'Ruksa' kwa watumishi wa umma kushiriki siasa

Acha uongo wewe Dr.(?) Kamala aliposhindwa ubunge wa Nkenge hakurudi MZUMBE IDM kufundisha.

Dr. Mvungi alikuwa mgombea, hakuchagulia, wapo aspirants wengi tu kutoka CCM walioshindwa kwenye preferential votes na wengine kwenye general election lakini wakarudi makazini. Tatizo hapa ni kwamba tayari umechaguliwa wether VITI MAALUM au kupitia JIMBO automatically unapoteza ajira ya utumishi wa umma.

BTW, serikali siku nyingi ilishasitisha LIKIZO BILA MALIPO, unless for special jobs kama wale wanaokwenda kufanya kazi kwenye International organization. Sijui kama viti maalumu ni SPECIAL JOBS.

But one thing I'm SURE for, and I bet my neck. First Kama huyo binti asingekuwa mtoto wa Kawawa and Second Kama binti huyo angeupata huo ubunge wa viti maalumu kupitia vyama vya UPINZANI. Believe asingerudi tena NSSF.

BTW, sikapendi haka ka-binti kwani eti ndiyo kawa wakilishi ka wafanyakazi kupitia viti maalumu, lakini sijakasikia hata siku moja kakitetea wafanyakazi kuhusu sheria kandamizi ya SSRA ya kuzuia mafao ya kujitoa. UZURI WA MKAKASI NDANI NI KIPANDE CHA MTI!

Sina uhakika kama amewahi kufanya kazi ofice hiyo. Unakumbuka huo waraka ulitoka lini? Mimi nakumbuka kama uliotoka baada ya uchaguzi wakati tayari yeye alishaondoka.
 
haki pekee ya mtumishi wa umma ambayo habanwi na sheria ni kupiga kura kushiriki siasa on favour ya magamba ya magamba watakustahi vinginevyo unahatarisha ajira yako ila unaweza kupiga siasa nje ya eneo la kazi .
Nasikia kuwa magamaba hawana maofisa waandamizi.
 
Jamani naomba msaada wenu wa kisheria,ninawauliza wenzangu je ni kosa kushiriki siasa ukiwa mtumishi wa shirika lililo chini ya serikari, kama vile TRA,TANROAD nk, wengine mtanishanga lakini wanajamii wenzangu nisaidieni
 
kwa maadili yao kosa, na wakijua tu hasa ukiwa chama pinzani wanakumwaga..kuwa makini utapoteza kazi
 
Sio kosa kabisa.
Ukweli ni kwamba ccm hawakuwa tayari kwa mfumo wa vyama vingi au walijua vyama vyote vitakuwa chini yao iliwaweze kupata misaada ya wadhungu na kwa kiasi flani walifanikiwa maana vyama pinzani vingi ni vibaraka wa ccm,wanatuhadaa wananchi,sasa cdm ndiyo chama halali cha upinzani ccm,ndiyo maana ccm lazima wakatae halikuwa lengo lao kuwa na chama kinachoishi upinzani wa kweli, pia vyama vingine vinavyojiita upinzani kiukweli sio wapinzani ila ni njia za kujirahisishia maishatu kama kina mbatia na wezake,sikiliza kauli zao wanalaumu chadema kufanya mikutano kila kukicha.wanadai siasa safi,sijui wanamaanisha siasa safi ni kutofanya mikutano au kutokosoa serikali na kuwaambia ukweli wananchi!!!!!ccm hawakuwa na nia ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi ndiyo maana haya yote yanatokea.
 
Code of Ethics and Public Service Conduct - Tanzania.
IX. Political Neutrality
1. A public servant can participate in politcs provided that when so doing observe the following limitations:-
i) Shall not conduct or engage oneself in politics during working offocial hours or at working premises;
ii) shall not take in political activities which will compromise or be seem to compromise his/her to the Government loyality;
iii) inaendelea.
Kwa miongozo zaidi tafuta "Code of Ethics"
 
Habari zenu wadau wenzangu wa JF! Mimi ni kijana wa kitanzania ambaye nimemaliza shahada yangu ya kwanza katika Elimu katika chuo kimoja cha umma hapa nchini mwaka huu.Ndugu zangu binafsi nahusudu sana siasa na hata pale chuoni niliwahi kushika nafasi ya ubunge wa kuchaguliwa,swali langu nahitaji kufahamu,, Je endapo nitakuwa muajiriwa wa serikali naweza nikaendelea kufanya siasa hasa za vyama vya upinzani ili kutimiza ndoto zangu?.Tafadhalini naomba ushauri wenu,maana ishatokea watu wengi wanaonifahamu wananitabiria mafanikio makubwa katika siasa.
 
hili ni darasa tosha na inabidi makala kama hizi ziandikwe na kutolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hata kwenye mikutano ya kisiasa
 
Ni sheria tu kandamizi ambazo tumezirithi toka kwa wakoloni. Wakoloni waliwazuia watumishi katika serikali za kikoloni kushiriki siasa kwa sababu ya kupunguza nguvu za movements za kudai uhuru. Ndo mana Nyerere alipojiingiza kwenye harakati za chama cha Tanu alilazimika kuacha kazi yake ya ualimu. Cha kushangaza baada ya uhuru sheria hiyo ikarithiwa kama ilivyo, mi naona ni wakati sasa kuitafakari upya sheria hiyo kama ina tija yoyote, na kama sivyo iondolewe.
 
Ni kweli watumishi wanaruhusiwa kujihusisha na siasa, hakuna sheria inayozuia watumishi waote kujihusisha na sisa. ILA ifahamike kwamba pale multipartism ilipoanza CCM walikuwa waoga sana hasa baada ya MREMA kuwachachafya, waliamini watapoteza uchaguzi wa 2000. Hivyo watua walizoanza kuzichukua ilikuwa ni KUKANDAMIZA watumishi wanajihusisha na "siasa za upinzani", watumishi wakawa waoga mpaka sasa. HATA HIVYO hali inaendelea kubadilika, japo kwa kasi isiyoridhisha. WATUMISHI WAPINZANI WA SERIKALI walikuwa wanakandamizwa (1) kwa vitisho na ubabe wa wakubwa zao; (2) kwa sheria inayotaka pale mtumishi anapoteuliwa kupeperusha bendera ya chama cha siasa, akishindwa harudi kkwenye utumishi, na hii haijabadilika; na (3) basi usiporudi kwenye utumishi, unakosa kazi - hii kwa sasa si tatizo kwani watumishi wana vyanzo mbadala vya mapato kuwawezesha kuishi biala utumishi wa umma kwa sasa. Kwa hali inabadilika
 
Ni kwa muda mrefu tumekuwa tukishuhudia watumishi wa Umma au Waliostaafu Utumishi wa Umma wamekuwa wakitangaza nia au kugombea nafasi za kisiasa hasa Ubunge au Urais kupitia CCM, kwani kwa vyama upinzani sio tukio la kawaida.

Lakini kama inavyojulikana, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa pamoja na ya Utumishi wa Umma, Mtumishi wa Umma haruhusiwi kushiriki active politics i.e kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au kugombea nafasi za kisiasa wakati akiwa ni mtumishi wa Umma.

Pamoja na Sheria hizo, hata Katiba ya CCM inatamka bayana kuwa mwanachama atakuwa na sifa na haki ya kugombea uongozi ndani au kupitia CCM iwapo atatimiza miaka mitano (5) tangu awe mwanachama.

Hata hivyo, wafuatao waliwahi kugombea au kutaka kugombea kupitia CCM wakati wakiwa watumishi wa Umma au mara tu baada ya kustaafu utumishi wa Umma na bila ya kutimiza masharti yaliyowekwa na Katiba ya CCM:

1.Andrew Chenge- Alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
2. Alfred Tibaigana- Alikuwa Kamanda Polisi wa Kanda ya Dsm
3.Balozi Ali Karume- Balozi wa Tanzania
4. .......................
5. ......................

Swali. Je ina maana kuwa waliendelea kuwa wanaccm wakiwa watumishi wa Umma.?
Na kama sio hivyo, ni lini walipata sifa ya kugombea kwa mujibu wa Katiba ya CCM ilhali bado au walikuwa hawamaliza miaka 5 tangu wamestaafu utumishi wa umma?

mtu yoyote anapoajiriwa serikali wakati ni mwanachama wa chama fulani pindi apatapo ajira serikalini uwanachama wake unasitishwa sio kama anakuwa sio mwanachama bali anaendelea kuwa mwanachama kivuli, ndio maana waajiriwa wengi hugombea pindi wanapostafu au wakati wowote atakapo na pindi apitishwapo na chama chake kugombea automatic anakuwa sio mfanyakazi tena. Kwa hali ndio maana tibagana na chenge waligombea.
 
mie ni mwanachama na mwanaharakati ila hapa halshauri m.wa wilaya anapita eti anaonya juu yangu kushabikia upinzani CDM
 
Habari ndugu wana JF! Mimi ni muhitimu wa chuo kikuu ngazi ya shahada ya kwanza ya elimu na Mungu akipenda nategemea kupangwa post za ualimu mapema mwakani,ndugu wadau swali langu nahitaji kufahamu, je naweza nikajikita katika harakati za siasa wakati nikiwa kazini? Maana binafsi ni mkereketwa wa siasa za upinzani na vilevile nina mpango wa kugombea chaguzi zijazo ndani ya chama na serikali.
 
Yaani mhitimu wa chuo kikuu gazi ya shahada hujui haya unayouliza? Sasa hao wanafunzi utakuwa unawafundisha nini?
 
Yaani mhitimu wa chuo kikuu gazi ya shahada hujui haya unayouliza? Sasa hao wanafunzi utakuwa unawafundisha nini?

Niliataka kumjibu lakini umeua kila kitu!

Anyway in a nutshell, sheria zinaruhusu mtumishi wa umma kushirikia siasa i.e kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Lakini pia sheria inakataza (kimaandishi) mtumishi wa umma kuwa kiongozi wa chama cha siasa (ukiwa CCM your exmpted watafumbia macho).

Ukitaka kugombea uongozi i.e Ubunge, Udiwani ni lazima uchukue LIKIZO bila malipo. Hapa ndiyo mtego, kwani kama ukishindwa na uligombea kupitia UPINZANI ukirudi kazini kwako wanakwambia nafasi yako tayari imeshajazwa kaendelea na siasa.

Lakini tegemea mikwara mingi kama mwajiri wako (TAMISEMI/DEO) wakifahamu wewe ni mkerekeretwa wa vyama vya upinzani.
 
Jifunze kujitegemea kwanza , halafu ndiyo uingie kwenye siasa za upinzani , maana kwa kazi yako ya ualimu bila shaka watakufukuza , wana fitna za kutisha ! Unaweza hata kusingiziwa kubaka mwanafunzi wako ! kwani mshahara wao bei gani bwana ! Si ni kama boom tu , tafuta kazi kwenye international firm uwe huru .
 
Bado kurekebisha katiba tu. Huu waraka ni mzuri lakini katiba iko kimya. Inazungumzia maofosa waandamizi, hao ni kina nani? Mambo yetu bado hovyo hovyo sana.
 
Back
Top Bottom