Rushwa na uraia wa Siyoi, CCM watafutana uchawi badala ya kujibu HOJA

naomba kuuliza na mimi uraia wangu..baba alizaliwa Kigali...akaja tanzania 1958..akasoma huku elimu yote hadi chuo kikuu..na akapewa passport ila cjui kaipataje...na mimi nimezaliwa bongo...ila nakuwa kigali na kivu mara nyingi tu...na nina passport ya tanzania..je mimi ni raia wa wapi? na mzazi wangu je?....kuwa na passport ya Tanzania ni kigezo cha kuwa mtanzania?....msaada wenu japo nimeingilia mada
 
Kama una umri wa miaka 18 na zaidi, nakushauri Jumatatu uamkie Uhamiaji. As of this second wewe sio raia wa Tanzania, hiyo passsport haina tofauti na ticket ya basi la Sumry.
 
@Mwigulu,
Kwa uelewa wangu Katiba ya Tanzania inasema kuwa kama mtu amezaliwa nje ya mipaka ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kama wazazi wake hawakuwa nje ya nchi kwa shughuli za kibalozi basi mtu huyo atakuwa na uraia wa Tanzania hadi atapofikisha umri wa miaka 18. Na ili aendelee kuwa raia wa Tanzania mara baada ya kufikia umri wa miaka 18 ni lazima mtu huyo aukane uraia wa huko alikozaliwa. Kwa maana hiyo Sioi alitakiwa aukane uraia wa Kenya. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania na sio katiba ya Kenya au nchi nyingine yoyote.

Hoja yako hapo juu kwamba zipo nchi ukizaliwa unakuwa na uraia (automatically) ina utata kwa sababu moja kuu. Hakuna mahali popote kwenye katiba/sheria za uhamiaji Tanzania inaposema kuwa ili mtu aukane uraia ni lazima awe amepata uraia wa huko alikozaliwa. Ingekuwa ni hivyo basi tungeweza kusema uraia wa Tanzania unatolewa kwa kufuata/ambatana na katiba ya nchi alikozaliwa mhusika! Kinachoangaliwa hapa kwa mujibu wa katiba ni nchi hii ni alikozaliwa mtu huyo regarless amepewa cheti cha kuzaliwa au passport. Na kwa maana hiyo Sioi amezaliwa Kenya, sasa alipofikisha miaka 18 alitakiwa aukane U-kenya wake.

Kesi inayompata Sioi inafanana sana na ile iliyompata Jenerali Ulimwengu. Na wote tunajuwa Jenerali aliomba uraia wa Tanzania. Hapa serikali itapata shida kwa vyovyote vile maana tayari kuna incidents kama hizi huko nyuma na watu walipewa hukumu, sasa kama watapindisha kwa sababu mkasa umemwangukia mtoto wao hilo ni litakuwa jambo jingine, lakini wakae wakijua what goes around comes around. Wametesa sana watu kwa huu mtindo this time around inakula kwao!
FJM,
Hiyo sheria ni kifungu gani? Hakuna kitu kama hicho mkuu.

Sheria ya uraia iko wazi mno ila kwasababu watu wana discuss kisiasa zaidi basi wanashindwa kujichimbia kuelewa maana ya hiyo sheria.

Hakuna tofauti kubwa kwenye sheria juu ya wale waliozaliwa ndani ya nchi na wale wa nje ya nchi.

Wala hata hilo la wafanyakazi wa ubalozi halitajwi kwasababu halikuwa muhimu kwenye hili.

Sheria yenyewe hii hapa: http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/6-1995.pdf

Kesi ya Ulimwengu ilikuwa tofauti maana yeye alizaliwa na wazazi ambao walikuwa na uraia wa nchi nyingine wa kuzaliwa. Laiti mzazi mmoja wa Siyoi angelikuwa Mkenya hapo kungelikuwa na tatizo. Au pia angelizaliwa nchi inayotambua uraia wa kuzaliwa kama USA pia kungelikuwa na matatizo.
 
... Soma katiba ya kenya.
Mkuu, katiba ya Kenya isomwe ili iweje? Tanzania haiongozwi na katiba za nchi nyingine. Daah, kuna kazi kubwa sana ya kuelimisha watu hasa wakati huu wa mchakato wa katiba mpya! Labda tueleweshane kidogo kuwa Immigration huwa wanademand uthibitisho wa uraia wa Tanzania, na si wa nje. Ndio maana Uhamiaji huwa inatoa masaa 24 or so kwa asiye raia anayeishi bila taratibu, kuondoka nchini bila kueleza aende wapi!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Katika hatua za kuikimbia nchi enzi za wazalendo Sokoine, wengi wa vijana wanaoweza kugombea nafasi za uongozi kwa
sasa ambao wazazi wao walikuwa viongozi, wamezaliwa nje ya nchi. Tukianza kufuatiliana tutaumbuka sana baada ya kujua
wale tulio wakabidhi nchi hii katika nyadhifa za serikali wapo ambao sio watanzania. Usipotaka shari usigombee uongozi wa
kisiasa wala hutajulikana. Mimi sipo nimepita tu
 
naomba kuuliza na mimi uraia wangu..baba alizaliwa Kigali...akaja tanzania 1958..akasoma huku elimu yote hadi chuo kikuu..na akapewa passport ila cjui kaipataje...na mimi nimezaliwa bongo...ila nakuwa kigali na kivu mara nyingi tu...na nina passport ya tanzania..je mimi ni raia wa wapi? na mzazi wangu je?....kuwa na passport ya Tanzania ni kigezo cha kuwa mtanzania?....msaada wenu japo nimeingilia mada

Mtu Chake,

Kama babako hakuukana uraia wake wa kigali, hapo wewe una uraia wa nchi mbili kitu ambacho TZ hakiruhusiwi. kwahiyo wewe sio Mtanzania.

Je mama alizaliwa TZ? Kama na yeye yuko kama baba, hapo huenda hata sio Mtanzania kabisa. Inatakiwa uombe uraia wa Tanzania kama wanavyoomba wageni wengine. Lakini kama mama ni Mtanzania basi nenda kaukane huo uraia wa nchi nyingine.

Kuwa na passport ya TZ hakukufanyi wewe uwe Mtanzania.
 
naomba kuuliza na mimi uraia wangu..baba alizaliwa Kigali...akaja tanzania 1958..akasoma huku elimu yote hadi chuo kikuu..na akapewa passport ila cjui kaipataje...na mimi nimezaliwa bongo...ila nakuwa kigali na kivu mara nyingi tu...na nina passport ya tanzania..je mimi ni raia wa wapi? na mzazi wangu je?....kuwa na passport ya Tanzania ni kigezo cha kuwa mtanzania?....msaada wenu japo nimeingilia mada

Mkuu, baada ye mzee wako kuhamia Tanzania, je, aliukana uraia wa Rwanda (alikozaliwa) kabla wewe hujazaliwa? Kama jibu ni ndio, kwa maana kwamba aliukana uraia wa Rwanda KABLA HUJAZALIWA, basi wewe ni raia halali wa Tanzania. Vinginevyo, kama hakuukana uraia huo KABALA HUJAZALIWA na kama una zaidi ya miaka 18, kama alivyokushauri FJM hapo juu mimi pia nakushauri uamkie Uhamiaji, Jumatatu alfajiri ili kuutafuta uraia wa Tanzania.

Vinginevyo hadi muda huu ulitakiwa uwe rumande ukisubiri kupelekwa mahakamani kwa kuishi nchini kinyume cha sheria na mbaya zaidi kwa kughushi nyaraka hadi kupata passport ya Tanzania ambayo automatically imegeuka sawa na karatasi la "chooni".
 
Mwigulu LM Nchemba..................Verified User(teheteheteheehetehte) Kumbe wengine user wa kimachale........poa bana.........mpe hi......Kube.......nadhani meonana hapo Arusha
 
je mama alizaliwa TZ? Kama na yeye yuko kama baba, hapo huenda hata sio Mtanzania kabisa. Inatakiwa uombe uraia wa Tanzania kama wanavyoomba wageni wengine. Lakini kama mama ni Mtanzania basi nenda kaukane huo uraia wa nchi nyingine.

Kuwa na passport ya TZ hakukufanyi wewe uwe Mtanzania.​

mama naye kachanganya uraia tanzania na zambia
 
kama mtu ulikuwa na mazingira ya utata wa uraia kwanini usishughulikie mapema na kunana uraia wa nchi nyingine na ubaki mtanzania mpaka uchaguzi utokee
 
... angelizaliwa nchi inayotambua uraia wa kuzaliwa kama USA pia kungelikuwa na matatizo.

@Mtanzania, hapo kwenye red ndio kwenye mgogoro (spin). Naomba ninukuu baadhi ya sehemu ya majibu toka Idara ya Uhamiaji kwenda kwa RC- Arusha.

"Kifungu cha 7 (1) kinatoa ukomo wa uraia wa mtu aliyepata kwa kurithi kuwa ni miaka 18. Mara baada ya kutimiza umri huo kama mtu huyo kama mtu huyo anataka kuendelea kuwa raia wa Tanzania anapaswa kuukana uraia wa nchi hiyo na kutoa kutoa kiapo cha utii au kututhibitishia kuwa pamoja na kuzaliwa nje ya nchi hana uraia wa nchi hiyo.

Kwa mtazamamo huo basi kama Bw. Sumari alizaliwa kweli nchini Kenya alipotimiza umri wa miaka 18 alihitajika kututhibitishia kuwa kweli yeye sio raia wa Kenya na kutupatia ushahidi wa uraia wa wazazi wake au kuukana uraia wa Kenya na kutuletea cheti (Renunciation certificate) toka Kenya.

Kwa kuwa raia wengi huwa hawatimizi jambo hilo kwa kutojua sheria huwa wale wanaotuthibitishia kuwa wao sio raia wa nchi hiyo wala hawajawahi kupata Uraia wa huko hata baada ya kupita umri tajwa hapo juu maombi yao huwa yanafikiriwa". (mwsisho wa kunukuu).

My take: Kwa maoni yangu Team ya Sioi walipitiwa. Na sasa itabidi wafanye kazi ya ziada kuzika huu mkosi. Wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza kuwaridhisha wakubwa lakini kibarua kitakuwa kwa watu wa Arumeru. Hii publicity kwamba ni Mkenya itakuwa ngumu sana kuifuta kwenye vichwa vya watu wa Arumeru ukizingatia kuwa Sioi hata Kimeru haongei toafauti na Nassari. Very Unfortunate ukizingatia kuwa huyu Sioi bado anaomboleza kifo cha baba yake mzazi.
 
Hapa kweli kuna ngoma nzito, tofauti na nilivyodhani mwanzo. Yaani leo hadi Mwigulu anatoa ushauri kwa CHADEMA !!!
 
mama naye kachanganya uraia tanzania na zambia

Mtu Chake,
Njia rahisi ni kumwambia mama akaukane uraia wa Zambia kwanza. Kisha wewe pia uukane uraia wa Rwanda na hata Zambia.

Uzuri wa kuukana uria ni kwamba hata kama hukuwa nao, unakuwa hujapoteza kitu.

Ukienda kuukana bila mama kuukana wake kwanza bado unaweza kuwa kwenye matatizo. Maana hapo itakuwa mama hakuwa Mtanzania na baba hakuwa Mtanzania kwahiyo na wewe hujawahi kuwa Mtanzania, hivyo inabidi uombe upya.
 
kama mtu ulikuwa na mazingira ya utata wa uraia kwanini usishughulikie mapema na kunana uraia wa nchi nyingine na ubaki mtanzania mpaka uchaguzi utokee

Mkuu wangu jibu liko wazi, sio kila anayejiita mtanzania anaipenda Tanzania kwa dhati! Mijitu mingine ipo kimaslahi zaidi na imekaa kimtego kusikilizia upepo, ukivuma vibaya yanatimua vumbi kuelekea huko ambako "moyo" wao wa dhati upo na kutuachia li-nchi letu. Ukivuma vizuri kwao na opportunity kama hizi kuwajia, mara nyingi bila kutarajia, ndio hapo yanashtuka. Kwa ufupi HAWANA UZALENDO KWA NCHII HII.
 
@Mtanzania, hapo kwenye red ndio kwenye mgogoro (spin). Naomba ninukuu baadhi ya sehemu ya majibu toka Idara ya Uhamiaji kwenda kwa RC- Arusha.

"Kifungu cha 7 (1) kinatoa ukomo wa uraia wa mtu aliyepata kwa kurithi kuwa ni miaka 18. Mara baada ya kutimiza umri huo kama mtu huyo kama mtu huyo anataka kuendelea kuwa raia wa Tanzania anapaswa kuukana uraia wa nchi hiyo na kutoa kutoa kiapo cha utii au kututhibitishia kuwa pamoja na kuzaliwa nje ya nchi hana uraia wa nchi hiyo.

Kwa mtazamamo huo basi kama Bw. Sumari alizaliwa kweli nchini Kenya alipotimiza umri wa miaka 18 alihitajika kututhibitishia kuwa kweli yeye sio raia wa Kenya na kutupatia ushahidi wa uraia wa wazazi wake au kuukana uraia wa Kenya na kutuletea cheti (Renunciation certificate) toka Kenya.

Kwa kuwa raia wengi huwa hawatimizi jambo hilo kwa kutojua sheria huwa wale wanaotuthibitishia kuwa wao sio raia wa nchi hiyo wala hawajawahi kupata Uraia wa huko hata baada ya kupita umri tajwa hapo juu maombi yao huwa yanafikiriwa". (mwsisho wa kunukuu).

My take: Kwa maoni yangu Team ya Sioi walipitiwa. Na sasa itabidi wafanye kazi ya ziada kuzika huu mkosi. Wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza kuwaridhisha wakubwa lakini kibarua kitakuwa kwa watu wa Arumeru. Hii publicity kwamba ni Mkenya itakuwa ngumu sana kuifuta kwenye vichwa vya watu wa Arumeru ukizingatia kuwa Sioi hata Kimeru haongei toafauti na Nassari. Very Unfortunate ukizingatia kuwa huyu Sioi bado anaomboleza kifo cha baba yake mzazi.

FJM,
Hayo maelezo ya mtu wa uhamiaji ni guidelines tu walizopewa kama nilivyofafanua kwenye post nyingine.

Wewe soma tena hiyo 7(1) na niambie kiwazi wazi wapi wameandika alichosema huyo mtu wa uhamiaji?

Kwa watu wengi hiyo tafsiri ya jamaa wa uhamiaji inafanya kazi. Lakini bado yenye nguvu ni act yenyewe na wala sio guidelines za idara ya uhamiaji.
 
Mtu Chake,
Njia rahisi ni kumwambia mama akaukane uraia wa Zambia kwanza. Kisha wewe pia uukane uraia wa Rwanda na hata Zambia.

Uzuri wa kuukana uria ni kwamba hata kama hukuwa nao, unakuwa hujapoteza kitu.

Ukienda kuukana bila mama kuukana wake kwanza bado unaweza kuwa kwenye matatizo. Maana hapo itakuwa mama hakuwa Mtanzania na baba hakuwa Mtanzania kwahiyo na wewe hujawahi kuwa Mtanzania, hivyo inabidi uombe upya.

Mkuu wangu hapo kwenye red sidhani kama ni sahihi sana. Kila mtu atawajibika kwa matendo yake mwenyewe. Ikitokea kwa mfano mama yuko kaburini na hakuwahi kuukana uraia wake wa awali? Je, mimi nitafungwa kwa hilo? Cha msingi yeye kama yeye maadam amefikisha umri unaotakiwa kisheria aukane uraia wa wazazi wake bila kujali wao waliukana au la!
 
NAGALIZO:-
Unapokuwa na uraia/passport ya nchi nyingine pamoja na Tanzania ni kwamba unakuwa umekosa sifa za kuwa raia wa Tanzania [yaani automatically wewe si raia wa Tanzania] ndiyo sababu wanasiasa wanaendesha kampeni ya chinichini ili hicho kipengele kifuatwa ibaki kwamba unapopatikana na uraia zaidi ya ule wa Tanzania basi uchague kati ya mambo matatu; 1. ukane uraia wa Tanzania, 2. ukane uraia wa nje na 3. utwae uraia wa nchi mbili!

Mkuu inasikitisha sana kuona kuwa watu wengi sana wana uraia wenye utata, lakini serikali iko kimya tu. Utata wa urais wao unaonekana pale wanapokuja kugombea nafasi za uongozi. Kama ni kweli mgombea ana pasi mbili za kusafiria, anakuwa amevunja sheria za nchi, na anatakiwa kuchukuliwa hatua, na kama ana uraia wa nchi mbili moja ikiwa ni Tanzania pia anatakiwa kuchukuliwa hatua, na kama ni mgeni inatakiwa ithibitishwe kuwa amelipia hati zake zote za ukazi na kuwa taratibu zote zinazohusiana na uhamiaji zimefuatwa.

Inaonesha kuwa kuna udhaifu mkubwa sana Uhamiaji. Ni Jambo la aibu kama kweli IGP amekwenda USA RIVER kwa sababu ya utata wam uraia wa mtu mmoja anayeeonekana kuwa mgombea wa CCM, wakati Dar es salaam makao makuu kuna mamia ya mambo muhimu yanayitakiwa kushughulikiwa. Still inaonekana hata ndani ya jeshi letu la Polisi usalama wa raia uko chini ya maslahi ya CCM.
 
Mkuu wangu hapo kwenye red sidhani kama ni sahihi sana. Kila mtu atawajibika kwa matendo yake mwenyewe. Ikitokea kwa mfano mama yuko kaburini na hakuwahi kuukana uraia wake wa awali? Je, mimi nitafungwa kwa hilo? Cha msingi yeye kama yeye maadam amefikisha umri unaotakiwa kisheria aukane uraia wa wazazi wake bila kujali wao waliukana au la!

Hapo sikuwa na maana ya kwamba utakuwa kwenye matatizo ya kufungwa. Nilikuwa na maana huyo mtu atakuwa sio Mtanzania hivyo lazima aombe Utanzania upya kama walivyofanya akina Ulimwengu.

Ili yeye aliyezaliwa TZ awe Mtanzania ni lazima mzazi wake mmoja awe Mtanzania wakati yeye anazaliwa. Sasa hapo kama mama hajaukana wa kwake kwanza ina maana wote baba na mama sio watanzania na hivyo na mtoto naye sio Mtanzania. Inatakiwa aombe uraia upya kama wanavyoomba wageni.

Kama mama amefariki bila kuukana uraia ule mwingine basi huyu ndugu yetu lazima aombe uraia upya. Option ya kuukana ule mwingine inakuwa haipo maana yeye anakuwa sio Mtanzania. Hiyo ndiyo ilikuwa argument yangu.
 
FJM,
Hiyo sheria ni kifungu gani? Hakuna kitu kama hicho mkuu.

Sheria ya uraia iko wazi mno ila kwasababu watu wana discuss kisiasa zaidi basi wanashindwa kujichimbia kuelewa maana ya hiyo sheria.

Hakuna tofauti kubwa kwenye sheria juu ya wale waliozaliwa ndani ya nchi na wale wa nje ya nchi.

Wala hata hilo la wafanyakazi wa ubalozi halitajwi kwasababu halikuwa muhimu kwenye hili.

Sheria yenyewe hii hapa: http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/6-1995.pdf

Kesi ya Ulimwengu ilikuwa tofauti maana yeye alizaliwa na wazazi ambao walikuwa na uraia wa nchi nyingine wa kuzaliwa. Laiti mzazi mmoja wa Siyoi angelikuwa Mkenya hapo kungelikuwa na tatizo. Au pia angelizaliwa nchi inayotambua uraia wa kuzaliwa kama USA pia kungelikuwa na matatizo.

Kwa maana hiyo Bw. Uhamiaji kapitiwa?
 
NAGALIZO:-
Unapokuwa na uraia/passport ya nchi nyingine pamoja na Tanzania ni kwamba unakuwa umekosa sifa za kuwa raia wa Tanzania [yaani automatically wewe si raia wa Tanzania] ndiyo sababu wanasiasa wanaendesha kampeni ya chinichini ili hicho kipengele kifuatwa ibaki kwamba unapopatikana na uraia zaidi ya ule wa Tanzania basi uchague kati ya mambo matatu; 1. ukane uraia wa Tanzania, 2. ukane uraia wa nje na 3. utwae uraia wa nchi mbili!

Nadhani walioweka kifungu cha Kikatiba/sheria kuhusiana na hapo kwenye red walikuwa na nia njema sana na nchi yetu - UZALENDO KWA TAIFA. Walaaniwe wanaotaka kutuletea kitu inaitwa "dual citizenship (uraia wa nchi mbili)".
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom