Saa ya ukombozi Tanzania ni sasa?

Shansila

Senior Member
Jan 28, 2012
189
36
Mungu hawezi kushuka na kusema nasi katika hali ya mwili!Mungu husema na wanadamu kwa njia mbalimbali!Mungu anasema na watanzania kupitia mgomo wa madaktari unaozidi kuwa na sura mpya kila siku nchini huku ukiendelea kugharimu maisha ya watz wanaougua kwa sasa.

Tunaweza kusema vyovyote,lakini hakuna ajuaye lini atakuwa mgonjwa na endapo atapata matibabu!Tuache ushabiki wa kisiasa,tuwaunge mkono madaktari tuikomboe Tza.Tunawezaje kuongopewa kirahisi kuwa serikali haina hela?

Kama hakuna hela,maazimisho ya miaka 50 ya uhuru & 35 ya CCM yangekwama,safari za nje za viongozi zingepungua!Tunawezaje kudanganywa kuwa nchi haina hela wakati Wazungu wametapakaa nchi nzima kupora madini mfano gas,almasi,dhahabu,uranium,mafuta n.k?

Wengine wamenunua mbuga zetu za wanyama na kupora rasilimali zetu kama vile hatupo?Kama watz tutasema imetosha na iwe hivyo sasa!
 
Kaka Kamugisha,niunge mkono,lkn nakusihi tusimwage damu,tushawishi strike ya nchi nzima na isiyokoma mpaka tumtoe mkoloni.
 
Maumivu ya kichwa huanza polepole,mwisho utasikia maumivu makali kupita kiasi........Hivi hii ina viongozi kweli?Hata mkuu wa kaya kauchuna 2...Hv kulikuwa na raha gani kutumia gharama kwa maadhimisho ya chama wakati madaktari hali ni tete?Ama kweli hii ni nchi iliyo chini mfalme juha.
 
Hakika saa ya ukombozi ni sasa na bahati haiji mara mbili jamaa wametuanzishia ni juu yetu kuamua nasi kuwaunga mkono hata kama ni kwa kuingia barabarani labda ndo mwenye nyumba atavunja ukimya
 
Kauli kama hii title yako ilitolewa miaka mingi iliyopita na wenzako wanaojiita wakongwe wa siasa na watanganyika halisi lakini hadi leo haijafanya kazi.
 
Hakika saa ya ukombozi ni sasa na bahati haiji mara mbili jamaa wametuanzishia ni juu yetu kuamua nasi kuwaunga mkono hata kama ni kwa kuingia barabarani labda ndo mwenye nyumba atavunja ukimya

Huna kumbukumbu sahihi, kauli hii ilikuwepo miaka mingi sana na migomo imekuwepo mingi tu lakini hakuna hata mmoja ulioonekana kuwa chanzo cha ukombozi unaousema
 
Mungu hawezi kushuka na kusema nasi katika hali ya mwili!Mungu husema na wanadamu kwa njia mbalimbali!Mungu anasema na watanzania kupitia mgomo wa madaktari unaozidi kuwa na sura mpya kila siku nchini huku ukiendelea kugharimu maisha ya watz wanaougua kwa sasa.

Tunaweza kusema vyovyote,lakini hakuna ajuaye lini atakuwa mgonjwa na endapo atapata matibabu!Tuache ushabiki wa kisiasa,tuwaunge mkono madaktari tuikomboe Tza.Tunawezaje kuongopewa kirahisi kuwa serikali haina hela?

Kama hakuna hela,maazimisho ya miaka 50 ya uhuru & 35 ya CCM yangekwama,safari za nje za viongozi zingepungua!Tunawezaje kudanganywa kuwa nchi haina hela wakati Wazungu wametapakaa nchi nzima kupora madini mfano gas,almasi,dhahabu,uranium,mafuta n.k?

Wengine wamenunua mbuga zetu za wanyama na kupora rasilimali zetu kama vile hatupo?Kama watz tutasema imetosha na iwe hivyo sasa!

Mungu hajaagiza muitafute haki kwa uasi ila kwakuomba kupitia Jina lamwanae Kristo Yesu tutapewa chocote tutaka
 
Back
Top Bottom