EngineerLMG
Senior Member
- Nov 28, 2013
- 125
- 75
Mara kwa mara huwa nasoma mambo kama "Wakenya mmeshindwa kutengeneza JF yenu"... "Tuwachie sisi JF yetu"... "Imetengenezwa na Watanzania"... "Hamna forums zenu"... "Hamna kazi ya kufanya mnakuja huku"...
Mnachosema ni kwamba hamtutaki kwenye forums zenu. Eti tusije. Lakini wacha niwaambie, tutasijaaa! Tena kwa rabsha na sokomoko.
Sababu moja itakayofanya tuzidi kusija JF inaweza kupatwa kwenye video hii hapa ya Coca Cola:
Tanzania ni kama ule mdogo. Na sisi? Si unajua tu.
Hata kama tunawahangaisha, deep down in our hearts, tunawapenda pia. Nyie ni ndugu zetu wa jadi. Na yeyote atakaye jaribu kuwasumbua, mtuambie tu. Tutapambana nao.
Kenya na Tanzania haziwezi kutenganishwa. Mimi kibinafsi, ninazo asili za Kitanzania (robo ya familia yangu iko TZ). Na tumetoka mbali, sisi majirani wawili.
TLDR: Tutaendelea kuja JF, tutaendelea kuwahangaisha, lakini hata hivyo, tunawapenda sana.