Rushwa anayoiona Sumaye: Takukuru mpo wapi?

Amiliki

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,085
1,004
Nimemsikiliza kwa makini Mh. Waziri Mkuu Mstaafu kwa heshima (si kwa kashfa ya kutuibia wananchi), Mh. Fredrick Sumaye akieleza kwamba rushwa ndani ya chaguzi za CCM si tatizo jipya ispokuwa la sasa limekuwa la aina yake kidogo kwani ni rushwa ya "Kimtandao" ambapo mtu anaweza akawa sehemu nyingine lakini aka-influence uchaguzi wa watu anaowataka toka sehemu nyingine ya nchi so long kwamba watakaochaguliwa atakuja kuwatumia huko mbeleni.

Swali ninalojiuliza, kama hivi vitu vipo dhahiri kihivi mpaka akina Sumaye wanavizungumza hadharani na hatujasikia mtu yeyote amekamatwa na rushwa na kuhukumiwa kwenye chaguzi za CCM, je kweli kuna haja gani ya kuwa na chombo kama Takukuru ambacho kinaendeshwa kwa kodi zetu?

Naomba kuwasilisha.
 
Sumaye alipokuwa waziri mkuu aliwaambia wafanyabiashara wakitakata mambo yao yawanyookee wajiunge na CCM.

Wenye pesa zao wakaitikia wito wamejiunga! sumaye anaanza kulialia na kula matapishi yake mwenyewe.

Amefilisika kisiasa; ni mwanasiasa aliyefulia.
 
mgomba101

Ni kweli hayo ni mapungufu yake, lakini hayazuii wajibu wa Takukuru wa kupambana na rushwa.
 
Last edited by a moderator:
TAA KUUKUU na si TAKUKURU wangekuwa ni chadema ungesikia wametuma helikopta ya polisi ikambebe mtoa rushwa...Chamacha magamba at work
 
Wakina hosea wanampangoo wa kwenda kugombea huko baada ya kuhujumu taifa sasa watakapozuia rushwa na wakati ndio njjia pekee inayomweka rais na wabunge wake mpaka leo hii atakwa mwendawazimu
 
Wakina hosea wanampangoo wa kwenda kugombea huko baada ya kuhujumu taifa sasa watakapozuia rushwa na wakati ndio njjia pekee inayomweka rais na wabunge wake mpaka leo hii atakwa mwendawazimu
Takukuru is a toothless organization!

Ukiona Takukuru wamemkamata mwana CCM kwa rushwa, ujue ni kwa maelekezo ya mkuu wa nchi! Haiwezekani rushwa ndani ya CCM zipo waziwazi kabisa, wagombea wakitumia mabilioni kuingia madarakani, badala yake mtasikia wanakamatwa akina Mwakalebela ambao wanadaiwa wamehonga shilingi elfu 50!

Wakati tumemsikia Sumaye akisema rushwa ndani ya CCM, ni ya mtandao, mtu anaweza akawa eneo fulani, lakini akitaka kuwaingiza watu wake kwa kutumia fedha kwa njia ya mtandao, anaweza kufanya hivyo, hata kuwapa ushindi wagombea katika wilaya zinazofikia hata 80! Kwa mazingira hayo bado Takukuru inatamba kuwa inapambana na rushwa Tanzania!

Lakini jambo hilo halishangazi sana, maana katika majina 30 yaliyomwagwa siku za karibuni, za wale mabilionea walioficha mapesa mengi Uswisi, na jina la Hosea lilitajwa!!
 
Tangu tangu iazishwe mimi sioni manufaa yake.Kimekuwa ni chombo cha kutafuna kodi zetu.Nasikia wanalipwa mishahara minono.Ni bora ifutwe.
 
Tume ya Kupamba na Kushiriki Rushwa Takukuru haina maana yoyote. Imejaza wala rushwa na vibaka ambao ukiwauliza walivyochuma mali zao hawana la kukwambia. Watawala mafisadi mara nyingi huanzisha vitu vya kuwapumbaza wananchi ili waendelee na mchezo wao mchafu. Takukuru ni kinyume cha kile unachodhania imesimamia-ni wala rushwa wakubwa. Kaangalia utajiri wa bosi wao utapata kichaa.
 
Inasubiri kama mwewe mwenye njaa kusubiri Simba ashibe na yenyewe ipate makombo ya kula
Maana tuhuma zinatolewa na bunge au vyombo vingine na yenyewe inakurupuka kama imeamshwa usingizini kwenda kusema inafanya uchunguzi na kutafuta ushahidi wa kuwapeleka watuhumiwa madarakani
Ila yenyewe haipo kwa kazi iliyopewa kuzuia na kupambana na rushwa ila inapambana na matokeo ya rushwa au wale ambao tayari washapokea rushwa
 
Sumaye naye mnafiki. Kama ameona kuna rushwa na hakuna haki CCM anangoja nini? Je anavuna alichopanda au anapanda alichovuna?
 
Tume ya Kuruhusu na Kuilinda Rushwa Tanzania...eti mpaka leo bado wanachunguza kuhusu mafisadi wa ndani ya Serikali waliokutwa na mabilioni katika bank accounts zao kule Switzerland.
 
Ni kweli hayo ni mapungufu yake, lakini hayazuii wajibu wa Takukuru wa kupambana na rushwa.

Muhuni tu Tluway, mbona asiwataje waliotoa rushwa kulikuwa na essence gani kupiga hadithi zile ambazo hakuna asiyezijua ndani ya chama cha mapinduzi?
 
Nani alikwambia TAKUKURU iko pale kupambana na rushwa?

Ile ni taasisi kwa sasa iko pale kulinda maslahi na mienendo ya watawala, lengo ni kufunika(Covering) uovu wa watawala.

Ndio maana kwa kadri takukuru ilivyoboreshwa(kuongezewa bageti na kupewa nguvu ya kisheria) ndio ambavyo rushwa ndogo na kubwa zimeongezeka mara dufu.

Embu fikiri mtu anaeiunda(JK) ni mla rushwa namba mmoja, anaeisimamia(Hosea) ni mla rushwa mkubwa, halafu anategemea nini?

Takukuru itaanza kupambana na rushwa siku utawala wa CCM ikiwa umeondoka madaraka.

Tuungane pamoja kuindoa CCM madarakani ili rushwa itokomezwe nchini.
 
Hivi ni chombo gani chenye mamlaka ya kufanya checks na balance pccb? ukiacha Dpp?

pili, je ofisa wa takukuru anaweza kumkamata mla rushwa influencial bila kibali cha siasa? waziri au rais?

tatu, je pccb ina wachunguzi wenye sifa?

nne, rasilimali kwa maana ya investment tuliyoifanya kwa kuiunda pccb, kuiwezesha in terms of majengo, human capital pamoja na mihela tunayowapa monthly je iko justified na vikesi vya kusingizia watu? na kukwepa kushtaki eg Epa, rada nk?

tano, kuonyesha kwamba tunapoteza pesa za nchi bure kwa hawa jamaa, ni kwamba over 90% ya kesi zao hufunguliwa baada ya media kufunguka na wao kuumbuka, sasa kama ndivyo polisi na Dpp wanatosha.

sita, kwenye kuzuia rushwa ndo kwa elimu kwa umma pekee? kwa kuunda club mashuleni? wameintervene mangapi kwenye tender, ajira nk ushuzi mtupu

On my opinion ant-corruption body in any country is a must, but a non profesional body is a waste, hatuna haja ya TZ kuwa na Takukuru tuna haja ya kuwa na chombo cha kitaalam, huru chenye weledi wa kuzuia na kupambana na rushwa likini hii agency tulionayo leo ni redundant.
 
ni wakati kwa serikali kutoa maelezo ya kina kuhusina na rushwa katika chma tawala cha (ccm)mafisadi
 
Hakuna siasa ila ni kudanganyana tu na mwanasiasa yoyote haaminiki hata awe nani.Sumaye anajua kama kuna rushwa tokea yupo na madaraka mbalimbali na asitudanganye kama na yeye hana madhambi.Kama kweli anaichukia na anajua kama rushwa ni dhambi basi angetoboa siri zote tokea hapo zamani lakini isiwe leo hii katolewa ndio aanzishe mazungumzo haya ni haisaidii kitu.
 
Hakuna ushahidi wa mtu kula au kutoa rushwa ktk chaguzi za ccm zinazoendelea. Pia kesi zilizopo Takukuru zimeshatosha maana wamepeleleza zaidi ya matajalio yao kwani . Wameshavuka malengo yao ya 2011/2012 hivyo sasa ni kutulia na record waliyokwisha ivunja. Kwa Mwaka huu kama unaweza kuchukua au kutoa rushwa wala wewe usiofu kwani Takukuru itaanza kazi lasmi january 2013.
NB: Naomba mtu aliye na mawasiliano ya kundi la wale waliosemwa na Sumaye kuwa wanapesa za kutosha ili nami nipate kujiunga na mtandao huo. Ni vema tufikirie kuungana na wanamtandao kwani hatuwezi tena kuwa upande wetu wenyewe na tukafika salama.
 
Huenda Takukuru si chombo sahihi cha kupambana na rushwa au Watendaji waliopo pale si Watu sahihi kuwepo kwenye chombo hicho.
 
Muhuni tu Tluway, mbona asiwataje waliotoa rushwa kulikuwa na essence gani kupiga hadithi zile ambazo hakuna asiyezijua ndani ya chama cha mapinduzi?

TAKUKURU ingejua kazi yake ingemhoji Sumaye ili atoe ushahidi wake. Hata hivyo, inasemekana kuwa siku hiyo
pale Katesh, TAKUKURU ilikaa kimya na ndiyo maana hadi leo wametulia kama suala lisilowahusu.
 
USELESS!! WHAT A WASTE OF TAX PAYER'S MONEY!!! yani hii organisation ni ya kulinda wala rushwa wakubwa na wale wadogo (waganga njaa) ndo wanaoshughulikiwa tena kwa kubambikiwa ili organisation ionekane wanafanya kazi!!! ama kweli TUME YA KULINDA NA KULINDA RUSHWA!!!
 
Back
Top Bottom