Rwandair - CRJ900 Next Gen arrives KIGALI on 5th Nov 2012

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Baada ya kuleta Ndege nyingine Crj next generation 900 Oct 2012
Naona sasa Kampuni ya ndege ya Rwandair inaongeza tena ndege nyingine
tar 5 Nov 2012 nasasa kuwa na ndege 7 za kwao
Tunawatakia kila la kheri kwenye anga za ndege
 
All the best!!! hivi yule chizi wa air Tanzania bado yupo. Mie nashangaa mtu anaitw chiz halafu unampa shirika wabongo bwana!!
 
Yaani hapa ndipo nafikaga mahali nawza hivi hii nchi Tanzania imelaaniwa na nani!!yaani
kanchi ka Rwanda kana ndege saba za kununua,sisi ndio kwanza tunawaza kukodi!!!!!
Ee Mungu tuhurumie watanzania,tutoe kwenye giza na laana ya mafisadi.
 
Kama hii

crj900-lufthansa.jpg
 
Nchi yetu inaangalia siasa tu, vitu muhimu kama kuwa Shirika la Ndege imara imeshindikana, siyo kurogwa ni kutokuwa na uhamuzi.
 
yanayoua mashirika sio managers bali ni ukubwa wa shirika na udogo wa mapato, hebu angalia shirika lina wafanyakazi wangapi na wana ndege ngapi? manager anashindwa kuendesha hizi ajira za mjomba na shangazi ndizo zinazoua shirika hebu tafuta wapi umeona tangazo la kazi shirika la ndege hapa TZ? lakini kila leo wameajiriwa wafanyakazi wepya, bodi ya shirika kila mwaka inatumia zaidi ya mshahara wa captain kumi kwa mwaka hivi bodi inafanya nini kuweza pewa hela yote hiyo? shirika halina pesa lakini bodi haikuvunjwa na wanalipwa kila mwezi
 
Halafu mijitu inakaa kumsifia Waziri fulani ambaye kachukua Mabehewa na Vichwa vya Train vya kwenda bara na kuviweka Dar wakati train lenyewe linafanya kazi kwa usanii mkubwa.

Hivi huwa hatuangalii Wanaume wa shoka wanapofanya kazi?

Kweli Watanzania RAHISI sana kuwanunua. Hata kwa kitu chao pia watataka kununua.

Kuna siku wataomba hata WAUZIWE wake zao wenyewe na wakishauziwa kwa BEI NAFUU, wataanza kuishukuru Serikali kwa kuwaonea huruma na kuwauzia wake zao kwa bei nafuu sana. Si ajabu wakaombwa na RUSHWA ili waweze kuwanunua wake zao wenyewe. Na akina mama wataambiwa hivyo hivyo kuwanunua waume zao.
 
Mbona bado! hivi sasa Rwanda inajiandaa kuwa Hongkong ya Africa tutakuwa tunashop karibu sana
 
Kungetokea machafuko na mauaji wakati wa kipindi hiki cha uamsho na tungepigana na kuchinjana perhaps ingetusaidia sana kama ilivyowasaidia Rwanda. Maendeleo hayaji hadi huu upuuzi wa sijui amani uishe na tushikishane adabu
 
Halafu mijitu inakaa kumsifia Waziri fulani ambaye kachukua Mabehewa na Vichwa vya Train vya kwenda bara na kuviweka Dar wakati train lenyewe linafanya kazi kwa usanii mkubwa

NDG MTOA HOJA sikonge maelezo yako hapo juu inaonyesha wewe una matatizo na chuki binafsi moyoni mwako!

maana hayana mashiko na hayajengi wala kutia moyo!
 
[yanayoua mashirika sio managers bali ni ukubwa wa shirika na udogo wa mapato, hebu angalia shirika lina wafanyakazi wangapi na wana ndege ngapi? manager anashindwa kuendesha hizi ajira za mjomba na shangazi ndizo zinazoua shirika hebu tafuta wapi umeona tangazo la kazi shirika la ndege hapa TZ? lakini kila leo wameajiriwa wafanyakazi wepya, bodi ya shirika kila mwaka inatumia zaidi ya mshahara wa captain kumi kwa mwaka hivi bodi inafanya nini kuweza pewa hela yote hiyo? shirika halina pesa lakini bodi haikuvunjwa na wanalipwa kila mwezi]

Ushauri wa bureeeee.. kwa ujumla Shirika la ndege TZ limebaki kuwa kichekesho na marumbano Wizarani na wadau tu. Kibiashara ATCL aipaswi kuwepo. Ushauri kwa serikali vunjeni hilo shirika mkiwa tayari anzisheni shirika jipya likiwa na uongozi mpya siyo hawa janja janja.
 
Back
Top Bottom