Rushwa ya ngono kwa walimu vyuoni

Je kuna kesi yoyote ya mwanafunzi kuombwa uroda ambayo iliwahi kufikishwa katika appeal board na haki ikatendeka? Ikizingatiwa mazingira ya kuombana rushwa ya ngono na ugumu wa ushahidi endapo mlalamikaji atalazimika kumshitaki mhadhiri?
Hata ukitajiwa utaijua? Huwa tunasema mahakama zetu hazitendi haki, lakini hii si mara zote. Tumeshuhudia baadhi ya kesi haki ikitendeka. Hivyo basi, hata hizo Appeals Boards zipo zinazoweza kutenda haki. By the way, kama mhadhiri anakutaka, vipi iwe vigumu kuthibitisha? Kwani hakuna mitego inayoweza kuwekwa kunasa watu kama hawa? Hakuna linaloshindikana kama ukidhamiria!
 
Jamani tujitume kwa kuajiajiri hadi watoto zetu wakasome university of alabama, universtiy of mississipi, university of oklahoma, university of cape town, university of manchester maana ufisadi umeshaiharibu nchi hii, kila kitu ngono na rushwa tu, au kama vipi wakapige ivy league university kabisa like yale, havard, princeton, illinois and so on... Huko hakuna but vyuo vyetu vya kata elimu mbovu na bado wanamegwa aaagh
 
Hata ukitajiwa utaijua? Huwa tunasema mahakama zetu hazitendi haki, lakini hii si mara zote. Tumeshuhudia baadhi ya kesi haki ikitendeka. Hivyo basi, hata hizo Appeals Boards zipo zinazoweza kutenda haki. By the way, kama mhadhiri anakutaka, vipi iwe vigumu kuthibitisha? Kwani hakuna mitego inayoweza kuwekwa kunasa watu kama hawa? Hakuna linaloshindikana kama ukidhamiria!

Kama ipo niambie ipo, sio nikitajiwa nitaijua! Na ni mitego ipi inayoweza kutumika kumnasa mhadhiri wa namna hiyo. Naomba unijibu plainly tu, usifanye kama tunabishana vile
 
Nadhani hunielewi ninachozungumza. una sababu gani ya kugawa ngono wakati una uhakika ulifanya vizuri?

Nakuelewa vema FP kwamba huhitaji kugawa ngono wakati una hakika umefanya vizuri. Naomba sasa na mimi unielewe. Swali langu ni kwamba pamoja na uhakika huo wa kuwa umefanya vizuri, ukakuta umefeli, na somo husika ni la mwalimu anayekumendea; je appeal board zinatenda haki?
 
..mtu ana sup 3..anaenda kujilegezalegeza ili apewe maswali.. What d u expect?

Mabint someni..
 
mtu anapo-appeal maana yake anaomba mtihani wake usahihishwe tena, na third marker. kwa maana hiyo, huyo mwalimu huwa hahusiki kabisa kwenye kusahihisha huo mtihani, na mbaya zaidi huwa haambiwi ni mwanafunzi gani ka-appeal, na unapelekwa kwa marker gani. sasa mwanafunzi kama aliandika vizuri huyu 3rd marker atamtoa bila mwl husika kujua
 
..mtu ana sup 3..anaenda kujilegezalegeza ili apewe maswali.. What d u expect?

Mabint someni..
sitaki kuamini kama kweli ukikomaa na kusoma vizuri unaweza kukamatwa kisa tu umemkataa mwl. atakukamata kweli kama umemkataa na somo lake hujafanya vizuri
 
mtu anapo-appeal maana yake anaomba mtihani wake usahihishwe tena, na third marker. kwa maana hiyo, huyo mwalimu huwa hahusiki kabisa kwenye kusahihisha huo mtihani, na mbaya zaidi huwa haambiwi ni mwanafunzi gani ka-appeal, na unapelekwa kwa marker gani. sasa mwanafunzi kama aliandika vizuri huyu 3rd marker atamtoa bila mwl husika kujua

Nisaidie tena, kuappeal ni bure ama unalipia?
 
Duh! college gani huko watu wachukue tahadhari?

Mbona hiyo tabia iko karibu vyuo vyote vya bongo... yeyote aliyepitia vyuo vya juu anajua huo mchezo wa walimu tena usiombe mwalimu ampende girlfriend wako utapata september confrence hadi ushangae...
 
sitaki kuamini kama kweli ukikomaa na kusoma vizuri unaweza kukamatwa kisa tu umemkataa mwl. atakukamata kweli kama umemkataa na somo lake hujafanya vizuri

aisee unaweza kukomaa lakini uwezo ndio hivyo tena kila exam una sup kadhaa. Lakini si busara kugawa uroda hata kama mtu anadhani uwezo wake kitaaluma ni mdogo. Kwa sababu kama uwezo ni mdogo na akaamua kugawa uroda basi ataliwa kwelikweli!!!! Pengine ni bora ku-postpon au kubadili kozi.

Wanabodi mnasemaje kuhusu hili la uwezo mdogo kiakili lakini body inalipa?
 
Kwani ni sababu gani humfanya Mwalimu amtongoze mtu?????

MT na wewe ni mhadhiri nini! Hapa mada sio kutongoza bali kuomba rushwa ya ngono. Ukifikiria kidogo tu zaidi ya pale ulipofikiria awali, utagundua kuna tofauti kati ya kumtongoza mwanafunzi na kumwomba ngono ili usimkamate katika somo lako.
 
Mbona hiyo tabia iko karibu vyuo vyote vya bongo... yeyote aliyepitia vyuo vya juu anajua huo mchezo wa walimu tena usiombe mwalimu ampende girlfriend wako utapata september confrence hadi ushangae...

mwalimu atajuaje uhusiano mahusiano binafsi ya wanafunzi wake?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom