Saadi Gaddafi aibuka na kukamatwa Mexico!

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,598
1,233
Jumatano, 07 Desemba 2011
Saadi Gadhafi akamatwa akitorokea Mexico

Al_Gadhafi_300x300_AP.jpg
Mpango wa kutoroka kwake uliongozwa na raia mmoja wa Canada akishirikiana na raia wa Mexico wawili.

Wizara ya mambo ya ndani ya Mexico imesema mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa zamanai wa Libya Moammar Gadhafi amekamatwa wakati akijaribu kuingia nchini humo kwa kutumia nyaraka za kugushi.

Pamoja naye watu wengine wanne wamekamatwa kuhusiana na njama hizo zilizofanyika mwezi novemba na kutangzwa jumatano.
Kukamatwa kwa wapangaji wa njama hizo zilizofanyika mwezi Novemba kulitangazwa jumatano.

Waziri wa mambo ya ndani wa Mexico Alejandro Poire amesema mpango ulikuwa ni kutoa nyaraka za kugushi kuonesha uraia wa Mexico kwa Saadi na familia yake na baadae kununua majengo kadhaa huko Mexico ambayo yatatumika kama hifadhi yao.

Moja ya nyumba zilizotarajiwa kununuliwa iko katika eneo la kifahari kwenye mji wa Bahia de Banderas katika jimbo la Nayarit.
Shirika la kijasusi la Mexico lilibaini kwa mara kwanza kuhusu mpango huo mwezi Septemba.

Aidha Poire anasema mawakala wa shirika hilo la kijasusi walifuatilia na kugundua kwamba Cynthia Ann Vanier raia wa Canada alikuwa kiongozi aliyewasiliana na familia ya Gadhafi na alikamatwa Novemba 10.

VOA
 
Duhu, VOA wamechemsha baab kubwa (zaidi ya Global Publishers wazee wa udaku!). Saadi hajakamatwa bali waliokamatwa ni wapambe wake waliokula njama za kumtorosha!

Mexico 'stops entry' of Libya's Saadi Gaddafi

_55356034_012892551-1.jpg

Saadi Gaddafi, 38, crossed the border into Niger in a convoy of vehicles in September

The Mexican authorities say they have stopped a plot by a criminal gang
organisation to smuggle one of the sons of Libya's ex-leader Col Muammar Gaddafi into the country.

Saadi Gaddafi has been under house arrest in the West African state of Niger since he fled Libya in September.

His lawyer, Nick Kaufman, denied Mr Gaddafi had ever tried to flout a UN travel ban and escape.


BBC


Nonda na Gang Chomba mpo?
 
Watu wengi wako katika kampeni ya kutaka NATO wafikishwe ICC, sasa kinachoendelea kwa sasa katika MS western media ni huu udaku na kuzusha habari za uongo kuhusu Aisha Gaddafi, ili bado iendelee kuwa Gaddfi family ndio news ili kuziba watu macho wasione u"shetani" wa US-NATO.

Je unafuatilia libya mpya? na mpango wa US-NATO syria?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom