Rushwa Bungeni: Kamati ya bunge ya Nishati na Madini yavunjwa

mtakumbuka jinsi bunge hili lililo chini ya Spika Anna Makinda lilivyoanza kwa kasi kwa kamati zake hususan Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa chini ya Mhe January Makamba kuiingilia kuiingilia Wizara ya Nishati na Madini na manejimeneti ya Tanesco mara kwa mara hadi kufikia hatua ya Kamati hii kuonekana ndio inaiendesha Tanesco hivyo madudu yote yaliyotokea Tanesco enzi za kamati hii yanamhusu moja kwa moja Mhe January Makamba hivyo naye atakiwe kujiuzulu
 
Zitto hayuko kamati ya nishati na Madini jamani aliyekuwa ni January Makamba naye kisha acha nafasi hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Naibu waziri.. Nafikri mwenyekiti wake anaitwa kitu kama - Selemani..
Watu mnataka tu kumwona Zitto akipigwa chini Miafrika bana duh!

Mkandara, haya madudu ya TANESCO yamefanyika muda mrefu. Huyu mwenyekiti wa sasa na muda mfupi sana kwenye hicho kiti, na haya madudu kayakuta. Jambo la kujiuliza hasa wale wanaoleta siasa za 'ujana', January Makamba aliona haya madudu wakati akiwa mwenyekiti wa kamati? 'Ujana' wa January ulifanya nini kuhusu hili shirika?
 
mkuu kamati ya mashirika ya umma na yenyewe ni miongon mwa kamati zinazohujumu tanesco n andio maana kama ulimsikia zitto alaitetea sana swala la umeme kukatika tz nzima kwa kigezo kwamba tanesco iliingiliwa katika matumizi ya fedha zake na serikali lakn kumbe hali haikauwa hivyo ni kwamba wao walitakiwa kwenda kuchukua mafuta kwa PUMA na hata hivyo waziri prof alisafiri toka dom kwa gari hadi dar na bado mafuta hayakuwa yamenunuliwa na ndipo aliposhukia tanesco na mafuta yakapatikana tena kwa mali kauli kutoka kwa hawa PUMA so zitto kama ndo muuza tairi ama muuza nguzo anajijua mwenyewe. ila anahusika sana tu
Sasa hapa ndipo napokwambia wewe ndio hujui kinacho elendelea. Unashindwa kuona nje ya changa walokumwagia usoni. Kwa nini Tanesco inunue mafuta PUMA iwe ndio hoja? kwa sababu ni Cheap? au ukweli ni kwamba ni rahisi kwa bei kati yake na kampuni nyinginezo mlopewa kuziona?.. Wewe unaweza kwenda kununua mafuta kwa gari lako cheap kuliko hata bei ya PUMA ambao wanawauzia Tanesco in Bulk wakati hawalipi kodi - Why?..
Halafu PUMA ni kampuni ya nani haswa? Sio BP shell kama watu wanavyodai isipokuwa ni kampuni ilonunua mali za BP kabla hawajaondoka nchini..Halafu sii kweli kwamba ati serikali yetu ina own 50% naomba mtu anipe ushahidi huo maana kampuni hii iko nchi 30 duniani na wana refine mafuta na kusafirisha. Na jiulize kwa nini leo iwe PUMA muhimu saana baada ya kuua shirika letu wenyewe TIPPER ambalo lingefanya kazi hii hii pasipo sisi kutumia mashirka ya nje - Hutalipata jibu..

BP haiwezi kabisa kuachana na nguvu ya jina lake na kujiita PUMA - ili iweje?. Ukweli ni upi basi... Kuna mtu kisha kula 10% toka Puma ambao pengine walinunua mali za BP kabla shirika hilo halija ondoka nchini mnadani (liquidation) pengine kuikolimba na TIPPER.. (naongezea tu).. Sisi Midanganyika ndio kwanza tumeona tuna save bil 3 kwa week kumbe hatukutakiwa kununua hata kwa Tsh 1000 kwa sababu mafuta siku zote bei huwa kubwa kutokana na kulipia Tax kubwa. Kama shirika halilipi tax mafuta unaweza kuyanunua chini ya nusu ya bei unayoona ktk metre pale Petrol station. Puma ni wezi kama wezi wengineo tu.

Hapa kuna mchezo Sis, viongozi wetu wenye hisa huko ama wanakula 10% Puma walipoona mafuta hayanunuliwi toka shirika hili ndipo vita ikaanza. Kina Ngeleja walikuwa wakipiga bao wakati wao kama huyu anayetaka mafuta ya Puma yanunuliwe ingawa ni kinyume cha kanuni lakini naye apige bao. Swala hapa wanachopigania ni tender tu na ulaji kama wewe unavyotafuta tender ku supply ndizi jeshini ukisukumana na kina Mkandara. Ukipata hata iwe kwa faida ya Tsh moja lakini kutokana na idadi kubwa ya wanajeshi wote utajikuta unatengeneza mamillioni.

Tanesco haina sababu kabisa ya kununua Mafuta kwa ajili ya shirika lolote isipokuwa mitambo yake tu. Na Tanesco inatakiwa ipewe fedha za kununua mitambo yake, kuendesha mitambo yake na sio kulipa madeni ya supplier wa mafuta kwa mashirika ambayo udharura wake ulikwisha toka 2008. Hivi unafikiri reli haijengwi kwa sababu hatuna fedha? Hivi unafikri ATC inagota kuendelea kwa sababu hatuna uwezo?.. Barricks, na madini mengineyo unafikiri kote hukuo hatuna uwezo wa sisi kujitegemea. Please mnaamini sana hawa wanasiasa wakati ukweli upo machoni mwenu. Kuishi mujini darasa jingine jamani..
 
Hili limetangazwa na spika wa bunge hivi punde, Na ni kutokana na baadhi ya wajumbe kuhusishwa na Kudai rushwa.

Hizi dili zote zilitengenezwa na January Makamba wakati akiwa Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini na alipotoka ikabiidi rafiki yake Zitto abebeshwe zigo la kumtetea Mhando wa tanesco kwa kuwa walijua alichokuwa akikifanya.
 
hahusiki kabisa
January Makamba anahusika kwa kuwa yeye ndio aliasisi utaratibu wa kuiingilia Wizara ya Madini na Nishati iliyokuwa chini ya Mhe Wiliama Ngeleja pamoja na menejimenti ya Tanesco na madudu haya yamefanyika wakati wa kipindi chake. Ikizingatiwa kuwa Mhando ni homeboy wa Makamba ililazimika Zitto ambaye ni rafiki yake January Makamba kimaslahi kubebeshwa zigo la kumtetea Mhando blindly. kama kweli Bunge limataka kujisafisha ni lazima uchunguzi huo umhusishe Janaury Makamba. Inafahamika kuwa wote wawili walikuwa katika mradi wa kutafuta fedha kwa ajili ya harakati za kugombea urais katika vyama vyao
 
Rekebisha title basi ionekane kuwa ni maoni yako tu sio kwamba amejiuzulu
 
Tumeona uzalendo wake [anaodai kuwanao] katka wizara ya nishati na madini................!

Kibanga Msese
 
Akina zitto imekula kwao... No more kupewa hongo na tanesco na wezi wengine.. Safi sana japokua u wonder ingekua kamati iko chini ya kigogo wa ccm sidhani kama wangeivunja

Mkuu soma posts zilizotangulia. ZZK sio mwenyekiti wala mjumbe wa kamati ya nishati. Ya kwake ni POAC (mashirika ya umma), ambayo kikanuni ni oversight, na lazima mwenyekiti wake atoke opposition
 
Shukrani nyingi kwa mwenyekiti wa CCM na Mh Raisi kwa kumteua huyo waziri wa nishati na madini. Tunataka mawaziri watano tu kama huyu basi heshima ya CCM itarudi kileleni. Ila tunaomba umlinde kwani genge la wahuni (mafisi) watapanga njama za kummaliza.
 
Back
Top Bottom