RUSHWA bungeni na Nchini: Tumeyataka wenyewe.

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,856
13,139
Kwa kweli mimi sishangai sana na habari za rushwa kupiga hodi Bungeni kwa kishindo.
Kwa miaka kadhaa tena ni Bunge hilihili liliibua rushwa kubwa kubwa kama ya RICHMOND,EPA, KAGODA, RADAR,MEREMETA na hata scandals za pesa nyingi kupitia Import Support progammes za wafadhili.

Iliyochunguzwa na kuchukuliwa hatua nusu nusu ni ile ya Richmond tu, na mpaka leo watuhumiwa wakuu wanaendelea kupeta katika siasa badala ya kuwa jela.

Rushwa siku hizi ni rafiki ya mfuko, iwe Polisi, mahakamani na sehemu nyingi tu za kutolea haki.Usipokuwa na fedha za kujinasua katika matatizo ole wako!

Hii rushwa kubwa kubwa ya fedha za kiwango cha mabilioni na matrilioni imeendelea kuvumiliwa kwa vile "hakuna ushahidi".

Kwa hali hii Mbunge mwenye damu nyekudu, anayeishi tTanzania tutegemee nini?

IF YOU CANT BEAT THEM,JOIN THEM!!!!

Tumecheka na nyani sasa tunakula mabua, na tumefunika kombe, wanaharamu wa rushwa hawataki kuondoka.

Wala rushwa tumewalea wenyewe na mimi sioni ni kwa vipi leo ushahidi wa rushwa ya wabunge wetu wapenzi utapatikana.

Wasalaam!
 
MKuu tatizo letu watanzania ni kuwa tumekuwa tukiyasikia na kuyaacha yapite.ila tunatakiwa kufanya maamuzi magumu kwa kuandamana hadi tuondoe huu mfumo kandamizi
 
Back
Top Bottom