.

Mimi na nyumba yangu tutatoa kura zetu kwa wagombea wa chama ambacho kimeonesha tayari mwelekeo wa kutuletea ukombozi watanzania. Nacho sio kingine bali CHADEMA.
 
Ni muhimu midahalo iendelee hata bila ushiriki wa CCM. Kama Tido Mhando atasimamisha midahalo kwa shinikizo la CCM atakuwa amewakosea Watanzania haki ya kuwapima vizuri wagombea kabla ya kupiga kura zao.

CCM inaogopa midahalo inaweza ikazungumzia UFISADI. They are very vulnerable on that score.
 
Midahalo muhimu unawezaje kuwa kiongozi ukaogopa maswali ya wananchi basi ww ni kiongozi usiokuwa na mwelekeo sahihi
 
mkuu hapa iringa mkurugenzi huwa anakataza midaharo au mahojiano kati ya mtangazaji na mgombea wa upinzani kwenye runinga ya manispaa. kazi ipo
 
Kupitia mdahalo ndio tutajua uelewa wa wagombea na sera za vyama vyao. Inaonekana ccm wameshaona kuwa kunadi sera zao ili zikubalike kwa watu wengi wenye uelewa ni kazi ngumu, na pia wagombea wao itakuwa vigumu kukinadi chama chao kupitia midahalo kwa madudu kilichofanya toka tumepata uhuru.
 
mkuu hapa iringa mkurugenzi huwa anakataza midaharo au mahojiano kati ya mtangazaji na mgombea wa upinzani kwenye runinga ya manispaa. kazi ipo

Huyo ni dikteta, anawanyima wananchi uhuru wa kusikiliza upande wa pili, anaingilia kazi ya waandishi wa habari. Nadhani hili llinazungumzika, ikiwa wapinzani watakaa pamoja naye au na kamati fulani ndani ya manispaa (?fair competition committee kama ipo ) ili kuhakikisha chombo kinachogharamiwa na manispaa kinatoa huduma bila upendeleo. Hao wanafunzi wa iliyokuwa Mkwawa hapo hawalioni wakamsemea huyo Mkurugenzi! Maskini Mkwawa ile tanashari ya 1970s ilishakufa!!!!!!!!!
 
Ni muhimu midahalo iendelee hata bila ushiriki wa CCM. Kama Tido Mhando atasimamisha midahalo kwa shinikizo la CCM atakuwa amewakosea Watanzania haki ya kuwapima vizuri wagombea kabla ya kupiga kura zao.

CCM inaogopa midahalo inaweza ikazungumzia UFISADI. They are very vulnerable on that score.

Tido Mhando alishatangaza kwamba midahalo itaendelea hata atapata watu wawili tu!
 
mkuu hapa iringa mkurugenzi huwa anakataza midaharo au mahojiano kati ya mtangazaji na mgombea wa upinzani kwenye runinga ya manispaa. kazi ipo
mh!kweli kazi ipo,lini kutakuwa na demokrasia ya kweli Tanzania jamani?
 
Ni muhimu midahalo iendelee hata bila ushiriki wa CCM. Kama Tido Mhando atasimamisha midahalo kwa shinikizo la CCM atakuwa amewakosea Watanzania haki ya kuwapima vizuri wagombea kabla ya kupiga kura zao.

CCM inaogopa midahalo inaweza ikazungumzia UFISADI. They are very vulnerable on that score.

Midahalo nadhani itaendelea cause leo nimeona tangazo TBC, leo saa tatu usiku kutakuwa na mdahalo wa jimbo la ARUMERU,
 
Kweni wao wanapenda kujimaliza wenyewe? wanajua fika madudu waliyofanya na hawana majibu kwa uchafu walioufanya ktk kipindi chote walichotawala ila bado wanataka kutuongoza kama walivyo bila kuwajibika kwa wanainchi au niseme wanafunika kombe mwanaharamu apite huku wakiwa wamesahau kuwa mbio za sakafuni siku zote huishia ukutani...lini ? hapo sijui ila Mungu bado anapanga, ....EPA,Meremeta,BOT,TPTL Scandal, Buzwagi contract, Buhemba,Tanesco..etc hazitakaa zifutike au kufa hivihivi maisha na milele amina
 
Nadhani hili siyo la kufumbia macho tuelimishe jamii na watanzania kwani haya ni moja ya mambo muhimu ambayo vyombo vya habari vingepigania kuhahakikisha kile walichoanzisha wanahabari wenzao kinatoa fursa pana na sahihi kwa wananchi kuwajua vyema wagombea haswa wa ubunge kwani ndiyo wanaotarajiwa kutuletea chachu ya maendeleo.

Sasa itakuwa vipi hawa watu wamezibwa midomo na kitambaa cheusi cha sekula ya katibu mkuu kumbe siyo tu hiyo bali walishinda kura za maoni kwani walitapakanya vyema viinua mgongo vyao vya bunge lililopita kwa kuwa nasema wewe ni kiongozi unatarajia kuwaongoza watu je utawasiliana nao vipi kama huwezi kuzungumza nao hivi leo.

acheni hizo !!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi midahalo bila sisi mafisadi haiwezekani?

Kama sisi m hawataki midahalo si waache tu na kukaa pembeni huku vyama vingine vikimwaga sera? WAtakuwa wamejimaliza wenyewe.

TBC endeleeni na midahalo kwa vyama vingine, hatuihitaji sisi m kushiriki maana ni waoga tutawauliza kwa nini wamebobea katika kutuletea ahadi kila baada ya miaka mitano na hawatimizi. Na hapo lazima wakache.
 
Ni kitu cha aibu kubwa sana kwa chama kikubwa na kizee kuliko vyote tanzania kwa sasa kukataza wagombea wake kutoshiriki midahalo ambayo itatuwezesha sisi wapiga kura kubaini kati ya mbivu na mbichi.

Katazo lao laonesha uwezo na upeo mdogo walio nao viongozi hao katika kushughulikia mambo ya msingi ya taifa letu. Poleni sana wanachama wa CCM kwa kudhalilishwa na uongozi wenu hasa wa mzee aliyefukuzwa ualimu kwa kosa analoona aibu kulisema na hiyo ndio taswira ya serikali inayoongozwa na chama hicho kilichoshika hatamu.

Poleni watanzania kwa kushindwa kupata fursa ya kuchanganua mbivu na mbichi zinazohusu CCM pia. Ila nakubali wanaoshiriki wanaosema wagombea wenzao waliolazimishwa kuingia mitini na kuwakejeli ambako kutasaidia wao nao wajibu kwa hoja ila sipendi matusi ama nguvu za hoja za kutudanganya kamwe. Wanachoongea CHADEMA ni kueleza ukweli nao huuma kiasi cha kuitwa matusi.

Poleni sana CCM
 
SIKU chache baada ya kuwazuia wagombea wake wa ubunge kushiriki katika mdahalo, CCM kimesema kuwa mgombea wake wa urais Jakaya Kikwete pia hatashiriki mdahalo wowote.

Wiki hii CCM ilitoa taarifa ya kuwazuia wagombea wake kushiriki katika mdahalo unaoendeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuhusisha wagombea wa vyama vyote katika kila jimbo, ikidai kuwa hauna tija na kwamba, watatumia majukwaa kuwafikia wapigakura.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Meneja wa Kampeni za CCM, Abdulrahaman Kinana alisema wameamua kumzuia Kikwete kushiriki katika mdahalo wa wagombea urais baada ya kubaini mdahalo huo hauna umuhimu wowote na akatoa sababu kuu tatu za kufikiwa kwa uamuzi huo.

"Umuazi wa kumzui Kikwete kushiriki mdahalo unatokana na kubaini kuwa sio muhimu katika kujinadi na kunadi sera zetu kwa wananchi zaidi ya utaratibu wa mikutano ya hadhara na ya ndani. Utaratibu huo bado unakidhi haja. "Tunaendelea nao," alisema Kinana na kuongeza; "Katika nchi 200 duniani zenye vyama vyama vingi vya siasa, ni nchi 10 kati ya hizo ndizo wagombea wake katika nafasi wanafanya mdahalo.''


Kinana alisema hawatashiriki mdahalo huo kwa sababu ya vyama vya upinzani vinataka kutuumia kunadi sera zao kutokana na kukosa mbinu za kutembelea maeneo mengi.

"Kutokana na wapinzani ambao sera zao hazitambuliki na hawana mbinu za kutembelea maeneo mengi, wanataka kutumia fursa ya mdahalo kujitangaza,'' alisema Kinana.`


Meneja kampeni huyo alitaja sababu nyingine kwamba, ratiba ya mgombea wao imejaa hivyo hakuna muda wa kushiriki mdahalo na kuwa mpango wao ni Kikwete kupita kila eneo kueleza mafanikio yaliyofikiwa na chama chake pamoja na kujua matatizo ya wananchi na kunadi sera za chama. "Mkiwa katika mdahalo mtaeleza sera za jumla na wakati mpango mkakati wa CCM ni mgombea wake kujinadi na kunadi sera zetu kwa wananchi katika maeneo yao husika,'' alisema Kinana.


Kinana alidai kuwa ilani za vyama vya upinzani hazina takwimu na ya CCM ambayo inamaelezo ya kina na takwimu za nchi nzima.


"Ukiangalia ilani za vyama vya upinzani, hazina takwimu na zipo kiujumla, ukiilinganisha na ya CCM,'' alisema Kinana. Kuhusu kama Kikwete atapata ushindi kama alivyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Kinana alisema: "Siamini kama wananchi watamuangusha, naamini atapata zaidi ya asilimia 80.1 alizopata mwaka 2005.''




CCM yazuia JK kushiriki mdahalo

chanzo: Mwananchi

My take, kumbe CCM wameshtuka wapinzani wanataka mdahalo kufikia watu wengi zaidi kwa mgongo wa CCM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom