‘Rushwa ya ngono inatumika kupata ubunge’

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
UTAFUTAJI wa vyeo kama ubunge na vingine vya maofisini miongoni mwa wanawake wasiojiamini, ni sababu kubwa ya kuendelea kuwepo kwa rushwa ya ngono nchini.

Aidha, imeelezwa kuwa matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na baadhi ya wanaume ni kichocheo kingine cha rushwa hiyo, inayochangia nchi kuwa na viongozi wasio na uwezo, maadili mema, kwa asilimia kubwa.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi iliyokutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujielimisha kuhusu unyanyasaji wa jinsia nchini, Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) alisema rushwa hiyo ipo na inarindima hata kwa wabunge.

Huku akiungwa mkono na Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CHADEMA), Dk.Gervas Mbassa, Ngoye alisema anachokizungumza kinafanyika si tu katika kuutafuta ubunge, bali hata katika kutafuta vyeo maofisini.

Wakati akisema hayo, Mbunge wa Viti Maalu, Margret Mkanga (CCM) alishtuka kwa mshangao ulioashiria kuisikia habari hiyo kwa mara ya kwaza na ndipo Ngoye alipomwambia, "Usishangae! It is a practical example, akimaanisha kuwa alichokizungumza ni mfano hai uliopo.

Kwa upande wake, Mbassa aliliambia gazeti hili kuwa hali hiyo ipo kweli na kwamba inatokana na kukosa utu miongoni mwa wanaoomba na wanaotoa rushwa ya ngono.

Alisema, wengi wanaojihusisha na rushwa hiyo na kushindwa kupata wanachokitaka huishia kuaibika au kupata maambukizi ya VVU huku walioigawa na kuupata uongozi wakiiharibu nchi kwa njia tofauti kutokana na kukosa maadili ya uongozi pamoja na uwezo wa kazi.

"Alichokisema Ngoye ni sahihi kabisa, rushwa ya ngono ipo hata kwa wabunge. Lakini pia ipo katika nyanja zingine ambazo si za siasa. Watu wanataka uongozi wakati wanajua hawana uwezo na matokeo yake wanaamua kutumia miili yao.

"Ufike wakati Watanzania tuikatae na kuthamini utu vinginevyo nchi itajaa viongozi watakaotusababishia matokeo mabaya," Ndassa alisema.

Wakati huo huo, baadhi ya wabunge wanaounda kamati hiyo wamewataka wanafunzi wanaoombwa rushwa ya ngono kutoa taarifa kwa maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili wahusika wakamatwe na kushitakiwa, kwa sababu kitendo hicho, licha ya kuwa kosa la jinai, kinatumiwa na wengi kusambaza VVU.

Mbunge wa Viti Maalum, Rosweeta Kasikila (CCM) na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), walisema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakitoa michango yao, kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, unaohusisha ngono nchini.

Kasikila ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, alisema kuwa wanafunzi ni waathirika wakubwa wa rushwa ya ngono na kwamba wanahitaji kupewa elimu zaidi juu ya athari za rushwa hiyo ya ngono kwa watu mbalimbali wanaowarubuni ili waikatae na kuwaripoti wanaowashawishi kuishiriki.

"Wapo wasichana na hata wavulana jasiri wanaowaeleza maofisa wa Takukuru kuhusu kuombwa rushwa ya ngono na hivyo kuandaa mitego inayowezesha kunaswa kwa wengi wao na kushitakiwa.

Hiyo ni njia mojawapo inayoweza kusaidia kupunguza kuenea kwa maambukizi ya VVU ambayo wengi wao huyapata wanaposhiriki kujamiiana huko", Kasikila alisema.

Naye Shelukindo alisema kuwa wanafunzi wanastahili kujengewa ujasiri wa kuwaeleza wakubwa wao na taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki zao ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa dhidi yao, kama vile kuhisishwa katika masuala ya kujamiiana kwa kurubuniwa kupata wanachokihitaji.

Alisema, rushwa ya ngono haistahili kuwepo mahali popote pale kwa kuwa ni njia mojawapo inayochochea maambukizi kutokana na ukweli kuwa mara nyingi wahusika wanaoishiriki hawapati muda au kukumbuka


CHANZO: Gazeti la Habari Leo
 
aina hii ya rushwa ni first class.why?
1.mtoa rushwa pia anaenjoy
2.natural
3.inaweza tengeneza familia. i.e rushwa-uchumba-ndoa
 
jamani tunda,nitalipataje tunda.tunda tamutamu,nitalipataje tunda? Nalog off
 
Kama sio kwa hongo hiyo basi jua ni jamaa wa viongozi waandamizi wa chama.
 
Kuna mmoja katoa rushwa ya ngono, akaajiriwa BOT then akapewa umbunge wa viti maalumu kisha mjomba wake akapewa ukuu wa mkoa. Hapo patamu
 
Mara nyingi wanaopata fursa ya kujadili ukimwi wanaishia kujitoa kana kwamba wao hawahusiki na salama na kuona wengine ndio wanao eneza.

Matokeo ni kuenea kwa ukimwi, bora kungelikuwa na kupima kwanza kwa mshiriki ndio watoe michango.
 
makengeza kidogo. hivi viti maalum si anateua mshua, kwa hiyo mshua ndo anafanya yote haya. duh lazima tuongee na rizzler one.
 
Hivi kumbe ni M'mama gani yule ambaye hana Mume nikampe "rushwa" nipate huo ubunge (joking)
 
Mfumo wa upendeleo wa viti maalum vya ubunge kwa wanawake huchochea wanawake wengi kujipendekeza kwa wakubwa na hivyo kutoa hisani ya uroda ili wapendelewe kupata viti vya ubunge.

Idadi kubwa ya wabunge wanawake wa viti maalum ni wenzangu mimi wanaoishi maisha huru bila kufungamana na mwanaume, kwani akina mama walifungamana na waume zao huwa vigumu kugawa uroda wa vibosile. Hii ni hatari kwa demokrasi na haki za msingi kwa wanawake, na matokeo yake tunapata wasiofaa kwenda kutetea ubakwaji wa demokrasi. Bora kufuta kabisa nafasi hizo.
 
.........kwanza hawa wabunge wa vitu maalumu wengi wao mimi huwaona ni watu wa kupiga makofi tu, kupitisha hoja dhaifu
 
Back
Top Bottom