Rushwa kwenye suala la ajira

Don 1

Member
Apr 7, 2016
8
1
Habari zenu waungwana,

kama kichwa cha habari tajwa hapo juu mnalizungumziaje hili swara la rushwa katika ajira,

maana inasemekana kwa Dada zetu huhitajika kutoa rushwa ya ngono na kwa vijana wa kiume huhitajika kutoa cent na inategemea utaambiwa utoe kiasi gani.

Kiukweli kama hili ni kweli ni tatizo kubwa saana ktk hili Taifa letu.., maana unaweza ukatoa hiyo rushwa na bado usiipate hiyo kazi., kinachotakiwa ni kujiamin na kumtanguliza Mungu katika mahitaji yako yote katika maisha yako maana inauma sana umejichanga ukatoa cent/umemvulia nguo jamaa halafu mwisho wa siku chenga kazi hakuna..,

kwa nin huyo mchukua rushwa usimuwinde na kumfanyia kitu mbaya.., maana laana haitoki kwa wazazi tu hata binadam wenzako wanaweza kukulaani.

Maisha ni Magum sana maana kuna wengine wanatoka familia masikin kabisaaaa kijana kajitahidi kusoma mpaka kamaliza chuo, anaingia sokoni kazi hakuna anaitwa kwenye interview anaombwa rushwa, familia inajichanga inampatia kijana wao akatoe mwisho wa siku kazi hakuna, wazazi wanaanza kumaliza imani juu ya kijana wao, huu huwa ni mwanzo wa binadam kubadilika na kuwa na roho mbaya, katiri yote hayo hutokana na maswahibu aliyokutana nayo.

Mi nawashauri vijana wenzangu unapomaliza chuo, mwaka wa kwanza ukapita kazi hakuna..,

mwaka wa pili kazi hakuna anza kubadilisha dira kuelekea Plan B yaani kujiajili maana Plan A kwa walio wengi huwa ni kuajiliwa, tafuta hata mtaji wa laki tatu/tano anza nao maana ndani ya miaka miwili siyo laki tano tena na utajikuta unaanza kufurahia maisha...,

Ahsanten na jitumeni kufanya kazi na msikate tamaa maana kukata tamaa ni DHAMBI.
 
Kuna mwanafunzi namfahamu wa kike alikuwa anatembea na mwalimu wake ati amemuahidi akimaliza atamtafutia tempo/ajira, alipomaliza tu na mahusiano na yule ticha yakaishia hapo ticha kampiga chini.
 
Kuna mwanafunzi namfahamu wa kike alikuwa anatembea na mwalimu wake ati amemuahidi akimaliza atamtafutia tempo/ajira, alipomaliza tu na mahusiano na yule ticha yakaishia hapo ticha kampiga chini.
Bila shaka ticha akadandia mwingine, aaaah acha waliwe tu wanaringa sana wakiwa wanatembea na "wakubwa" hawa viumbe.
 
Bila shaka ticha akadandia mwingine, aaaah acha waliwe tu wanaringa sana wakiwa wanatembea na "wakubwa" hawa viumbe.
Ngono imekua cheap sana na baadhi ya wasichana huitumia kama tool yakuwafanikishia mambo flani flani.
 
Na mabinti kwenye kutafunwa hawaishii hapo tu, walimu wa kike hasa waliopangwa mikoani na vijijini wasipopapenda wengi wao wamekuwa wakitafunwa sana na maafsa wa serikali ili tu wapate kuhamishwa vituo vyao vya kazi.
Ni % ndogo sana ya walimu wa kike huhama pasipo kuhusisha mili yao...
 
Ukiona mwajiri anakuomba rushwa mwanafunzi uliyemaliza chuo unatafuta ajira kujikwamua na ukali wa maisha baada ya msoto mkali wa boom, ujue hiyo ofisi, au kazi uliyoomba haina maslahi, ni njaa tupu. Haiwezekan HR au afisa mwajiri aliyeridhika na kazi yake aka risk kwa rushwa ya mtu unayetafuta ajira. Unajua kutafuta kazi ktk entry level ni indicator pia ya umaskin, labda kama ni sehemu kubwa au potential, au nafasi ya Udirector. Rushwa ya ngono iko kimatamanio zaid kuliko kucreate wealth, hiv mwanachuo anakupa laki mbili au tano halafu baadae mnakuwa mnaongeaje sasa? sipati picha.
 
Back
Top Bottom