Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,785
Ndugu wana JF,

Wakati tunaangalia kulia na kushoto ili kuifanya nchi yetu ipate viongozi yule ambaye kila mtu anamtaka , naona bado natatizwa na hiki kitu kinachoitwa ruzuku!

Ni kweli ruzuku itolewayo na serikali kwa vyama vya upinzani inaweza ikawa ni chachu ya mabadiliko nchini, lakini pia inaonekana kama ni chanzo cha matapeli wachache kuitumia vibaya, wengine kwa uroho tu, wengine wamekosa ajira na sababu nyingi zifananazo na hizo.

Napendekeza :

1. Ruzuku itolewe mwaka mmoja tu kwa vyama vinavyoanza;na kuwe na ufuatiliaji wa hali ya juu, juu ya matumizi ya hizo fedha au

2. Isitolewe kabisa, kwa sababu:

(a) Kila chama kizuri chenye sera nzuri kitakachowavutia wananchi ni dhahiri kitapata wanachama wazuri watakaohakikisha wanakitunza chenyewe na watu wake.

(b) Hali ya sasa hivi hata kama tutasema tunataka demokrasia ni dhahiri utitiri wa vyama hivi, unaleta

- Uadui kati ya wenyewe kwa wenyewe!

- Wengine kuona basi CCM iendelee tu maana vyama vingi vimeshajizolea umaarufu, aidha wataleta fujo na mara nyingi wanapigana kwa sababu ya fedha. N hii imeongeza hofu ya watu wengi kuwapigia kura hawa wapinzani.

- Kudhihirisha kuwa vyama vingi vinataka fedha tu, utavisikia wakati tunakaribia uchaguzi!!

Tukiwa na vyama ambavyo wananchi ndio wanaokiendesha, tutapata viongozi wanaowajali zaidi wananchi. Tutapata viongozi amabo hatima ya maamuzi yao ni kwa manufaa ya wananchi.

Kwa jinsi hii tutatengeneza akinaTsavangirai wetu akina Riala Odinga n.k

Viongozi wengi wa siasa hasa wapinzani , wawajabike wasiwajibike mwisho wa mwezi hela watapata tu.

Ni heri kupunguza vyama viwe vichache vya kiwananchi zaidi kuliko hali ya sasa. Afadhali hizo hela ziende mahospitalini n.k

Tukiangalia kwa undani sasa , hali hii ya kupewa ruzuku haitapelea vyama vya upinzani kushinda, sana sana tumeona migogoro ya ruzuku kila siku na watu kufanya ofisi za vyama kama vijiwe.

Pia kwa vyama vya siasa vikongwe, sijajua wana miradi gani, na wamewaza nini ili kupata income zao!

Naamini ubunifu wa kupata hela kwa njia ya halali , ndio ubunifu huo utahitajika pindi watakaposhika nchi.

Naomba chama, haswa kile kinachoona kiko tayari kujiendesha kwa nguvu ya umma, kiwe cha kwanza kusema hatutaki ruzuku , hizo fedha ziende hospitalini!

Vyama vikishuka chini, vikawa havina hela na viongozi wake waanze kuishi maisha ya kulingana na fedha za wanachama, wala yasiyo ya kifahari. Hawa vingozi watakuwa viongozi wa kweli.

Baadhi ya vyama vya siasa tulivyonavyo kamanilivyopata kwenye wikipedia ni:

• Chama Cha Mapinduzi (Revolutionary State Party)
• Civic United Front (Chama Cha Wananchi)
• Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
• Tanzania Labour Party
• United Democratic Party
• Chama cha Haki na Usitawi (CHAUSTA)
• Democratic Party (DP)
• Demokrasia Makini (MAKINI)
• Forum for the Restoration of Democracy (FORD)
• Jahazi Asilia
• National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR)
• National League for Democracy (NLD)
• National Reconstruction Alliance (NRA)
• Popular National Party (PONA)
• Sauti ya Umma (SAU)
• Tanzania Democratic Alliance (TADEA)
• Progressive Party of Tanzania-Maendeleo (PPT-Maendeleo)
• Union for Multiparty Democracy (UMD)
• United People's Democratic Party (UPDP)

Naomba tujadili

wakatabahu

Waberoya

Update:

Msimamo wangu haujabadilika-2011 April

Msimamo wangu haujabadilika-2012 May

Msimamo Wangu haujabadilika 2014 January

Msimamo Wangu haujabadilika 2015 November

Last edited by a moderator:
Ruzuku iondolewe kwa vyama vyote vya siasa au kwa vyama vya upinzani tu?

amesema vyama vya upinzani tu; CCM iendelee kuenjoy ruzuku yake ya bilioni 2 na ushee kwa mwezi. So, kina Zitto naona kwa mpango huu mmekwisha! LOL
 
amesema vyama vya upinzani tu; CCM iendelee kuenjoy ruzuku yake ya bilioni 2 na ushee kwa mwezi. So, kina Zitto naona kwa mpango huu mmekwisha! LOL

Ngoja nimsubiri ajibu maana kuna 'gross misunderstanding' kuhusu ruzuku. Wabunge wa CCM (imagine wabunge) wanasema CCM inapenda upinzani ndio maana inatoa ruzuku kwa wapinzani. Eti CCM inatoa ruzuku kwa wapinzani
 
Hakuna kinachonikera mimi katika siasa za bongo kama RUZUKU kwa vyama vya siasa na VITI MAALUM Bungeni. Gharama hizi zingeelekezwa kwenye huduma kwa Watanzania kama vile ELIMU tungepunguza kero nyingi za sasa kama mikopo ya elimu ya juu, madai ya walimu, ujenzi wa madarasa, vitabu vya kiada na ziada,...
 
Unaweza kuwa sahihi katika hoja zako. Ruzuku kwa vyama vya siasa sio Tanzania tu, nchi zote za Ulaya na hata Marekani zinatoa ruzuku kwa vyama na kwa wagombea.

Muhimu kuona je, vyama vya siasa vina nafasi katika uejnzi wa nchi? Je ruzuku inatumika kwa shughuli za kisheria? Tanzania sheria hii ni sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa.

Nini majukumu ya vyama vya siasa? Majukumu hayo yaweza kuendeshwa namna gani? Ruzuku ni muhiimu?
 
Ngoja nimsubiri ajibu maana kuna 'gross misunderstanding' kuhusu ruzuku. Wabunge wa CCM (imagine wabunge) wanasema CCM inapenda upinzani ndio maana inatoa ruzuku kwa wapinzani. Eti CCM inatoa ruzuku kwa wapinzani

Mtoa hoja anatakiwa kubadili kichwa cha habari kabla hatujaenda mbali. Hapa suala la ruzuku si kwa vyama vya upinzani tu. Ila kama kuna chama kinachofaidi ruzuku na kuitumia vibaya toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe ni CCM. Vinginevyo mtoa hoja kutuaminisha kuwa hana hakika na kitu anachoongelea..
 
Unaweza kuwa sahihi katika hoja zako. Ruzuku kwa vyama vya siasa sio Tanzania tu, nchi zote za Ulaya na hata Marekani zinatoa ruzuku kwa vyama na kwa wagombea.

Muhimu kuona je, vyama vya siasa vina nafasi katika uejnzi wa nchi? Je ruzuku inatumika kwa shughuli za kisheria? Tanzania sheria hii ni sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa.

Nini majukumu ya vyama vya siasa? Majukumu hayo yaweza kuendeshwa namna gani? Ruzuku ni muhiimu?
Sina tatizo na hoja zako Zitto.

Ni kweli nchi nyingi duniani zinatoa ruzuku kwa vyama na vikundi vingine vinavyofanya kazi za jamii. Ila inabidi tujiulize, nani alianzisha haya mambo ya ruzuku, viti maalumu n.k hapa TZ? Je tulikaa wadau wote tukakubaliana?? Kwa vile hatukukubaliana, ndo maana tunapata matatizo kibao.

Suala la msingi hapa TZ lingekuwa kukaa chini tutafuta muafaka wa pamoja kwa mambo ya muhimu yanayotuhusu kama Taifa. Lakini kinachoonekana ni CCM kuendelea kutumia NEC kuamua mambo ya msingi yanayowahusu wananchi wote. Hili ndilo kosa kubwa ambalo mzimu wake utaendelea kututesa.
 
Waberoya kwanini iondolewe kwa vyama vya upinzani tu na si vyama vyote vya siasa?

Kwa maoni yangu, ingefaa iondolewe kwa vyama vyote vya siasa, ili pesa hizo zielekezwe katika mambo ya maendeleo na tafiti.

Inashangaza kwamba serikali inamwaga mapesa yote hayo kwa ajili ya siasa badala ya kuyawekeza katika shughuli za maendeleo na tafiti mbali mbali zenye kuleta tija.

Ndo maana tunabaki kulalama kwamba madini yetu yanachukuliwa, kwa vile serikali haitaki kuwekeza katika tafiti na training za kuwa andaa vijana kufanya hizo shughuli wenyewe badala yake pesa zote zinapeleka kwenye siasa ambazo tunaishia kuona zinatengeneza magenge ya mafisadi wanao liangamiza taifa!

Stop wasting our money eti ruzuku!
 
Unaweza kuwa sahihi katika hoja zako. Ruzuku kwa vyama vya siasa sio Tanzania tu, nchi zote za Ulaya na hata Marekani zinatoa ruzuku kwa vyama na kwa wagombea.

Muhimu kuona je, vyama vya siasa vina nafasi katika uejnzi wa nchi? Je ruzuku inatumika kwa shughuli za kisheria? Tanzania sheria hii ni sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa.

Nini majukumu ya vyama vya siasa? Majukumu hayo yaweza kuendeshwa namna gani? Ruzuku ni muhiimu?

Zitto,
Nchi masikini kabisa kama hii tunatoa RUZUKU ili watu wafanye siasa! Makanisa na Misikiti vinajiendeshaje? Kodi tunayokusanya inaweza kuyabeba yote haya? Hivi Bunge kubwa na la MARAHA tulilonalo kwa sasa linahitajika? Kwa nini kila HALMASHAURI/MANISPAA/JIJI isingekuwa na Mbunge mmoja tu? Mchango wako wewe kwa sasa ni sawa na Wabunge wangapi wa CCM?
 
Sina tatizo na hoja zako Zitto.

Ni kweli nchi nyingi duniani zinatoa ruzuku kwa vyama na vikundi vingine vinavyofanya kazi za jamii. Ila inabidi tujiulize, nani alianzisha haya mambo ya ruzuku, viti maalumu n.k hapa TZ? Je tulikaa wadau wote tukakubaliana?? Kwa vile hatukukubaliana, ndo maana tunapata matatizo kibao.

Suala la msingi hapa TZ lingekuwa kukaa chini tutafuta muafaka wa pamoja kwa mambo ya muhimu yanayotuhusu kama Taifa. Lakini kinachoonekana ni CCM kuendelea kutumia NEC kuamua mambo ya msingi yanayowahusu wananchi wote. Hili ndilo kosa kubwa ambalo mzimu wake utaendelea kututesa.
Ruzuku inatolewa kwa mujibu wa sheria, sheria namba 5 ya mwaka 1992. Sheria zote za nchi hupitishwa na Bunge. Hivyo wabunge wa wakati ule walikubaliana. Sheria ilirekebishwa kwa kiasi kikubwa mwaka 1996. Bunge la mwaka 1996 lilikuwa ni Bunge la vyama vingi tofauti na lile la 1992.

Kuwapo kwa viti maalumu Bungeni ni kwa mujibu wa Katiba ambayo hupitishwa na Bunge kwa theluthi mbili ya wabunge wote. Viti maalumu havikuamuliwa na mtu mmoja bali Bunge la Taifa.

Kuna mabadiliko ya katiba yanakuja kuhusiana na suala la viti vya Bunge. Nadhani kuna haja ya majdala kuhusiana na suala la viti maalumu ili tupate mwafaka wa kitaifa.
 
ruzuku iondolewe kwa vyama vyote vya siasa au kwa vyama vya upinzani tu?

amesema vyama vya upinzani tu; ccm iendelee kuenjoy ruzuku yake ya bilioni 2 na ushee kwa mwezi. So, kina zitto naona kwa mpango huu mmekwisha! Lol

ngoja nimsubiri ajibu maana kuna 'gross misunderstanding' kuhusu ruzuku. Wabunge wa ccm (imagine wabunge) wanasema ccm inapenda upinzani ndio maana inatoa ruzuku kwa wapinzani. Eti ccm inatoa ruzuku kwa wapinzani

zito mkjj na wengine naamaanisha kwa vyama vyote , sorry for kutoelezea hilo.ccm nao pia mkumbuke ni wapinzani miaka ijayo!

Ni kwa vyama vyote viwe tawala au la!
 
Mods,can you change title please, sijajua how: tite should read:

.RUZUKU IONDOLEWE KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI.
 
Mh. Zitto, nimeshajibu na kubadili title kama watu walivyoshauri , natamani nisikie kutoka kwako,

MKJJ unasemaje katika hili??
 
Sioni sababu ya msingi ya kuondoa ruzuku kwa vyama vya siasa. Hoja hapa ingekuwa ni uwiano wa mgawanyo wa ruzuku yenyewe na auditing kwa vyama vyote vinavyopokea ruzuku. Kama wengi mnavyotambua, kuna umuhimu wa kuwa na vyama vya upinzani katika nchi. Nadhani climax ya upinzani nchini inaanza kuonekana. Sio lazima kukitoa chama tawala madarakani, lakini kama tunaweza kukiwajibisha kwa kiasi fulani, basi hayo ni mafanikio flani ya kuwa na vyama vya upinzani. Serikali inahaha kwa sasa. Hayo yote ni sababu ya nguvu kidogo tu ya upinzani. Hii ina maana basi, tukigawa ruzuku kwa uwiano wa kura chama ilichopata kitaifa, basi vyama vikubwa vya kisiasa vitapata ruzuku kubwa hivyo kuweza kuikabili serikali na kuiwajibisha.

Kwahiyo la msingi hapa ni kuwepo ukaguzi wa matumizi ya fedha hizi za ruzuku.
 
Hakuna aiyetambua umuhimu wa vyama vya upinzani mpaka sasa, tatizo ni vingapi na vinafanya nini? na wote hawana nia hiyo unayoisema?

naamini kuna vyama hapa hujui wenyeviti wao ni kina nani achili mbali hata kujua kama vipo?

• Chama Cha Mapinduzi (Revolutionary State Party)
• Civic United Front (Chama Cha Wananchi)
• Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
• Tanzania Labour Party
• United Democratic Party
• Chama cha Haki na Usitawi (CHAUSTA)
• Democratic Party (DP)
• Demokrasia Makini (MAKINI)
• Forum for the Restoration of Democracy (FORD)
• Jahazi Asilia
• National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR)
• National League for Democracy (NLD)
• National Reconstruction Alliance (NRA)
• Popular National Party (PONA)
• Sauti ya Umma (SAU)
• Tanzania Democratic Alliance (TADEA)
• Progressive Party of Tanzania-Maendeleo (PPT-Maendeleo)
• Union for Multiparty Democracy (UMD)
• United People's Democratic Party (UPDP)

Ukizungumzia vyama vizuri vya upinzani nadhani unazungumzia CHADEMA TU , NA CUF-visiwani,

CHADEMA TAYARI WANAUZIKA NA KUNUNULIKA! NA SI GHIVYO VINGINE, CHADEMA KINAWEZA KABISA KIKABEBWA NA WANANCHI.

TUTAPUNGUZA POMBE NA SIGFARA TUCHANGE HILI CHAMA KIDUMU, KIENDELEE NA HATIMAYE TUPATE VIONGOZI WAZURI WA BAADAE.

HALI YA SASA mr.Zero mimi na wewe tu7naweza kuanzisha chama chetu cha siasa tukapata hizo hela.

MATOKEO YAKE NDIYO CHAMA CHA PROFESSOR sHAYO KUPATA KURA YA URAIS 1 TABORA!!!! yaani hata wawakilishi wake wenyewe wengine hawakupiga kura!!
 
Nashukuru kwamba unatambua kuna umuhimu wa vyama vingi vya siasa hapa nchini. Hapa hatuongelei vyama vya upinzani na chama tawala, bali vyama vyote vya kisiasa kwa ujumla. Kama kuna umuhimu wa vyama vya siasa, basi lazima tutambue umuhimu wa vyama hivi kupewa ruzuku ili viweze kuikabili na kuiwajibisha serikali iliyoko madarakani. Either itakuwa ni serikali ya CCM au CHADEMA, vyama vingine vya upinzani vitakuwa na jukumu la kuikabili na kuiwajibisha serikali.

Utitiri wa vyama vingi vya kisiasa ni hoja ya msingi pia. Ninachoamini mimi, na wengi pia wanaamini, vyama vingi vidogo vidogo, vimeanzishwa kwa nia nzuri tu ya kuwa na sera na itikadi tofauti na chama kingine. Hii inawapa watanzania fursa ya kuchagua sera na itikadi wanazoona zinafaa kuiongoza nchi hii. Lakini cha msingi hapa ni kwamba, vyama hivi vidogo, itafika stage either vitajiunga na vyama vikubwa au vitakufa kibudu. Hapo ndipo vitabaki vyama vichache vikubwa vyenye nguvu na nia ya kweli ya kuleta mabadiliko hapa nchini.

Hapa ndio hoja yangu ya mgawanyo wa ruzuku kwa uwiano wa kura inaingia. Its obvious kwamba vyama vidogo vitapata kura chache kwenye chaguzi kuu, hivyo kupata ruzuku kidogo sana ya kujiendesha. Hapa either vitakufa au vitajiunga na vyama vikubwa. Vyama vikubwa vitapata kura nyingi hivyo kupata ruzuku kubwa. Hii ina maana upinzani mkubwa kwa serikali iliyoko madarakani.
 
Huku kambi ya upinzani ikiwa imevuna majimbo mengi zaidi katika uchaguzi wa mwaka 2010, na chama tawala kupoteza majimbo mengi na vilevile kura za urais, Hii inamaanisha kuwa kambi ya upinzani itaongezewa ruzuku na chama tawala kupoteza mamilioni ya Shilingi za Ruzuku, Tumefatilia kura za viti maalum na kadhalika, swali langu ni jee mgawo wa Ruzuku kwa vyama vya siasa umekaaje ili kuviwezesha vyama kujijenga na kuwa imara. Ni juzi tuu watanzania wametolewa matongotongo baada ya kuelezwa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni hupewa sh. 100 MIL, Shangingi pamoja na dereva, Nyumba na samani na wafanyakazi wawili, hii ni faraja kwa kambi ya upinzani, Je ruzuku wanafaidika kwa kiwango gani na mahesabu yake yakoje...

Wasalaam

BNN
 
Hapo pekundu ni kwa mwezi,kwa mwaka au kwa siku!tafadhari toa ufafanuzi!!
 
Hizo hela zisitumiwe kuitanua CLUB BILLICANAS na badala yake uletewe wewe?
 
Back
Top Bottom