Rushwa na faini za trafic barabarani

evaluator

Senior Member
Feb 15, 2011
181
50
Imekua nijambo la kawaida kwa traffic wetu kuchukua rushwa au kukuandikia kulipa faini papo kwa papo,pia pesa hizo tunazolipa hazifiki hata kwenye vituo vyao acha serikarini. ushauri:nashauri serikali ifungue account bank zote kwaajiri ya watu kulipa faini uko badala ya kumpa traffic mkononi.pia iandae utaratibu ambao mtu akikutwa na kosa sio lazima alipe faini papo hapo,apewe muda angalau wa siku saba awe ameshalipa kwenye hiyo account na apeleke risiti kituo chochote cha polisi coz hakupita barabarani kuja fanya kosa.kwa kua kwasasa leseni ziko recorded kwenye mtandao,system zifungwe kila kituo ambapo na traffic akikuandikia faini anachukua licence no ya hiyo leseni yako then anaimark hilo kosa kwenye system na faini yake aliyokuandikia then ww ukishalipa unapeleka risiti kituo chochote wakicheq leseni yako wanaingia kwenye mtandao na kureset ile mark bila yule polisi kuusika.great thinkers hii mnaionaje?
 
wazo zuri na lita punguza,rushwa na usumbufu.
Ni kweli wazo ni lakini kwa watanzania huo ni utaratibu mrefu hivyo ni vigumu kutekelezwa hasa ukuzingatia trafic wenyewe hawataki hela nyingi buku mbili mpaka tano.
 
Tanzania rushwa inawezekana kuisha kuna malipo kwa njia ya electronics ukukamatwa bora ulipe kwa njia hiyo ziwekwe hizo njia mambo ya kuandikisha makaratasi yamepitwa na wakati umesikia kamanda wa POLISI SHULE IPO
 
Hili nalo tatizo na leo nmeshuhudia traffic wakimtoza konda elfu 30'akn hapo hapo hakuna sehemu ambayo ameweka saini ya kile alichokichukua,kwa hyo kuna uhuni unafanywa na hawa polisi fedha na hapo hapo nmeshuhudia traffic wakimbambikiza abiria kesi kisa tu ati amehoji uhalali wa lile tozo then kakwida juu akarushwa juu ya gari lao kwa hyo ni unyanyasaji wa wazi kabisa
 
Usinitie machungu ni muda huu tu Trafic kanisimamisha amenikuta ninakosa la kutofunga mkanda, nimemwambia najua Notification ni Elfu 20000 twende kituoni nikawalipe kwa Check kwakua sina cash yakutosha sanasana nina Elfu 5000 tu akaniambia hawapokei Hundi wanapokea Cash tu, nikamwambia sasa basi ngoja niende bank akasema usinipotezee muda we niachie hiyo Elfu 5000! Basi nikawa sina jinsi nikamuachia.
 
..Kifungu cha 15 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa kinasema Mtoaji na Mpokeaji Rushwa wote mnatenda kosa. Kifupi wewe ni Mtuhumiwa unaetakiwa ukasimame kizimbani.
 
Trafiki trafiki trafiki.....
wana laana hawa jamaa, hawakawii kukuzushia leseni yako feki, na kupisha ufunguzi wanakuweka ndani kwenye sero zao
 
..Kifungu cha 15 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa kinasema Mtoaji na Mpokeaji Rushwa wote mnatenda kosa. Kifupi wewe ni Mtuhumiwa unaetakiwa ukasimame kizimbani.
Akasimame Kizimbani baba yako! Yaani nimekubali kosa na ninataka kwenda kukulipa halafu unaniambia hampokei Check??
 
Usinitie machungu ni muda huu tu Trafic kanisimamisha amenikuta ninakosa la kutofunga mkanda, nimemwambia najua Notification ni Elfu 20000 twende kituoni nikawalipe kwa Check kwakua sina cash yakutosha sanasana nina Elfu 5000 tu akaniambia hawapokei Hundi wanapokea Cash tu, nikamwambia sasa basi ngoja niende bank akasema usinipotezee muda we niachie hiyo Elfu 5000! Basi nikawa sina jinsi nikamuachia.
Ndugu Ndallo,hyo ndio njaa ya matraffic wa hapa kwetu
 
Kha! Mkuu hapo utainyima serikali mapato kabisa, hutapelekwa polisi labda watu wenyewe wakubali kulipa Faini badala ya kutoa Nusu ya fine.
 
Trafiki trafiki trafiki.....
wana laana hawa jamaa, hawakawii kukuzushia leseni yako feki, na kupisha ufunguzi wanakuweka ndani kwenye sero zao
Samahani lakini kusema kuwa "nawachukia polisi wote, na sitakuwa na urafiki na polisi" ni wanafiki,waongo,wauaji,Wezi,wapokea rushwa nk
 
Imekua nijambo la kawaida kwa traffic wetu kuchukua rushwa au kukuandikia kulipa faini papo kwa papo,pia pesa hizo tunazolipa hazifiki hata kwenye vituo vyao acha serikarini. ushauri:nashauri serikali ifungue account bank zote kwaajiri ya watu kulipa faini uko badala ya kumpa traffic mkononi.pia iandae utaratibu ambao mtu akikutwa na kosa sio lazima alipe faini papo hapo,apewe muda angalau wa siku saba awe ameshalipa kwenye hiyo account na apeleke risiti kituo chochote cha polisi coz hakupita barabarani kuja fanya kosa.kwa kua kwasasa leseni ziko recorded kwenye mtandao,system zifungwe kila kituo ambapo na traffic akikuandikia faini anachukua licence no ya hiyo leseni yako then anaimark hilo kosa kwenye system na faini yake aliyokuandikia then ww ukishalipa unapeleka risiti kituo chochote wakicheq leseni yako wanaingia kwenye mtandao na kureset ile mark bila yule polisi kuusika.great thinkers hii mnaionaje?

Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !
 
Ukwel fine ikishaandikwa ni lazima ilipwe la sivyo ufikishwe mahakamani,na fine ni elf30 saiz imepitishwa na wabunge wetu,na fine ya sumatra inaanzia laki,madereva ndio wanalazmisha kutoa hela kutokana na makosa yao ndo mana walimlaani jerry muro kwa kuwapga pcha trafk wao,dereva hajakaguliwa konda anakimbilia kwa trafk nakutoa hela,muogopeni mungu polic maisha yao magumu sana msiwaone vle mnapiga kelele na bukubuku mawazr wanaiba mabilion wakipita mnawapigia makofi na kuwatoa watoto madarasan waje kmshangilia,watanzania amken tutende hak panapo stail madokta wamegoma hamna vfaa mafao duni mnataka mponda hajiuzuru,umeme hamna mbona wafanyakaz wa tanesco hawagomi kushnikiza ngeleja hajiuzuru?je mbona wabunge hawakugoma kushnikiza posho nakushnikiza spka ajiuzuru,mmepinga nauli za kvuko nakutaka maguful ajiuzuru vp kupanda bei umeme?ngeleja bado yupo tu!
 
Mtoa maada haongera kwa kutoa wazo zuri,hata hivyo pengine tungehitaji ushaidi kuthibitisha kuwa;

  1. unapolipa faini na kupewa risti, pesa hafiki vituoni.
  2. Kwenye hiyo akaunti unayosema, watakao husika na uchukuaji wa hiyo pesa na waadilifu kupita hao Trafiki
  3. wewe si miongoni mwa wanaoshawishi kutoa rushwa mara ukamatwapo
  4. Ni mara ngapi umekamatwa ukiwa na makosa,ukadaiwa rushwa na ukakataa kutoa kisha ukapelekwa vituo vya polisi/trafic kwa taratibu za kisheria?
Pia katika maelezo yako unadai kuwa huwa hautegemei kutenda makosa barabarani,Je chombo chako cha usafiri
hukaguliwa mara ngapi na nani?Maana unapoa tembea barabarani mapungufu ya chombo chako ww ndo unayajua,ukiachilia mbali makosa ya kutofuata sheria za barabarani.

Tupunguze lawama jamani, na tuwe na miyo ya shukurani maana kwa kiasi kikubwa askari wetu wanafanya kazi kubwa mno,nagalia mfano wanaoongoza magari katika jiji la Dar na kwingineko hata wanaolinda mali na maisha yetu.Unataka wafanye lipi ndiyo uwapongeze au wasitekeleze wajibu wao?Mimi kwa utafiti wangu nimeshuhudia askari asiyetimiza wajibu wake ndiye husemwa vizuri na watu wengi na hiii ni kwa sababu watu wengi huishi kwa kuvunja sheria.

Je, kwa mwenendo huo tutafika?
 
Back
Top Bottom