Rwanda yapiga marufuku adhana na miziki makanisani

..wengine ambao tunaishi karibu na misikiti na makanisa adhana na kengele ndiyo alarm clocks zetu za kutuamsha asubuhi.

..inawezekana Kagame kajipatia tenda ya kuagiza alarm clocks Rwanda, sasa hapo anajaribu kuondoa upinzani ktk soko/biashara.

...sio kila mtu ni fisadi kama CCM,maana ndio kila kitu wanachofanya motive kwao ni 10%!
 
mnajua maana ya religion tolerance, tusimsupport tu kagame tu, maeneo kama SA mbona kanisa na miskiti wanaendeleza mambo yao kama kawaida....sheria hiyo haifai TZ kwani sisi ni watu wa kupendana na umoja popote pale unapo mkuta m tZ hasa nje ya nchi na wenzake utaligundua hilo

...hakuna mtu ameingiliwa dini yake hapo lakini ibada zao zisiwe usumbufu kwa wengine,nchi lazima iwe na sheria ili watu waheshimiane.
 
Du ndugu yangu hapa nadhani unahitaji kuelimishwa tu, huo uchafuzi wa mazingira kwa sauti/kelele ni lazima viwango fulani vifikiwe ndio uchafuzi huo utimie, na kwa sauti za makanisa na misikiti nyingi hazifiki huko. Kwa karne hii kiongozi wa kuigwa si yule mbabe bali anayetawala kwa misingi ya kidemokrasia, hapa inamaanisha uhuru wa kuabudu pia. Kwa kigezo hicho tu Tanzania haipaswi kuiga kutoka kwa Kagame ila Kagame anapaswa kuja kujifunza hapa ni kwa jinsi gani raia wenye dini mbalimbali wamepewa fursa ya kuabudu na uhuru wao unalindwa katika katiba ya nchi(tazama ibara ya 19 katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2006.) Huo usumbufu kwa raia una maanisha raia gani tena ambao si waumini? unajua kwa sasa watu wasio waislamu wala wakristo ni chini ya asilimia 2 tu? tena wengi wa hao wanafuata imani nyingine na za kiyahudi, kibudha n.k ambazo zinasitiza umuhimu wa uhuru watu kuabudu.
Elewa mwandishi alichoseme.HAJAWANYIMA UHURU WA KUABUDU.Bali wamekatazwa KUPIGE KELELE? Mungu anayeyaona ya moyoni hata kabla hujayatamuka iweje leo mpige makalelele hivyo.hata kwa hao mabwana zetu dini zilipochipukia hawapigi kelele hivyo.Na mimi nakerwa kweli.
 
kwa muumini yeyote anaye jua kusali hata subiri adhana bali natakiwa kujua muda kwisha...hongera kagame......
 
Kama Generali Kagame kalewa madaraka, nivizuri apumzike awapishe wengine amabao bado wanakiu ya kuongoza nchi. Kwa serikali kuingilia uhuru wa kuabudu ni sawa na mwanadam kujichimbia kaburi yeye mwenyewe.Ni vizuri Bw Kagame ajifunze kwanza yanayotokea Notthern and South Ireland baina ya wakatoliki na wa Protestant,kiaha ajifunze yaliotokea nchini Afghanistani baina ya waislam na utawala wa kikominist chinin ya USSR. Kisha namuomba Bw Kagame arejeshe kumbukumbu zake za kihistoria kwa yale yaliotokea South America, baina ya Wkatoliki na srikali ya Fashist Samoza wa Sadinista.Siku zote wa Mungu ndio hushinda na sio watu wa shetani. Hii ni ishara ya wazi kuwa Bw Kagame sasa aanza kuporomoka kihadhi hasa baada ya kufanikiwa katika mageuzi ya kiuchumi tangu atawale nchi Rwanda takribani miaka 14 iliyopita. Ama kweli Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Sasa Kagame achafua mandhari ya mema yote aliyoyafanya kwa Wanyarwanda. Kama yeye ni an Atheist/Agronist, isiwe ndiyo sababu ya kuwazuwilia watu wangine kutekeleza yale yaliomo katika imani zao za kidini.Huu ni ushetani na kamwe hauwezi kuvumilika na hatimaye ni kuzuka vita vingine ambavyo vitapelekea kumwagika kwa damu za Wanyarwanda wasio na hatia bure breshi.Kagame hapo umechemsha kama si kupasha moto.
 
Inaonesha mwisho wake hauko mbali. Hizo ni dalili za kulewa madaraka. Mwisho atasema makanisa na misikiti yote yafungwe. Hajui kama dini ina umuhimu wake ktk kuhamasisha maadili mema kwa wananchi.
 
Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka. Hii ni kwa sababu uhuru kwako wewe unaweza kuwa kero kwa mwingine. Ndo maana kuna sheria. Je, Al Qaeda waachiwe full uhuru kulipua watu? Wale wenye ibada za kuchinja maalbino waachiwe uhuru kamili? Wale wenye ibada za kuchuna ngozi nao waachiwe uhuru kamili? Dogo Rama nae apewe uhuru bila mipaka? Majambazi, vibaka na wabakaji nao wapewe uhuru kamili? Si wana haki?

Kwa binadamu yeyote mwenye akili timamu, kelele wakati mwingine ni kero. Mtu unapotaka kulala usiku na mwingine anapiga kelele, iwe ni burudani au ya kidini, hiyo ni kero.

Wakubwa nchi hii wanafahamu hiyo. Maeneo wanayokaa wakubwa (O'bay, Masaki, Mbezi Beach, Upanga, nk) huwezi sikia kelele za misikiti, makanisa wala mabaa. Juzijuzi tu hapa Leaders Club wamepigwa marufuku kufanya shughuli za kelele kwasababu wakubwa wanaokaa karibu wanapata disturbance na wakashinikiza sheria ifuatwe.

Huko uswahilini ambako wengi wanaoishi huko ni malimbukeni ndo wanafurahia na kushabikia makelele. Wachache wanaokerwa na kelele za huko uswahilini ni vijana wasomi wanaoanza maisha kwenye nyumba za kupanga.

Sheria za kuzuia disturbance za kelele hazitekelezwi huko uswahilini kwa sababu ya ulimbukeni. Rwanda wanaondokana na ulimbukeni na ni mfano wa kuigwa.
 
WAUNGWANA NA MIMI MJOMBA WA MOROGORO LAZIMA NISEME SIKUMPENDA JULIUS NYERERE!
Watanzania amkeni , ila bado namuheshimu kwa misingi aliotuekea kwani mfano ni Mzee Chiluba aliitangaza Zambia is a christian country si anakumbana na adhabu za Mungu sasa nafikiri kila mtu anaona Chiluba anavyotumika adhabu hapa hapa duniani. Watanzania siku zote musikubali kutumiwa na viongozi wadini , Nyerere alisema pale Mbeya mwaka 1995 kuwa kuna wale wasomali wote waislamu ila wengine wana nywele ngumu na wengine nywele laini angalieni wanayouana namaliza maneno ya Julius Nyerere. Wanasiasa waache kuingilia dini ,Pengo alitoa onyo hilo karibuni, Nawarudisha kwa Brother Kaguta Museveni aliwarudisha MA Chief na Kings KABAKA for political gain leo si munaona vipi Uganda inavyo kumbana na yale yale aliyoyakataa Nyerere ya ukabila na Udini , Kina Mangi Mkuu na Fundikiria wangekua na power ya Uchifu wao leo Tanzania tungekua kama Uganda tumegawanyika ila angalieni ukiend Mtwara Mangi yuko , Mpemba yuko , Mmakonde yuko ,Mnyachusa yuko. Kagame is not model for Watanzania we should proud our self who we are we cant be like Rwanda, Burundi or Congo , or Wajaluo we are Wabongo mix no Religion can rule us look recently Zanzibar ubaguzi unayowatafuna Wapemba na Wangazija wanvyobaguliwa kwa maslahi ya Kisiasa tusikubali kutafunwa na ubaguzi wa kidini au kikabila angalieni Dunia inayotaulaani Watanzania kwa kuuwa Albino lets unite and create Tanzania ALbino Foundation and donate money to help these people . Mjomba Mloka Morogogoro. Turiani.
 
Hivi na nyinyi mna nyumba gani ambazo makelele ya nje yanaishia ndani? acheni kulaumu waumini jengeni nyumba bora ili muepuke kelele za mitaani, na pia mtusaidie na sisi na makelele yenu huko vyumbani yanatupa wakati mguu tunapopita karibu na madirisha yenu na watoto wetu....utasikia baba mbona mama nanii analia?

Kijana Umepinda......
 
Jamani..sound doesnt matter peace is louder than voice -thats why we fall in to confrict!!
what you think is haven is a hell to some one who dont think so!!

Rwanda think that is not noise people are washiping !!

Rwanda acheni ubaguzi think kwanini ukae kwenye kelele...
sipendi hili wazo!!
 
hueleweki, kelele si ibada wewe,unawahubiria walioko nje au waliohudhuria?tena inapokuwa bugudha inafifisha hata maana ya ibada.njue kuna wagonjwa, wtoto wamelala,watu wamechoka halafu mijinga kuchaa inapiga kelele,si waislamu hata walokole wale wa kuimba kucha,baa miziki mtani,marufuku,big up baba kagame tutaiga mfano wako tukishaing'oa ccm
 
Hili ni suala la mipango miji- Dogo kua na heshima na wakongwe!! hivi ume tumwa na serikali ya Rwanda nini?-

Mipango miji waangalie wapi watoe au wajenge msikiti/kanisa la kakobe /ukumbi wa hip hop/ viwanja vya michezo-- huu wote ni upumbavu tuna shindwa nini kuandaa mazingira ili kuondoa vurugu zisizo kua na sababu!!...

mkileta mzaa nita wazalilisha!!
 
mipango miji wewe dogo hakuna tanzania tutasubiri hadi tufe,halamashauri bado saaana tuu,iliyopo tuondoe kelele kwanza mipango itafuata bidae kwani tushashindwa,hivyo huu uhuru wa kupiga makelele hovyo usimame,kwanza ni kosa kisheria kupiga makelele tosha kabisa kumtia mtu au kikundi hatiani!!so mipango wait till 2030 may be! kwani changes zinatokea at the speed of a snail!
 
Tulia tupo kazini...
kua na heshima...sio unaropoka ropoka una cheka cheka...
Dogo haya makelele yanapoteza Mbwa...

acheni dhalau...
 
Kagame is right, unajua kuabudu ni uhuru sasa isiwe taabu kwa watu wengine, halafu mimi sioni point watu kuanza kuchangia kuwa Kagame amepotea au amelewa madaraka, angelewa madaraka basi angepiga dini marufuku, lakini alichopitisha ni watu kuwa waastarabu na kuabudu pasipo kubughudhi wengine, kwani nani alisema pasipo abudu kimya kimya Mungu hasikii------------mimi huwa nakereka na haya mapokeo ya kusali huku watu wakilia na kupiga muziki utafikiri sasa watu wamefungulia dansi, tuwe waastarabu na tusali kwa utulivu nafikiri Mungu atatusaidia tu na kusikia maombi yetu.

Rom
 
kagame ana weza akawa mvuta Bangi tu au alisha wahi kufanya hivyo...

kumbuka hawa jamaa wana jaribu vitu ambavyo sometime results ni mabaya
 
Back
Top Bottom