Saa ya Fisadi mkuu

Firigisi

Member
Feb 13, 2009
91
33
Jamaa mmoja aliota amekufa na kuchukuliwa na malaika hadi mbinguni. Alipofika mapokezi ya mbingu akashangaa kuona ukutani kuna saa nyingi sana, akamuuliza malaika wa mapokezi “hizi saa za nini? Malaika akamwambia “hizo ni roho za watu, ukiona inatembea ujue mtu huyo anafanya dhambi, na ukiona inaongeza mwendo (speed) ujue mtu huyo anafanya dhambi mbaya sana”.

Jamaa akauliza “mbona ile imesimama?malaika akamwambia ” hiyo ni ya mtakatifu mmoja, yeye huwa hafanyi dhambi kabisa”.

Kwa udadisi zaidi jamaa akauliza ” Saa ya yule fisadi mkuu katika nchi yetu iko wapi? Malaika akamwambia “hiyo inakaa ofisini kwa Mungu mwenyewe” Kwa mshangao mkubwa jamaa akauliza “kwa nini?
Malaika akamjibu “hiyo Mungu anaitumia kama feni…
 
Eeeh, mbona nchi yetu tear and wear itakuwa kubwa sana speed siyo mchezo wa mishale ya saa.:wave:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom