Bryson Mbeula
Member
- Sep 25, 2011
- 46
- 4
Kwa ufupi ni aina ya utapeli ambapo anakuja mtu mmoja kwako kama wewe ni mwenye pesa anatangaza kuitafuta rupia tena anasema dau kubwa, akiondoka baada ya siku kadhaa, anakuja mwenzake ambaye anatangaza kuuza rupia kwa bei ya chini kidogo tofauti na ile aliyotangaza yule wa kwanza. Let's say, jamaa alisema atainunua kwa 10milion, huyu mwenye nayo atasema anauza 7ml. Hivyo kwa kuwa wewe unataka faida, na jamaa kakuachia mawasiliano, unampigia kumwambia umepata rupia, hapo tapeli mnunuzi atakusisitiza uinunue yeye akija atakupa hiyo 10m..kwa tamaa zako unanunua ili upate faida nono ndani ya kipindi kifupi. Ukinunua tu, jamaa wanaenda kugawana hizo hela na huo ndio unakuwa mwisho. Pia kuna ujanja mwingine wa kitapeli wa kumtajirisha mtu kwa rupia..itategemea wamekuingia kwa gia ipi. But all in all, rupia ni utapeli. Be warned
Daah!ebwana eee,haya maisha yana mambo mengi kweli,nilishuhudia jirani yetu anafirisika hivi hivi kwa kutafuta rupia!