Sababu 3 zilizonyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema,mtumishi wa Serikali anitonya

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,
Kuna sababu tatu za kutokea kwa vifo ktk mikutano ya Chadema . Sababu ya kubwa ya kwanza iliyonifanya hata leo nilete uzi huu hapa ni maelezo ya rafiki yangu anayefanya kazi ktk mmoja ya taasisi za serikal akinitonya kwamba, serikali inataka kutunga sheria ya kuzuia ama kuthibiti mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyokwisha dokezwa na mwanasheria mkuu wa serikali Bungeni. Tatizo kubwa ambalo linawakabili mpaka sasa serikalini, ni kukubalika kwa sheria hiyo mbele ya Umma. Hii inatokana na baadhi ya maofisa (yeye amewaita objective) wanadhani kwamba itapingwa sana na vyama vya siasa na hata wananchi hawataiunga mkono sheria husika. Mmoja ya mapendekezo ni kwamba ili kupunguza vurugu na usumbufu ktk mikutano na maandamano, viogozi wasiruhusiwe kwenda kwenye majimbo yasiyo yao kisheria (Hoja ya Anne Kilango Bungeni) bila kupata ruhusa na bila sababu inayoeleweka. Huyo bwana akasema, nina wasiwasi na vifo hivi na harakati zinaendelea huku serikalini za kuhalalisha sheria hiyo ambayo yeye pamoja na kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini, ana ona kama ni mbovu kabla hata draft ya kwanza yenyewe haijaandaliwa.

Hoja ya pili kubwa sana ni hao Maofisa objective wanaopinga sheria hiyo, wanadhani kwamba sheria hiyo itagombanisha serikali na wafadhili kiasi cha kuzuia misaada na mikopo. Hoja hii ya pili ya wapinzani wa sheria hii ndio yenye nguvu kuliko kuliko ile ya kwanza. Sasa yeye ananiuliza, hebu fanyeni utafiti isijekuwa yanajengwa mazingira ya kuwalainisha wahisani na kuhalalisha sheria hiyo kabla sheria haijatungwa na hamjazuiwa kufanya shughuli zenu za kisiasa.
Kwa maoni yake japokuwa hana ushahidi, vifo hivi na utata unaozingira vifo vyenyewe kunaweza kuwa na uhusiano na taarifa zake. (Hayo ni ya rafiki yangu aliyoniambia)


Sababu ya 2; Vifo vya Singida na Morogoro, kwa nini vinaweza kuwa na mkono wa mtu.
Kifo cha Singida kwa kiwango kikubwa ina halalisha (justify) maelezo ya huyo rafiki yangu. Hii ni kwa sabau, Katika mikutano iliyofanyika Singida, viongozi wa Chadema walipata taarifa kuwa vurugu zitatokea ktk mkutano wao. Wakaomba ulinzi wa kutosha wa Jeshi la Polisi. Pamoja na kutoa taarifa polisi na polisi kuwepo, bado vurugu hizo zilitokea na mtu akafa katka mazingira ya kutatanisha viongozi hao wakiwa wameshaondoka. (Singida polisi hawakuhusishwa, lakini ndipo kulipo na ile kambi ya vijana wa ccm iliyofichuliwa na Dr Slaa). Baadaye polisi na ccm wakajenga mazingira ya kukihusisha Chadema. Chadema walipeleka hoja hiyo bungeni ili ijadiliwe kwa undani na ukweli ujulikane, wakakwama pamoja na kuiweka kwa urefu ktk maoni ya msemaji wa kambi hiyo – walizuiwa kusoma. Kitu gani kinafichwa?

Morogoro.
Morogoro polisi waliua. Mashuhuda wapo. Polisi ikajiundia kamati ya kujichunguza chap chap na kuleta matokeo feki kwa kiwango cha kutia aibu. Pili, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka Jf na baadhi ya magazeti, kuna tetesi za wanandugu kushawishiwa ili kuichafuaChadema. Sakata hili lina maswali ya kujiuliza kama ifuatavyo. Kwa nini Chadema walikwekewa mizengwe kushiriki msiba huo. Kwanini wanandugu wa marehemu Ali ambao mwanzoni walikuwa wanaandaa mazishi vizuri na Chadema wakageuka ghafla na kutumia msiba huo dhidi ya Chadema kama hakuna mkono wa ccm na serikali? Tatu, ni lini ccm na serikali walikaa na kuwashawishi wanandugu wa Marehemu Ali dhidi ya Chadema ktk kipindi kifupi namna hii kama hamna maandalizi, kabla ya kifo? Ktk siku mbili waliwezaje kulifuatilia asili yake na wakawa tayari kwenda mkoa wa Tanga kutafuta ndugu zake kuwashawishi? Naomba kushawishiwa kuwa yote haya hayana maandalizi ya kabla.
Mmoja ya comment hapa chini [QUOTE=Ndukidi; Siku tatu kabla ya mkutano wa Morogoro Nape Nnauye akongea kwenye radio moja, alisikika akishauri wananchi wa Morogoro wasiende kwenye mkutano wa CDM kwani kutatokea vurugu na wanaweza kuumia.. alikuwa anaongea kama vile kuna mpango funali, nilikuwa namsikiliza na watu wengine , kuna mtu akasema mbona anaongea hivi , au wamepanga kufanya vurugu.. kilichotokea baada ya hapo wote tunajua...
Binafsi namini huu ni mkakati wa serikali kutaka ama kufuta CDM, au kupiga vita mikutano ya CDM kabisa.[/QUOTE]
Na mimi nauliza Tangu lini Nape amerithiswa cheo cha utabiri cha Shehe Yahaya?

Sababu # 3; inazohalalisha kuwa vifo hivi vina msukumo nyuma yake.
Chadema ilipoanza operesheni hii Morogoro baada ya ile ya kwanza kufanikiwa sana (tena huko mtwara na Lindi) ilikutana na mizengwe Mingi sana ya kukwamisha zoezi hili. Polisi walikuja na hoja nyingi sana dhaifu. Mara polisi wachache, mara kuna vyama vingine vimeomba kufanya mikutano nk. Chadema wakalazimika kwenda morogoro vijijini na kuahirisha morogoro mjini kwa muda. Maswali ya kujiuliza, Je, polisi walikuwa wanazuia mikutano kwa hoja dhaifu kwa msukumo wa nani? Je, tuamini kwamba baada ya kushindwa kuzuia mikutano ccm hawana plan B? Kama ipo ni ipi? Vifo hivi na utata wake vipi? Ni hoja yangu kuwa baada ya kukwama kuzuia mikutano husika wasingeweza kukaa kimya. Lazima wangekuja na mikakati mipya kama hii tunayoiona. Nashawishika kuamini kuwa wana mkono ktk vifo hivi.

Nikisema kwamba Serikali ikishindwa kutunga sheria ya kuzuia na kuthibiti mikutano hii, watatumia vifo hivi vyenye utata kuzuia mikutano husika, nitakosea? Je, wahisani na wananchi watawaelewa? Ni suala la Muda tu.
Je, kauli ya wasira kuwa tunaweza kuifuta Chadema inawaandaa wananchi kwa lipi? Je, mkakati wa kulifanikisha hilo ni upi? Nikidhania kwamba vifo hivi ni njia mmojawapo nitakosea? Je, baada ya CD ya ukabila, udini na ukanda kuchuja hii CD mpya ya vurugu itauza? Je, yote haya lengo lake ni nini? Kuifuta Chadema kama alivyosema wasira? Kuichafua ikataliwe na wananchi au kutisha wananchi wagomee mikutano yake na kuidhoofisha? Time will tell.

NB; Ikumbukwe, kiwango cha kukataliwa kwa ccm kabla na baada ya Uchaguzi wa Arumeru kinazidi kupanda. Hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwamba wakaamua kufa kibudu. Tafakari.


 
Yaani sababu zote zinaitoa CDM kwenye picha. Kwa nini unatumia nguvu kuisafisha kama tayari ni safi? Wananchi wana akili wanajua ukweli.
 
Hili linaeleweka mkuu maan CCM sasa hivi ni maji ya shingo kwahyo mbinu pekee ni kufanya mauaji
 
Angalieni picha kwenye mwananchi, yule askali ndio kashutu mwanahabari live ananekana
 
Somo zuri sana.
Ukweli mtupu.

TUENDELEZE MAOMBI NA SALA.
 
Everyone is crying out for peace yes
None is crying out for justice
(2x)

(CHORUS)
I don't want no peace
I need equal rights and justice (3x)
Got to get it
Equal rights and justice

Everybody want to go to heaven
But nobody want to die
Everybody want to go to up to heaven
But none o them (2x) want to die

CHORUS
(Just give me my share)

What is due to Caesar
You better give it on to Caesar
And what belong to I and I
You better (2x) give it up to I

CHORUS
(I'm fighting for it)

Everyone heading for the top
But tell me how far is it from the bottom
Nobody knows but
Everybody fighting to reach the top
How far is it from the bottom

CHORUS

Everyone is talking about crime
Tell me who are the criminals
I said everybody's talking about crime, crime
Tell me who, who are the criminals
I really don't see them

CHORUS

There be no crime
Equal rights and justice (Precedes each line below)
There be no criminals
Everyone is fighting for
Palestine is fighting for
Down in Angola
Down in Botswana
Down in Zimbabwe
Down in Rhodesia
Right here in Jamaica

by Peter Tosh.
 
Yaani sababu zote zinaitoa CDM kwenye picha. Kwa nini unatumia nguvu kuisafisha kama tayari ni safi? Wananchi wana akili wanajua ukweli.

Mwananchi gani unaemsema hapa unayempa akili hiyo iliyopinda kama yako! Kwenda haja kwako kisha ukacheka baada ya kuvuta halufu ya kinyesi wakati ukijua inatokana na mavitu ya haramu ulokula ni wehu tu kujidanganya eti kuna mwananchi mwenye akili kama yako!

 
Everyone is crying out for peace yes
None is crying out for justice
(2x)

(CHORUS)
I don't want no peace
I need equal rights and justice (3x)
Got to get it
Equal rights and justice

Everybody want to go to heaven
But nobody want to die
Everybody want to go to up to heaven
But none o them (2x) want to die

CHORUS
(Just give me my share)

What is due to Caesar
You better give it on to Caesar
And what belong to I and I
You better (2x) give it up to I

CHORUS
(I'm fighting for it)

Everyone heading for the top
But tell me how far is it from the bottom
Nobody knows but
Everybody fighting to reach the top
How far is it from the bottom

CHORUS

Everyone is talking about crime
Tell me who are the criminals
I said everybody's talking about crime, crime
Tell me who, who are the criminals
I really don't see them

CHORUS

There be no crime
Equal rights and justice (Precedes each line below)
There be no criminals
Everyone is fighting for
Palestine is fighting for
Down in Angola
Down in Botswana
Down in Zimbabwe
Down in Rhodesia
Right here in Tanzania.

by Peter Tosh.
 
You're totally out of control, you're a hater, and you're unattractive inside and outside(by Serena Williams).


Yaani sababu zote zinaitoa CDM kwenye picha. Kwa nini unatumia nguvu kuisafisha kama tayari ni safi? Wananchi wana akili wanajua ukweli.
 
Siku tatu kabla ya mkutano wa Morogoro Nape Nnauye akongea kwenye radio moja, alisikika akishauri wananchi wa Morogoro wasiende kwenye mkutano wa CDM kwani kutatokea vurugu na wanaweza kuumia.. alikuwa anaongea kama vile kuna mpango funali, nilikuwa namsikiliza na watu wengine , kuna mtu akasema mbona anaongea hivi , au wamepanga kufanya vurugu.. kilichotokea baada ya hapo wote tunajua...

Binafsi namini huu ni mkakati wa serikali kutaka ama kufuta CDM, au kupiga vita mikutano ya CDM kabisa.
 
Back
Top Bottom