Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
SHIRIKA la Ndege la Rwanda (RwandAir) linatarajia kuzindua rasmi safari zake za ndege za kutoka Dar es Salaam kupitia Bujumbura kuanzia kesho.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi yake iliyoko jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa huduma hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Asubuhi saa moja muda wa Rwanda ndege zitaondoka kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kigali kila siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili pia zitaondoka Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa tano asubuhi kwenda moja kwa moja Kigali, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa shirika hilo la ndege linakusudia kuongeza zaidi njia na safari zake mara itakapokamilisha ununuzi wa ndege aina ya Boeing 767 na 737-800 Machi.
Muda si mrefu tutatoa ofa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia 2010 mara tutakapoanza safari za moja kwa moja kutoka Kigali kwenda JBurg Afrika ya Kusini, iliongeza taarifa hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima
My Take:
I remember them day; Serengeti yetu ikitua Bujumbura!