Sababu Kubwa 2 za Kuukataa Mchakato huu wa Katiba Mpya

Je wapo ambapo wanauunga mkono mchakato huu? Kwanini wanafanya hivyo wajaribu kutushawishi na sisi wengine...
Tupo na tulishasema huko nyuma, labda tuu tufanyareference upya!.
Kwa kifupi ni 'haba na haba'...
Kidogo kidogo...
Moja shika sii kumi nenda rudi!,
Ukipewa shubiri, usichukue pima!
If you can't get what you want, just take what you get!, because something is better than nothing!.
Kwa vile katiba iliyopo ni nothing, na japo tunataka "katiba bora", huu mchakato, hautatupatia katiba bora, bali utatupatia "bora katiba!". Hii bora katiba ni something better than nothing!, tuipokee na tukishaingia wenyewe, ndipo tuwaletee hiyo katiba bora!.

Pasco.
 
KASORO KWENYE MCHAKATO WA KATIBA: JAJI WARIOBA ATUELEZE UHALALI WA MABARAZA YA KATIBA YALIYOCHAGULIWA
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Warioba ametoa tamko lenye utata mkubwa kuhusu uamuzi wa tume yake kukataa kurudia chaguzi za mabaraza ya katiba. Utata huu unatokana na kwamba tume inakiri kuwepo kwa kasoro kubwa sana katika mchakato wa chaguzi hizo (kasoro hizo zimeelezwa sana na makundi mbalimbali pamoja na taasisi wadau. Sipendi kuzirudia hapa).

Kinachoshangaza, Jaji Warioba (mtu anayeheshimiwa na watu wengi) anatoa tamko zito kwa maelezo mepesi. Ati kwamba, pamoja na kasoro hizo, tume yake haitarudia chaguzi hizo. Lakini hatoI sababu za msingi na zenye mashiko kwa nini chaguzi zisirudiwe. Anatoa sababu kuwa tume yake ina watu wenye weledi na wanafanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa. Lakini, weledi wa tume si suala linalolalamikiwa hapa: na watanzania hawategemei kuwa tume haina weledi. Weledi ni jambo moja, na ufanisi ni jambo jingine. Pengine, maamuzi yao ya kukataa kurudia chaguzi yanaweza kutufanya tuhoji nini maana ya weledi wanaousema!!

Masuali ambayo Jaji huyu anapaswa kuyajibu ni: Je, hayo mabaraza ni halali? Nini uhalali wa mabaraza hayo yaliyochaguliwa kwa njia zisizo halali? Yeye ni mwanasheria (bila shaka) nadhani anayo majibu.

Siamini kuwa, katika suala nyeti la katiba, kuvurugwa kwa taratibu za chaguzi si tatizo la kisheria. Swali ni: je, kwa nini matokeo ya chaguzi zingine hutenguliwa na chaguzi kurudiwa inapogundulika kasoro kubwa? Naamini jibu analo Jaji Warioba.

Swali jingine: Je, Jaji Warioba anatambua madhara ya maamuzi anayoyafanya? Kama hatambui, nini sababu wa kutufanya tuamini kuwa tume yake ina weledi wa kutosha? Anatambua kuwa kipimo cha weledi wao ni pamoja na kujua kuwa katiba inayotafutwa si yao bali ni ya watanzania wote?

Je, Jaji Warioba na tume yake wapo tarayi kubeba mzigo wa madhara ya maamuzi yao? Anawezaje kunishawishi kuwa tume hii si “Tume Maslahi”? Ni vipi mabilioni ya fedha za wanyonge zinatumika kulipia watu posho nono lakini wakashindwa kabisa kubaini, kuzuia, kudhibiti, na kuondoa kasoro kubwa kwenye mchakato wa katiba? Weledi wao hauhusiki na masuala haya? Walishindwa kubaini kasoro, wakashindwa kuzuia kasoro na kuzidhibiti!!! Sawa!!! lakini hata baada ya kugundua kasoro wanashindwa kuziondoa!!!! Inaingia akilini kweli?

Je, Jaji Warioba anatambua kuwa watanzania wa sasa si wale wa kale wanaoweza kuburuzwa tu? Hajui kuwa asipoondoa kasoro hizi mwanzoni hatakuwa na uhalali wa kuondoa kasoro zingine huko mbeleni? Huu weledi wa hii tume ni upi? Hawajui hata mantiki ndogo tu, kwamba “usipoziba ufa utajenga ukuta”.

Je, Jaji Warioba bado anatarajia kuendelea kuheshimiwa na watanzania? Hapa ndipo anapaswa kutafuta jibu lake. Kwangu mimi, nina mashaka makubwa na yeye! Afanye maamuzi magumu yenye tija: kama ni kuwatumikia watanzania au kama ni kuwatumikia watawala!

Mwisho natoa rai kwa watanzania kusimama imara katika kusimamia haki ya kupata katiba mpya “halili” na sio “feki”. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ooh boy; hii ilikuwa ni 2011... yote niliyoyasema ndiyo haya yanatokea... kuna njia nyingine ya kutoka kwa kweli?
 
Kweli Kabisa CCM wamedakia na pengine kupora mchakato wa katiba ila na pengine kudai tena mchakato uanze upya kuliko hivi ilivyo sasa
 
Back
Top Bottom