Rushwa Bungeni: Kamati ya bunge ya Nishati na Madini yavunjwa

yapo hapo ndipo palipo niacha hoi hivi fred na veronica ndio wanafanya tukose umeme? Yani watu watatu ni zaidi ya watu million 40 kweli.
Hivi zitto alikuwa ana tetea nini?

ngoja nikwambie kitu kaka mkubwa rutta, Zitto kama mwenyekiti wa kamati sijui ya mashirika ya umma kama skosei ni miongoni mwa zile kamati ambazo zinztajwa kuhusika katika hili sakata la kuhujumu tanesco. na ndio maana nakwambia kabisa zitto alikuwa na haki ya kuitetea hii manake alijua jumba litamdondokea tu.

sijui kama mnyika ni memba wa hii kamati ila nijuavyo huyu suleiman zedi yeye ni mbuzi wa kafara tu manake haya aliyafanya jan makamba tukubali tukatae manake hata tenda nyingi kama ni za mwaka jana ni dhahiri huyu hausiki. natamani kila mtu angetanjwa na huyua Mhando na mkewe Vero na mwanae Alfred wawe sued kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Picha+na+2.JPG
 
Mh. Mnyika nae ni mjumbe wa hiyo kamati Scofied wewe unaamini kuwa kwa ile hotuba ya upinzani ilivyowakandia Tanesco amepokea rushwa? Mimi nadhani kamati ya hesabu za mashirika ya umma ndiyo iliyokuwa inamtetea Mhando na siyo kamati ya nishati.

Hahahaa jamani mapenzi na chuki binafsi ni kitu hatari! Yani kwa ajili Mnyika ni mjumbe wa kamati ya Nishati iliyovunjwa, sasa unataka ivunjwe ya hesabu ya mashirika ya umma ili iwe Zitto na sio Mnyika. Hahahaa
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti wa hii kamati ni Seleman Zedi, miongoni mwa wajumbe wa hii kamati ni Sara Msafiri (mbunge Viti maalum UVCCM) Munde Tambwe (viti maalum CCM), Chirstopher ole Sendeka, John Mnyika (CDM). Hii kamati ilikuwa inaongozwa na Naibu waziri wa sayansi na Technolojia Januari Makamba kabla ya reshufle ndogo iliyofanywa na JK Mwanzoni mwa mwezi June

Selemani Zeddy atawajibika kisiasa kwa sababu yeye ndie Mwenyekiti wa hii kamati, Wanaodaiwa kuivuruga TANESCO ni Zitto Kabwe na January Makamba, wakishirikiana na Munde Tambwe na Sara Msafiri. Sina nia ya Kumsafisha Zeddy but jamaa ni Clean, namfahamu since akiwa ZAIN. Haya madudu aliyoyasema Prof. Mulongo yalifanyika January Makamba akiwa ni Mwenyekiti.

Munde ni fisadi mkubwa aliwahi kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na Manispaa ya Tabora kwa ubadhirifu wa Shs 987,214,000/= akiwa ni karani idara ya uhasibu manispaa ya Tabora.

Nashauri ni vizuri kamati ya uongozi ya bunge uwe unawafanyia wajumbe wa kamati vetting kabla ya uteuzi
Mkuu kuna ukweli mkubwa sana ktk uloyazuungumza isipokuwa sii kweli Zitto na Makamba ndio wanaivuruga Tanesco hapana. Kuna nguvu kubwa sana nyuma ya viongozi wetu ambao ndio mdudu ndani ya kokwa la Tanesco sio Zitto wala Makamba..

Yawezekana Zitto na Makamba wana vita kubwa na Ngereja au sasa Wizara ya Nishati na Madini kwenyewe na sii Tanesco. Malengo yao kwa undani wake siyajui lakini nachoelewa sasa hivi roho ya uchumi wa Tz ni Wizara ya madini na Nishati na kwa yeyote atakaye control wizara hii ndiye atakuwa na nguvu ya Utawala..

Lakini pamoja na yote haya vita zote hizi ni kutafuta Ulaji tu maana watu wote wanakwepa ukweli kwamba kuna mdudu kaingia ndani ya kokwa, na anatakiwa kutolewa harakla sana, hii kusingizia kuoza kwa embe mkasahau mdudu huyu ni sawa na kujitia Upofu..
 
kamati ya nishati na madini ilivunjwa ilikua inaundwa na
1. january makamba kwa sasa ni selemani zedi- m/kiti
2. diana chilolo-m/mwekiti
3. khalfani aesh kwa sasa kavuliwa ubunge na mahakama.
4. prof.kulikoyega kahigi
5. yusufu haji khamisi
6. mariam kisangi
7. catherine magige
8. amos makala kwasasa naibu waziri wa habari u. na michezo
9.dkt. anthon mbasa
10. abia nyabakari
11. charles mwijage
12. yusufu nassir
13. ole sendeka
14. mussa silima (marehemu)
15. dkt. festus limbu
16. shafin sumar
17. lucy mayenga
18. josephine chagulla
19.mwanamrisho abama
20. david silinde
21. suleiman masoud
22. selemani zedi kwasasa ni m/kiti
23. kisyeri welema chambiri
24. munde abdallah
25. sara msafiri
26. vicky kamata
27. ali mbaruk salim
28. pamela pallangyo katibu wa kamati
hii ndio kamati ya nishati na madini.
Dah Leo tume save posho ya vikao kwa Tsh ngapi Vile?...Spika kavunja kamati ya bunge kwa maslahi ya Taifa, ametunusuru mamillioni. ahaaa! ahaa!!!
 
Zitto hayuko kamati ya nishati na Madini jamani aliyekuwa ni January Makamba naye kisha acha nafasi hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Naibu waziri.. Nafikri mwenyekiti wake anaitwa kitu kama - Selemani..
Watu mnataka tu kumwona Zitto akipigwa chini Miafrika bana duh!

mkuu kamati ya mashirika ya umma na yenyewe ni miongon mwa kamati zinazohujumu tanesco n andio maana kama ulimsikia zitto alaitetea sana swala la umeme kukatika tz nzima kwa kigezo kwamba tanesco iliingiliwa katika matumizi ya fedha zake na serikali lakn kumbe hali haikauwa hivyo ni kwamba wao walitakiwa kwenda kuchukua mafuta kwa PUMA na hata hivyo waziri prof alisafiri toka dom kwa gari hadi dar na bado mafuta hayakuwa yamenunuliwa na ndipo aliposhukia tanesco na mafuta yakapatikana tena kwa mali kauli kutoka kwa hawa PUMA so zitto kama ndo muuza tairi ama muuza nguzo anajijua mwenyewe. ila anahusika sana tu
 
Kuvunja kamati moja moja hakutasaidia chochote. Bunge lote linanuka rushwa, Dodoma kumejaa lobbyists. Kanuni za bunge zipitiwe upya, na kila kila mmbunge anayekutana na makampuni/au madalali wa makampuni iwe wazi.

Pia ningetaka kuona Spika anafanya kazi kwa kutumia akili yake badala ya kuleta usanii wa kipumbavu wa kumpandikiza mbunge atoe hoja ili ionekane imetokana na bunge. Ina maana kama mbunge hakutoa hoja Spika asingefanya chochote? Anaridhika kuongoza bunge lilizama kwenye rushwa? Kama hajaridhika anafanya nini? Au mpaka apewe maagizo?

Hakumpandikiza Mbunge atoe hoja ili ionekane imetokana bunge hii sio sahihi, Vita Kawawa (Mb) akichangia akichangia hoja ya wizara ya nishati na madini leo asubuhi sambamba na mchango wake kwa kutumia kanuni ya 53 ya bunge (nisahihishwe) alilitaka bunge kutaja majina ya wabunge wanaohusishwa kutaka Mangula.

Na kwamba bunge lifahamishwe wahusika hao, spika alimpinga kwa hoja kwamba Vita Kawawa alisimama kuchangia tu, hivyo hakutoa hoja...
Na ndio maana baadae amemruhusu kutoa hoja na ikaungwa mkono.

Ndivyo ilivyokuwa unless FJM uwe unaona kwa angle tofauti.
 
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya nishati na madini
  1. Selemani Zedi-mwenyekiti alichaguliwa baada ya January kuongezewwa ulaji
  2. Sendeka-mjumbe
  3. Diana Chilolo makamu mwenyekiti
  4. Mh J J Mnyika -mjumbe
  5. wengine mtajazia wakuu,lakini kwa haraka ninaowakumbuka ndo hao
 
Jamani Zitto kabwe kamati yake ni inahusika na masuara ya mashirika ya umma yeye akiwa mwenyekiti, sasa kuvunjwa kwa kamati ya nishati na madini kunamhusu nini?
 
Prof alichosema wanaofanya biashara na Tanesco ni baadhi ya wabunge sasa si lazima wawe ni sehemu ya kamati
 
mkuu kamati ya mashirika ya umma na yenyewe ni miongon mwa kamati zinazohujumu tanesco n andio maana kama ulimsikia zitto alaitetea sana swala la umeme kukatika tz nzima kwa kigezo kwamba tanesco iliingiliwa katika matumizi ya fedha zake na serikali lakn kumbe hali haikauwa hivyo ni kwamba wao walitakiwa kwenda kuchukua mafuta kwa PUMA na hata hivyo waziri prof alisafiri toka dom kwa gari hadi dar na bado mafuta hayakuwa yamenunuliwa na ndipo aliposhukia tanesco na mafuta yakapatikana tena kwa mali kauli kutoka kwa hawa PUMA so zitto kama ndo muuza tairi ama muuza nguzo anajijua mwenyewe. ila anahusika sana tu

zitto hapa lazima ana husika na ndio maana waziri alisema anashangaa watu kusema hawakutenda haki kumsimamisha mkurugenzi wa tanesco!

Pengine ana weza akajitoa! Je kwa nini alikuwa ana mtetea mtu kama huyu ambae watu wana ushahidi ni mwizi, yeye na mafilia yake?
Hapo ndio umakini na heshima ya zitto iliposhuka!

Na kwa mwendo nilio uona ina wezekana ccm wana uhakika zitto alichukua rushwa au anafanya biashara hisivyo na tanesco na ndio maana alimtetea jamaa! Na ni mkakati wa kummaliza kabisa.
 
Kwa sababu binafsi yangu sina imani na viongozi wa nchi yangu na bunge lake nina mashaka sana na kila wanapovunja kamati au kumwachisha mtu kazi. Siku zote ni kwa maslahi ya Mafisadi. Nakumbuka toka katibu mkuu wa Tanesco Patrick Lutabanzibwa miaka ile ya IPTL hadi Mwenyekiti kamati ya Bunge ya nishati na Madini alipokuwa Shelukindo na Mwakyembe walivyopigwa vita hadi majimboni mwao kwa scandal ya Richmond na wengine ndio hawakurudi tena bungeni.

Siwezi uamini maamuzi yoyote ya bunge yanayofanywa pasipo uchunguzi kufanyika na wahusika kuhojiwa kwa sababu sijawahi kuona bunge likivunja kamati yoyote kwa tuhuma pekee siku zote Spika amekuwa wa kwanza kuwaomba washtaka kutoa ushahidi tena kwa amri na ukali huwapa muda wa kuwakilisha ushahidi wao..

Kifupi sina imani na Spika wala bunge kwa sababu hawa wote ni vibaraka wa Mafisadi ambao wamejikita ktk wizara hii ya Nishati na madini toka 2007 na sasa hivi wameitawala wizara hiyo ambayo kwa leo ndio Uti wa mgongo kwa uchumi wa taifa la walalahoi..

hata mimi hii spidi ya spika ya kuafiki hoja ya kuvunja kamati inanipa wasiwasi.
sitashangaa iwapo kuvunja kamati ni mkakati wa kuficha madudu.
 
Dah, mungu saidia! Wezi siku zenu zinahesabika, ni suala la muda tu!
 
Jamani Zitto kabwe
kamati yake ni inahusika na masuara ya mashirika ya umma yeye akiwa
mwenyekiti, sasa kuvunjwa kwa kamati ya nishati na madini kunamhusu
nini?

Just coold down Gondwe the young man Zito this time has bite something bigger than he can chew
 
Ni aibu kubwa kwa greatthinker kuhoji maswali ya ajabu. Hv mnaouliza kamati za ZZK hamjui kuwa upinzani wanaongoza oversight pekee na MH. ZZK ana POAC. Nishati na madini ni Selemani Zedi wa CCM
 
Hahahaa jamani mapenzi na chuki binafsi ni kitu hatari! Yani kwa ajili Mnyika ni mjumbe wa kamati ya Nishati iliyovunjwa, sasa unataka ivunjwe ya hesabu ya mashirika ya umma ili iwe Zitto na sio Mnyika. Hahahaa

Mr nice 2 mimi na wewe hatujaelewana. Mara Mhando aliposimamishwa kamati ya kwanza ya Bunge kukurupuka na kutaka kujua kwa nini amesimamishwa ni ya POAC; pili kama ulifuatilia hotuba ya Mh. Mnyika haikumpamba mtu yeyote hivyo kutoa maamuzi ya jumla kwa wanakamati wote ni wala rushwa si sahihi. Au ukali wa ile hotuba walinywa rushwa ndio ikaandikwa vile kwamba Liwalo na Liwe?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom