Sababu ya vijana kukosa ajira yatajwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Israel Mgussi, Dodoma.
NYADHIFA zaidi ya moja kurudikiwa mtu mmoja imedaiwa kuwa chanzo cha vijana wengi kukosa ajira na fursa zilizopo katika kulitumikia taifa lao ipasavyo licha ya vigezo na sifa walizonazo.

Akizungumza na Waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Msaidizi wa Kituo cha msaada wa kisheria Tanzania (Talac), Godwin Ngongi alisema kuwa tatizo la ajira nchini ni bomu ambalo kama serikali haitalivalia nyuga ikiwemo kufuta mtindo wa kurudikiana nyadhifa, linaweza kuja kusababisha mvutano na vurugu nchini.

Ngongi alisema, kwa kuwa Katiba iliyopo sasa haizui mtu mmoja kushika nafasi nyingi za kazi, ametoa hamasa kwa Katiba ijayo ikazingatia hilo ili kuzuia wachache kujirundikia nyadhifa hasa katika nyanja za kisiasa jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine limekuwa ni chanzo kwa vijana kukosa fursa ya kuitumikia nchi yake.

“Katiba ijayo izuie jambo hili, haiwezekani mtu huyo awe Mbunge na wakati huo huo anakuwa Mkuu wa Mkoa, au mtu anastaafu kwa mujibu wa sheria katika utumishi wa umma kutokana na umri kumtupa kisha mtu huyo huyo anateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya fulani, hii si haki kama mtu umri wake wa kustaafu umetimia na ameshastaafu haipendezi kumchomeka katika nafasi nyingine maana mshahara anaopokea ni ule ule kutoka kwa walipa kodi wa nchi.”Alisema Ngongi.

Alisisitiza kuwa Katiba ijayo lazima izuie mtindo huu ulioibuka sasa wa utendaji usiokuwa na kikomo ambao kwa namna moja ama nyingine umekuwa ukiwanyima vijana fursa ya kulitumikia taifa pamoja na kuchangia kushuka kwa ufanisi kazini.

“Mtu anapokuwa amestaafu kutokana na umri kumtupa kwa nini ateuliwe katika nafasi nyingine za utumishi wa umma? Kwa kweli hii mbali na kuwanyima vijana fursa inasababisha ukiritimba pamoja na kushuka kwa ufanisi kazini, lazima kuwe na kikomo, kama mtu ametimiza umri wa miaka 60 apumzike tu, hakuna haja ya kubebana na kuteuana kwenye nafasi hizi zinazoitwa za kisiasa katika Katiba mpya izuie jambo hili.”Alisema Ngongi.

Ngongi alisema kuwa kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kwa lengo la kulitumikia taifa lake ipasavyo lakini mtindo huu ulioibuka sasa unawanyima vijana wanaohitimu katika vyuo mbalimbali nchini kulitumikia taifa na zaidi ya hapo umesababisha mfumo wa ajira uendane na hulka ya kujuana na si ufanisi na sifa ya mtu.

Pia alionya mtindo ulioibuka sasa ambapo kila nafasi za kazi zinazotangazwa na taasisi za umma au binafsi zinamtaka mhusika awe na uzoefu wa kazi usiopungua mwaka mmoja akisema jambo hili limesababisha vijana wengi kujikuta hawana sifa ya kuajiriwa ingawa wamehitimu katika vyuo na uwezo wa kutenda kazi wanao.

Chanzo.
Sababu ya vijana kukosa ajira yatajwa
 
NYADHIFA zaidi ya moja kurudikiwa mtu mmoja

hofu ya watawala wa afrika ndo maana wanafanya hivyo!
 
Sihitaji hata kupewa sababu za kukosa ajira vijana maana hata mtoto wa naibu waziri wa kazi mwenye dhamana ya kuzalisha ajira, mtoto wake wa kumzaa hana kazi!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom