RwandAir Haoooo!

Honorable Kagame is bringing real change in Rwanda. May God give him more strengths so he see his plans accomplished for the people of Rwanda. Yangu macho mie katka Jumuiya ya Afrika Mashariki. May Rwanda show Tanzania the way forward. :D
vERY PAINFUL THRUTH. mAY gOD HELP US
 
Hawa jamaa wa Rwanda wapo serious kwenye mambo mengi tu. Kuanzia Kigali centre mpaka mpakani mwa DRC (Mji wa Goma), kuna lami ya ukweli hasa. Nadhani hata kutoka Nyakanazi mpaka mpakani mwa Rwanda, barabara ni ya ukweli pia

Kagame nchi anaiendesha kijeshi. Waziri unapresent workplan zako, wizara inapewa fwedha na next year, unawekwa kitimoto ulete feedback pesa imetumikaje as compared na output. Sio blah blah kama zetu huko bungeni kati ya mawaziri na wabunge kila mwaka wa budget. Wizi mtupu
 
Nafikiri ni vizuri kujifunza toka Rwanda. Kagame amedhihirisha kuwa kiongozi makini katika mikakati ya maendeleo ya taifa lake. Sisi janja yetu hivi imeishia katika kutafuta wawekezaji na kuwaachia masuala yote ya mikakati. Tusubiri Air Sonangol watakavyoipaisha (au kuizamisha) ATC.
 
Thats why I believe in competition. Thats why I believe in the EAST AFRICAN COMMUNITY. Ngoja kwanza wanaojua priority zao watupige bao nadhani ndo tutaamka. Ngoja kwanza tuwe wapagazi kwenye nchi yetu ndo tutajua what globalization means! Tumeilaumu sana Kenya kwa mengi, wakati jamaa wanainvest kwenye ingenuity yao. Sasa sijui kwa Rwanda nchi ambayo ilikuwa na almost nusu ya raia wake wakilishwa makambini kama wakimbizi pale Ngara na Kigoma, leo wanatupiga bao tutasingizia nini. Ohh nearly forgot, apologetics watakwambia kwamba Kagame ni dictator!

May the best brain earn the reward. So I say! I really hope that this competition will make people wake up! Kwa mwendo huu wa kukalia porojo na kutafuta wa kumlaumu, Tanzania we are in for the long night. To make any progress, we need to take responsibility. Period. Huwezi panda mahindi ukategemea mpunga. Ukichagua mediocre leadership, expect mediocre results.

Viva Rwanda, viva EAC. Viva Tanzania

Masanja,
 
Thanks God, Kenya Airways na Ethiopian walikuwa wanatuibia!!!!!!!! wezi wakubwa. Sasa ushndani utapunguza bei.
Lakini jamani mbona mnaimba sana eti Rwanda imeendelea? Nani kaenda kule?
Mjomba, nikipata nauli ntaenda Kigali na Rwanda air. Nione kama kweli hizo nyimbo ni kweli au mnaimba vibwagizo vya nyimbo msizojua. Sidhani kama Rwanda imeendela kama Tanzania, sidhani kama Kigali ni nzuri kama DSM.

Mwenye pesa anasaidie niende, ntawajuza nitakachokiona. Plese JM lazima mtu aende
ulichosema nikweli jamaa wanatafuta public attention,na maendeleo kidogo ni hapo kigali tu,ambayo waweza fananisha na mkoa wa mbeya tu.ukitoka nje kidogo ni soo tupu,hata hivyo penye ukweli tuwasifie jamaa wana jitihada kali sana ya maendeleo natamani tungebadilishana,kiwete aende kule kagame aje hapa tz,yaani ingekua raha sana mafisadi wetu wangechezeshwa kadance mpaka matumbo yangenywea kabisa.
 
sidhani kama tunahitaji shirika la ndege la taifa.
serikali inatakiwa iache ATC ife kabisa kabisa na isitoe hata shillingi moja
ATC ni mzigo kwa taifa
Precision wanafanya kazi nzuri na ni wakati wa kuingalia precision kama ndege ya taifa.

hela ya kuipa ATC zitumike kwenye kujenga viwanja vya DAR na KIA ili viwe kwenye hali ya kimataifa
 
Thats why I believe in competition. Thats why I believe in the EAST AFRICAN COMMUNITY. Ngoja kwanza wanaojua priority zao watupige bao nadhani ndo tutaamka. Ngoja kwanza tuwe wapagazi kwenye nchi yetu ndo tutajua what globalization means! Tumeilaumu sana Kenya kwa mengi, wakati jamaa wanainvest kwenye ingenuity yao. Sasa sijui kwa Rwanda nchi ambayo ilikuwa na almost nusu ya raia wake wakilishwa makambini kama wakimbizi pale Ngara na Kigoma, leo wanatupiga bao tutasingizia nini. Ohh nearly forgot, apologetics watakwambia kwamba Kagame ni dictator!

May the best brain earn the reward. So I say! I really hope that this competition will make people wake up! Kwa mwendo huu wa kukalia porojo na kutafuta wa kumlaumu, Tanzania we are in for the long night. To make any progress, we need to take responsibility. Period. Huwezi panda mahindi ukategemea mpunga. Ukichagua mediocre leadership, expect mediocre results.

Viva Rwanda, viva EAC. Viva Tanzania

Masanja,

Haya maneno yamenigusa! Watanzania ugonjwa wetu ndo hapo!
 
Probably Tanzania tunaponzwa sana na amani. Amani hiyo inatufanya tusiwashambulie viongozi walioshindwa kutekeleza majukumu yao. Rwanda 9na sasa Congo) wanakwenda vizuri sana kiuchumi kwa sababu hawana upuuzi wa "huyu kiongozi ni mwenzetu;" kiongozi yeoyte akivuruga, naye unavurugwa papo kwa papo. Kenya wana utaratibu wa aina hiyo siku nyingi sana na ndiyo maana wameendelea kiuchumi kuliko sisi.
 
ndio maana wananitibua sana wapinzani ati hata kama sheria ni mbaya za uchaguzi wako tayari kujaribu kushinda kwa kutumia sheria hizo hizo mbaya! Ingekuwa nchi nyingine watu wangeandamana mpaka kieleweke.
 
Kagame ameweza kuchochea maendeleo huko Rwanda sawa nakubaliana na hilo lakini hakuna Demokrasia huko!

Ingawa si muhimu sana ukichukulia historia ya Rwanda; nadhani Tanzania tunahitaji mwanajeshi kama Kagame! walau kwa miaka 5!
 
si tumechagua rais handsome, check bob, tunategemea nini? kaiz ni kwenda kutembelea ulaya na kujijumuisha ktk majukwaa ya marais wa nchi tajirir kana kwamba na yeye ni rais wa nchi tajiri! sio wote ila izo ndio tabia za watu wa pwani! sifa bila maendeleo.
 
Hata kucheka cheka nayo ni kazi pia wakuu....dont forget that!!
 
ndio maana wananitibua sana wapinzani ati hata kama sheria ni mbaya za uchaguzi wako tayari kujaribu kushinda kwa kutumia sheria hizo hizo mbaya! Ingekuwa nchi nyingine watu wangeandamana mpaka kieleweke.

Kusema kweli jambo hili nimeshaliwaza sana MM. Sidhani kama kuna sababu yoyote kwa chama chochote cha siasa kushiriki uchaguzi Tanzania. Ni vyema wakapiga full-stop! na kumwambia msajili na wasimamizi wa uchaguzi NEC "Natioanal Election commision, whatever they call themselves, kama wanataka waende kushiriki peke yao. Wabunge wa upinzani wangesema huu ni mwisho kama katiba haibadilishhwi ikafanana na ya " A true democratic Country" basi hatupo tena Bungeni. Tena waseme wote sasa Wanajiunga na CCM ili iwe wazi zaidi kuwa Katiba ni ya Chama kimoja! Na uchaguzi uwe ni wa chama kimoja. BASI!
 
11th February 2010 (Ippmedia)


RwandaEmbassy%281%29.jpg

Balozi wa Rwanda nchini, Fatuma Ndagiza, akifurahia jambo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika makao makuu ya IPP, jijini Dar es Salaam jana.



Balozi wa Rwanda nchini, Fatuma Ndangiza, amemwomba Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, kuhamasisha wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kwenda kuwekeza nchini humo.
Aliyasema hayo jana ofisini kwa Mengi ambako walikutana na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa Rwanda na Tanzania.
Balozi alisema Rwanda imejitahidi kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na imekuwa ikiwapokea kwa mikono miwili watu wanaokwenda kuwekeza nchini humo.
“Wewe ulikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) hivyo unaushawishi mkubwa, tunaomba utusaidie kuwaeleza Watanzania na wawekezaji wengine duniani kuwa Rwanda kuna fursa nzuri za uwekezaji na mazingira yameboreshwa, tumeondoa kabisa ukiritimba na hatuvumlii hata kidogo vitendo vya rushwa, ” alisema.
Alisema serikali ya nchi hiyo imekuwa mwiba kwa wala rushwa kwani haina mchezo kabisa na watu wanaopata tuhuma za aina mbalimbali.
Alisema watumishi wa umma wanapoingia madarakani Sheria inawataka wataje mali zao na wanapotoka pia wanatakiwa kufanya hivyo na wasiofanya hivyo wanachukuliwa hatua hali.
Alisema kuonyesha kuwa serikali haina mzaha katika suala hilo, hivi karibuni iliwasimamisha kazi kwa miezi sita watumishi 130 ambao hawakutaja mali zao na watalazimika kulipa faini.
Balozi Ndangiza alimsifu Mengi kwa kuwekeza kwenye vyombo vya habari ambavyo alivielezea kuwa ni sauti ya wanyonge.
“Watu wengi wanaogopa kuwekeza kwenye vyombo vya habari, wanapenda kuwekeza sehemu ambayo inafaida ya harakaharaka lakini wewe kwa kweli umesaidia sana jamii katika upatikanaji wa habari na sisi tunapata habari nyingi sana kutoka Tanzania kupitia kituo cha ITV na EATV na tunakuomba uje uwekeze kwetu Rwanda,” alisema.
“Kabla ya kuja Tanzania mwishoni mwa mwaka jana nilikutana na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, wakaniambia ukienda Tanzania mtafute Mengi ni rafiki yetu na tunapenda aje kuwekeza Rwanda, ndiyo maana nikawa natafuta nafasi ya kukutana na wewe,” alisema.
Kwa upande wake, Mengi alisema wakati nchi zinahamasisha uwekezaji kutoka nje, wawekezaji wa ndani nao lazima wawekewe mazingira mazuri na wapewe moyo.
Alisema imekuwa kawaida kwa nchi za Afrika kuwakaribisha kwa mikono miwili wawekezaji kutoka Ulaya na Marekani lakini wale wanaotoka kwenye nchi zao hawathaminiwi ipasavyo.
“Wawekezaji wazalendo ni muhimu sana na ndiyo nguzo kuu ya uchumi maana ukitokea mtikisiko wa uchumi wawekezaji wa nje wanaondoka zao lakini wazalendo wanabaki, hapa Tanzania mwaka jana kulikuwa na wawekezaji wengi waliokuwa wakitafiti madini lakini ulipootokea mtikisiko wakaondoka,” alisema.
Mengi alisema Rwanda ni mfano wa kuigwa kwa kukaribisha wawekezaji vizuri na imepiga hatua kubwa kiuchumi katika kipindi kifupi.
“Niliwahi kwenda Rwanda kutafuta fursa za uwekezaji, kweli mlinikaribisha vuzuri sana, mimi na kwa niaba ya wafanyabiashara wenzangu nawapongeza sana kwa hatua kubwa mliyofikia maana mmefanya maajabu makubwa,” alisema.
 
Back
Top Bottom