Sababu ya Man Utd kubebwa hii hapa

Uzi ndo kwaanza unakuwa relevant.

Sijui kama mtoa mada bado yuko hai.

Who knows may be alistaafu na akina Faggie na Gill.
mtoa uzi yuko hai, na wala hoja hazitabadilika. Man utd sio timu ndogo, kifedha imeshajijenga sana na ina uwezo wa kusajili wachezaji wazuri ikafanya vizuri. Ila kumbuka, kwa sasa haiogopwi uwanjani. Hii haimaanishi si timu nzuri. Na kumbuka hata wakati tunaongelea kubebwa hatukumaanisha timu iliyokuwa inabebwa ilikuwa mbaya. Inawezekana kweli kubeba gunia la misumari, la hasha. Man u bado haijafikia mafanikio kiasi cha kumuua mtoa mada. Kama mtu wa mpira siwezi kuanza kufikiria kutoa uzi wangu kwa sababu ya matokeo ya nusu msimu. Liverpool imefanya vibaya kwa sababu zilizo wazi msimu huu. Suarez hayupo, sturridge hayupo na kocha amepata tabu na wachezaji wapya. Nani asiyejua kazi ya sturridge na suarez, au angalau sturridge tu ambaye bado ni mchezaji wetu. De gea angeumia leo muda mrefu tungeongea story nyingine. Hata mechi na liverpool ndiye aliyewatoa. Amekuwa mtamu msimu mzima. Au unataka nisingizie goli la offside walilopewa man utd?? Hapana, liverpool imekuwa na matatizo mengi kuliko hayo. Hata man u wasingepewa hilo goli bado wangefungwa tu. Kwa nini nasema haya? Hukumu isitolewe bila kujali sababu kama hizi, tena hata kabla nusu msimu haujaisha. Uzi uendelee, tutaonana baada ya msimu kufikia tamati. Kila la kheri liverpool na man utd. Hukumu ya uzi huu tutaitoa baada ya misimu mingine zaidi ya miwili. tusubiri huu wa pili uishe, na wa tatu na wanne, pengine tutakuwa tumezisahau liverpool na man utd, labda wafalme watakuwa chelsea na man city, time will tell.
Mengi ya kuongea yapo ila muda wake bado. Nawaachia wanazi wenye uwezo wa kuchambua neno moja moja, na si dhana nzima
 
EMT wengine tuache tuna uchungu usiofutika, huko ulaya Liverpool majanga, huku nyumbani Simba nao majanga, loh.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom