Rushwa Bungeni: Kamati ya bunge ya Nishati na Madini yavunjwa

Sasa mnaona ushahidi Mawaziri waliokuwa wameteuliwa kishikaji walivyokuwa wanatumaliza

Sisemi zaidi, sitaki kunukuliwa
 
Spika wa bunge ameivunja rasmi kamati ya nishati na madini leo akiitimisha kupitishwa kwa bugdet hiyo......kazi kwako ndumilakuwili Mzito Mkabwela..

Mh. Mnyika nae ni mjumbe wa hiyo kamati Scofied wewe unaamini kuwa kwa ile hotuba ya upinzani ilivyowakandia Tanesco amepokea rushwa? Mimi nadhani kamati ya hesabu za mashirika ya umma ndiyo iliyokuwa inamtetea Mhando na siyo kamati ya nishati.
 
Last edited by a moderator:
mkuu nina hofu sana na vitisho ambavyo amekuwa akipata hata leo humu bungeni jamani prof ni kichwa aisee hata simba chawene na mwenzie wako vizuri hofu wasije tu waka mfanya kama mwakyembe walivyo mfanya.
inabidi wawape ulinzi!
Ngoja nika google niangalie kama nitawapata wajumbe wa kamati hii
 
Kimsingi, kuvunjwa kwa hii kamati ni kwamba Spika amekubali madai ya rushwa, sasa nategemea pamoja na kuivunja, hatua za kisheria zitakuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote. Bunge halina mamlaka ya kutafsiri sheria, watuhumiwa wafikishwe mbele ya mahakama ijulikane moja.
 
Iwapo itakuwa kweli si kisasi iwapo itakuwa uongo kitakuwa ni kisasi na kutaka kumchafua ZZK na kumshusha kisiasa. Cha muhimu tunamuomba Zitto ajitokeze akanushe hizi tuuma iwe kwenye vyombo vya habari au hata humu JF ili tuendelee kuwa na imani naye lakini akikaa kimya inaonyesha kuna ukweli ndani yake.
 
kweli nyepesi zuberi kabwe unakazi hii ndo tanzania bana ukitangaza nia vikwazo kibao
 
Akina zitto imekula kwao... No more kupewa hongo na tanesco na wezi wengine.. Safi sana japokua u wonder ingekua kamati iko chini ya kigogo wa ccm sidhani kama wangeivunja
 
Kwa sababu binafsi yangu sina imani na viongozi wa nchi yangu na bunge lake nina mashaka sana na kila wanapovunja kamati au kumwachisha mtu kazi. Siku zote ni kwa maslahi ya Mafisadi. Nakumbuka toka katibu mkuu wa Tanesco Patrick Lutabanzibwa miaka ile ya IPTL hadi Mwenyekiti kamati ya Bunge ya nishati na Madini alipokuwa Shelukindo na Mwakyembe walivyopigwa vita hadi majimboni mwao kwa scandal ya Richmond na wengine ndio hawakurudi tena bungeni.

Siwezi uamini maamuzi yoyote ya bunge yanayofanywa pasipo uchunguzi kufanyika na wahusika kuhojiwa kwa sababu sijawahi kuona bunge likivunja kamati yoyote kwa tuhuma pekee siku zote Spika amekuwa wa kwanza kuwaomba washtaka kutoa ushahidi tena kwa amri na ukali huwapa muda wa kuwakilisha ushahidi wao..

Kifupi sina imani na Spika wala bunge kwa sababu hawa wote ni vibaraka wa Mafisadi ambao wamejikita ktk wizara hii ya Nishati na madini toka 2007 na sasa hivi wameitawala wizara hiyo ambayo kwa leo ndio Uti wa mgongo kwa uchumi wa taifa la walalahoi..
 
Tuhuma za rushwa zimetawala kwa baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,ingawaje hawajatajwa bungeni rasmi ila mmoja wapo ni Zitto Kabwe,na kwa hoja iliyotolewa na Vita Kawawa ya kuvunja kamati ya nishati na madini na nyingine zilizoshutumiwa;pengine POAC inayoongozwa na Zito,je kwa shutuma hizi haiwezi kuwa ni mipango ya kummaliza Zitto kisiasa baada ya yeye kuwamaliza wenzake?rejea sakata la kutokuwa na imani na waziri mkuu iliyopelekea baraza la mawari kuundwa upya na wengine kutoswa.JE NI SHUTUMA ZA KWELI AU NDIO VISASI?
Nakapanya unaweza kuwa sahihi au usiwe sahihi. Unlike kamati ya Cheyo, kamati ya Nishati na ile ya POAC wamekuwa "more serious" kwenye kuisimamia serikali naona anataka kuzipunguza makali tegemea Mh.Mbatia kuongoza kamati mojawapo nyeti
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti wa hii kamati ni Seleman Zedi, miongoni mwa wajumbe wa hii kamati ni Sara Msafiri (mbunge Viti maalum UVCCM) Munde Tambwe (viti maalum CCM), Chirstopher ole Sendeka, John Mnyika (CDM). Hii kamati ilikuwa inaongozwa na Naibu waziri wa sayansi na Technolojia Januari Makamba kabla ya reshufle ndogo iliyofanywa na JK Mwanzoni mwa mwezi June

Selemani Zeddy atawajibika kisiasa kwa sababu yeye ndie Mwenyekiti wa hii kamati, Wanaodaiwa kuivuruga TANESCO ni Zitto Kabwe na January Makamba, wakishirikiana na Munde Tambwe na Sara Msafiri. Sina nia ya Kumsafisha Zeddy but jamaa ni Clean, namfahamu since akiwa ZAIN. Haya madudu aliyoyasema Prof. Mulongo yalifanyika January Makamba akiwa ni Mwenyekiti.

Munde ni fisadi mkubwa aliwahi kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na Manispaa ya Tabora kwa ubadhirifu wa Shs 987,214,000/= akiwa ni karani idara ya uhasibu manispaa ya Tabora.

Nashauri ni vizuri kamati ya uongozi ya bunge uwe unawafanyia wajumbe wa kamati vetting kabla ya uteuzi
 
Sijaelewa, iliyomtetea Mhando ni kamati ya madini na nishati au ni ile ya mashirika ya umma?
 
Wapi Ritz, Rejao, Mkigoma, et al? Hutokaa uwaone kwenye uzi kama huu unaojadili maslahi ya taifa! Ha ha ha ha!
 
Zitto hayuko kamati ya nishati na Madini jamani aliyekuwa ni January Makamba naye kisha acha nafasi hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Naibu waziri.. Nafikri mwenyekiti wake anaitwa kitu kama - Selemani..
Watu mnataka tu kumwona Zitto akipigwa chini Miafrika bana duh!
 
ila wamechana laivu fred na mama yake paoja na lwakatare safi sana. hebu gugo unipe desa

yapo hapo ndipo palipo niacha hoi hivi fred na veronica ndio wanafanya tukose umeme? Yani watu watatu ni zaidi ya watu million 40 kweli.
Hivi zitto alikuwa ana tetea nini?
 
Spika wa bunge ameivunja rasmi kamati ya nishati na madini leo akiitimisha kupitishwa kwa bugdet hiyo......kazi kwako ndumilakuwili Mzito Mkabwela..

ameshanunuliwa huyu jamaa hela sio kitu cha mchezo ndio mana Yesu alimsamehe tu yuda
 
Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa ilikuwa inaundwa na:

1. January Makamba (kwa sasa ni Selemani Zedi) - M/kiti
2. Diana Chilolo- Makamu Mwenyekiti
3. Khalfani Aesh (kwa sasa kavuliwa ubunge na mahakama).
4. Prof. Kulikoyega Kahigi
5. Yusufu Haji Khamisi
6. Mariam Kisangi
7. Catherine Magige
8. Amos Makalla (kwa sasa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo)
9. Dkt. Anthony Mbassa
10. Abia Nyabakari
11. Charles Mwijage
12. Yusufu Nassir
13. Ole Sendeka
14. Mussa Silima (marehemu)
15. Dkt. Festus Limbu
16. Shafin Sumar
17. Lucy Mayenga
18. Josephine Chagulla
19. Mwanamrisho Abama
20. David Silinde
21. Suleiman Masoud
22. Selemani Zedi (kwa sasa ni m/kiti)
23. Kisyeri Werema Chambiri
24. Munde Abdallah
25. Sara Msafiri
26. Vicky Kamata
27. Ali Mbaruk Salim
28. Pamela Pallangyo - Katibu wa Kamati

hii ndio kamati ya nishati na madini.
 
Back
Top Bottom