Sababu 11 za kwanini Lowassa anaweza kuwa Rais bora Tanzania

Umeleta hoja nzuri kweli, kwa maslahi ya Watanzania makini wenye uwezo wa kutenganisha siasa oevu, na ubishani wa mfano kama ligi za Simba na Yanga.

Wengi wanamwona Lowasa kama unavomwona wewe.
Mtu aliyechoka, aliyeishiwa na mikakati ya kisiasa, wala uwezo wa kujinyanyua kidogo tu, hana.
Ni kitendawili kwa maadui zake na hata kwa wapenzi wake, hawajui kwa nini Lowasa kabaki na umaarufu wa hilo jina tu Lowasa, Lowasa, basi lakini uwezo wowote mwingine anaotarajiwa kuwa nao Kiongozi, yeye hana.

Binafsi mie namwangalia Lowasa wa miaka ya 1990 akiwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi miaka ya 1993 hadi 1995, hadi Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, baadaye Maji na Uvuvi hadi miaka ya 2005 alipo ukwaa u Waziri mkuu chini Mheshimiwa JK. Alikuwa mchapa kazi wa kiwango cha kuridhisha tu, japo alikuwa na ufisadi wake uliomsababisha Baba wa Taifa kumkataa "macho pima" asigombee Urais.

Alikuwa vizuri tu, kiakili, kiafya, na ki fikra.

Mambo kumuharibikia huyu bwana kwa kiwango cha kutisha, ni tangu alipojiuzulu U Waziri Mkuu 2008, na kukaa pembeni bila uwajibikaji mkubwa katika kazi za kila siku, akabaki na kiu moja tu kuwa iko siku inakuja, watu watasahau kashfa iliomweka pembeni, na atarudi tu ulingoni, sio kudai Uwaziri wake tu, bali kuwania kiti cha juu kuliko vyote nchini, cha Urais.

Cha kushangaza na kutia simanzi ni pale sura yake iliporudi hadharani, tukamwona mtu aliyerudi, siyo yule aliyeondoka.

Kabla hatujapata nafasi ya kumsoma vizuri, tukasikia kang'olewa kuwania kiti hicho kwa ticket ya CCM, na alipoamua kuhamia upande wa Upinzani, tukaamini sasa yatatimia maneno ya Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatokea CCM. Binafsi nikataraji kusikia CCM inavyoanikwa mabaya maovu yake, rushwa zake, ufisadi wake nk. Kutoka kwa "mtu" anayekijua chama hicho kwa undani. Lakini aah! Haikuwa hivo. Jamaa hakuwa na lolote la kuwaambia maaelfu ya wapenzi wake waliomsindikiza kuchukua fomu ya Urais, bali akaninyong'onyeza kumsikia anasema, " Rafiki yangu Kikwete ameharibu uchumi wa nchi yetu" eti " alichukua nchi mchele ulikuwa unauzwa sh 600 lakini leo unauzwa elfu 2, ameharibu uchumi hakuharibu?
Kiberiti kilikuwa kinauzwa senti hamsini, lakini sasa kinauzwa sh mia mbili, ameharibu uchumi au hakuharibu?"
Hayo ndio material Lowasa anawamwagia waliomiminika kumsikiliza. Mie nikajiuliza siku ile kiberiti kilikuwa kinauzwa sh mia moja tu, hakijafika sh mia mbili hadi hii leo, Huyu bwana Lowasa kafanya utafiti kweli? Au anaghilibu akili za watu? Na kama atakuwa kiongozi wa ghilba kwa watu wake, kutakuwa na usalama kweli?

Tamaa yangu ikatikisika. Mheshimiwa huyu kweli, nilidhani maneno atakayotoa siku hiyo, kila mfuasi wake angerudi nyumbani kichwa kinasisimka kwa maneno ya hekima na busara, maneno yenyewe ndio yale?

Basi kilichofuata katika mikutano yake mingine kila mtu alikiona, akisimama, dakika zake ni mbili tu, anachokisema hakina mashiko, mwelekeo wala sera au kuonyesha dira, kila mfuasi wake anayemsikiliza hujifanya kamwelewa japo hakuambulia chochote. Waandishi wa habari waliokimpendelea, wakafanya kazi za ziada kumnyooshea maneno anayoyasema mikutanoni, ili yaweze kusomeka na kuleta maana katika magazeti yao.
Al muradi Lowasa alionyesha udhaifu mkubwa sana kama mwanasiasa, tangu na hapo hadi hii leo.

Sikuwa na jinsi ya kujua Lowasa kilimfika kitu gani, hadi akadorora kwa kiwango kile,
zaidi ya kufikiri tu kuwa ile miaka 8 aliyokuwa nje ya "Ulingo wa Siasa" ilikuwa imemdhuru vibaya mno.
 
Mtu anaeamini kuwa anafaa kuwa Rais kwa kuwa ni zamu ya Walutheran hatufai
Kuliko kuwa na Rais Fisadi ni bora nchi iishi bila ya Rais
 
1.Ni mvumilivu

2.Mzalendo wa kweli

3.Ni mzoefu katika siasa za taifa hili

4.Ni mbunifu

5.Ni kiongozi imara

6.Ana ushawishi

7.Ana huruma

8.Ni mkweli

9.Ana hekima na busara

10.Ana maamuzi yenye faida kwa taifa

11.Ni mchaMungu.
Amekua Mbunge wa Monduli kwa miaka zaidi ya 20 lakini wamasai wanakunywa mikojo badala ya majiiii teh teh teh. Mnaweweseka sana. Ndo ishatoka hiyo. Asubili kupewa uenyekiti wa bodi ya parole kama Lyatonga
 
Back
Top Bottom