Rungwe District Football Association Office

Mwanjelwa

JF-Expert Member
Jul 29, 2007
956
145
These are kind of our football associations' offices at District level.

See the attachment
 
Attachments

  • Rungwe Football Office.jpg
    Rungwe Football Office.jpg
    59.5 KB · Views: 94
Choka fulani lakini si choka mbaya, let alone choka hatari, mi nilifikiri nitakuta mbavu za mbwa hivi.

Maana kuna Choka, Choka Fulani, Choka Mbaya, Choka Hatari na mwisho kabisa huko inakuwa si choka tena kuna Kufa Mtu. Hizo ndizo SI Units za nyumba mbovu kwa mujibu wa redio mbao.

Sasa hii Choka Fulani.

Mara nyingine kuwa na ofisi kama hizi zisizopita uwezo wa wananchi kwa sana ni poa tu, si unaona ofisi haina tofauti sana na nyumba za wananchi zilizo karibu hapo?

Sio mnajenga mkanisa mkuuubwa kama wa Yamoussoukrou unalipita mpaka Basilica la Rome, au kasri kubwa kama la Mzee Mobutu Gbadolite, halafu jirani wananchi wanaishi katika mbavu za mbwa na paa za nyasi.
 
Hivi niulize...Uwezo wa wanasoka unazaliwa kutokana na uzuri wa jengo la klabu yao, au ni mazoezi ya uwanjani?...! Lakini pia hapa Bongo unapoona jengo la mpira kama hilo ujue uongozi wa eneo hilo, kama ni wilaya au mkoa unatoa kipaumbele cha namna hiyohiyo kwa mpira!...Kwani tangu lini tukathamini mpira mkuu?
 
Mazee unaji contradict sasa.

Mara unasema/ question (by way of a rhetorical question) kwamba uwezo wa soka hautegemeani na uzuri wa jengo, which means watu wanaweza kuwa na jengo duni na soka nzuri.

Halafu hapo hapo unawalaumu watu wa eneo hilo kwa kutothamini soka mpaka jengo lao linakuwa duni hivi, na ku infer kwamba hata soka nalo litakuwa halijaliwi hivi hivi (completely negating your original position).

Sasa wakikunukuu na kukuambia uzuri wa soka hautegemei uzuri wa jengo, na wao wanaweka mkazo katika soka na sio katika jengo, utawaambia nini? In fact wanaweza kukwambia kwamba sababu ya jengo kuwa duni inawezekana kabisa ni kwamba wanawajali wachezaji zaidi na hawawezi kuhudumia wachezaji na jengo kwa sawa. Utawaambiaje?

Kama una facts njoo nazo hapa lakini ukianza kufanya assumptions zenye contradiction inakuwa tacky.
 
Kwa mtazamo wangu mimi kazi za ofisi hiyo kwa level ya wilaya ni ya uratibu tu ambayo pengine wajumbe wa kudumu ambao mara nyingi ni katibu na mwenyekiti wa wilaya, na ukizingatia muundo na umuhimu wa soka ambao tayari tunautekeleza kwa sasa ni soka la ridhaa sio la kulipwa na hii ndiyo maana hata wahusika (katibu na mwenyekiti wake) sio kazi pekee wanayofanya. wana kazi zao za ajira somewhere na hapo ni kama kijiwe tu. Na hii nijuavyo mimi ni hadi level ya ofisi ya TFF mkoa (kama nakosea wadau mtanifahamisha.

Hivyo kwa maelezo yangu hayo, ofisi ya namna hiyo haihitaji ubora unaozidi ilivyo kwani hata kufunguliwa kwa inaweza ikapita wiki nzima ikiwa haijafunguliwa.

Wajameni tusije kuingia kwenye mtego ule ule wa kukarabati ofisi za bunge kwa 30......bn wakati ki msingi sio kipaumbele na pia hakuna matatizo yoyote ya kiutendaji yanayo sababishwa na jinsi ofisi ilivyo sasa. Hii ofisi ya TFF Rungwe district binafsi naifahamu na haina ubaya wowote na nina amini nchi hii hii kuna wilaya hazina ofisi kabisa.

Labda tuhoji utendaji wa ofisi husika vinginevyo kwa level yake iko bomba sana !! Ukizingatia kwa pembeni kuna kinywaji na nyama choma, we acha kabisa !!
 
Duh! Hizi ndizo ofice zetu za mikoani na wilayai. Ila ukiuliza wapepata kiasi gani utashangaa ni kwanini hawazitumii kuendeleza ofice kama hizi! Lakini ndiyo kibongo bongo.
 
Choka fulani lakini si choka mbaya, let alone choka hatari, mi nilifikiri nitakuta mbavu za mbwa hivi.

Maana kuna Choka, Choka Fulani, Choka Mbaya, Choka Hatari na mwisho kabisa huko inakuwa si choka tena kuna Kufa Mtu. Hizo ndizo SI Units za nyumba mbovu kwa mujibu wa redio mbao.

Sasa hii Choka Fulani.

Mara nyingine kuwa na ofisi kama hizi zisizopita uwezo wa wananchi kwa sana ni poa tu, si unaona ofisi haina tofauti sana na nyumba za wananchi zilizo karibu hapo?

Sio mnajenga mkanisa mkuuubwa kama wa Yamoussoukrou unalipita mpaka Basilica la Rome, au kasri kubwa kama la Mzee Mobutu Gbadolite, halafu jirani wananchi wanaishi katika mbavu za mbwa na paa za nyasi.

Yaa. Lakini kwa hizi office ndugu yangu, tunaweza fika popote kweli? Maana ni choka hasa na kwa hakika wakati nikipiga picha, kwa siku mbili ilikuwa hazijafunguliwa kabisa! Nilishangaa sana na bado siweze hata kuamini. Nashindwa kushangaa
 
Back
Top Bottom