Sababu kuu za kuvunjika kwa mahusiano: Kupiga na kupigwa chini...

Mar 2, 2011
86
20
Ndugu zanguni wana JF; Leo nimeona niwaletee dokezo tu kwa mengi niliyochunguza juu ya mahusiano hasa ya mapenzi, uchumba na ndoa. Kichwa cha habari chahusika.

Sababu ya kwanza ni KUTOKUJIAMINI NA MTU ULIYENAYE. Hapa nielezee tu kwa ufupi; utakuta mtu yuko na mpenzi/mume/mke wake anadai hataki kumpa upendo wa dhati kwa vile anaogopa akiachwa ataumia sana. Hili hupelekea kila mtu mwenye fikra hizo kukaa mguu ndani-mguu nje; yaani kila mmoja yuko kwenye mkao wa kujihami kuachwa. Hii husababisha zaidi wapenzi wenye fikra hii kuwa na mawazo hasi (-) yasiyo ya maendeleo wala tija kwa maisha yao ya kesho bali kuendekeza kuchunana zaidi badala ya kushauriana tufanyeje kuandaa maisha yetu ya baadaye; watu wanawaza mambo yasiyojenga. MFANO. Mwanaume anawaza tu kwamba atembee sana na msichana (nimetumia tasfida) kila wakikutana ni kudo tu ili kwamba hata wakiachana amemdo vya kutosha roho haiumi na kwa Binti/mwanamke yeye anachowaza ni namna gani ataweza kumchuna sana/kuchukua pesa za mpenzi, kuspend n.k ili mradi tu ahahakikishe anamchuna to the maximum hata akiachwa au wakiachana roho haiumi. Hii hupelekea sababu ya pili.

Sababu ya pili ni KUPOTEZA MWELEKEO WA UPENDO. Hii ni kwamba mwanaume anaaza kuona mh! hapa nimeingia chocho, "kila siku vizinga haviishi, kila simu ikiita kwririririr.. hello... "nina shida ya 30,000/-, 50,000/- n.k" matokeo yake hata kama mwanaume alikuwa anakupenda anabadilisha mwelekeo na kutafuta wa sifa anayotaka amabaye wataweza kushauriana kwa maendeleo ya kujenga familia; yaani what we call "wife material".

Jamani najua zipo sababu nyingi sana zinazopelekea watu kuachana, ila kwa leo nimeona tu nigusie izo mbili.

USHAURI WANGU: NI HERI UKIMPENDA MTU MMOJA JIACHIE KABISA KWA UPANDE CHANYA (IN POSITIVE WAYS) NA MSIWE MGUU NDANI-MGUU NJE, ILI MUWE NA MTIZAMO CHANYA (POSITIVE MIND) WA MAISHA YA LEO NA KESHO, NA HII ITAWAWIA RAHISI KUWA NA UPENDO WA DHATI KWENU MNAOPENDANA NA HIVYO KILA MTU KUTOFANYA MAMBO YANAYOMKWAZA MPENZI WAKE NA KWA JINSI HII IKAWA/ITAKUWA NI RAHISI SANA KUSAMEHEANA KWA MAKOSA MADOGO MADOGO. TUSIWE WANAUME WA KUWAFANYA WAKE ZETU MAADUI NA KUFANYA MAMBO YA MAENDELEO KWA SIRI TUWASHIRIKISHE TU;; NA WANAWAKE MSIWE WATU WAKUFIKIRIA KUACHWA NA KUGAWANA MALI BALI SOTE KWA PAMOJA (WANAUME NA WANAWAKE) TUWE NA MTIZAMO WA WENZA WA MAISHA ILI TUSIKAE KWA KUJIHAMI JUU YA MALI N.K BALI TUPALILIE MAPENDANO NA MAPENZI YA KUDUMU KATIKA SHIDA NA RAHA.

Kwenu wana JF kwa maoni na michango yenu yote; KARIBUNI
 
Mungu akubariki kwa kukuongoza kulisema hili...........ni kweli huu ni mzizi mmojawapo unaodhoofisha mahusiano!
 
watu wanachokana haraka sana these days, so wanataka ku-spice up mambo kwa kupata vitu vipya kila wakati... kama mastaa wa majuu vile
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom