Ni kwa muda mrefu tumekuwa tukishuhudia watumishi wa Umma au Waliostaafu Utumishi wa Umma wamekuwa wakitangaza nia au kugombea nafasi za kisiasa hasa Ubunge au Urais kupitia CCM, kwani kwa vyama upinzani sio tukio la kawaida.
Lakini kama inavyojulikana, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa pamoja na ya Utumishi wa Umma, Mtumishi wa Umma haruhusiwi kushiriki active politics i.e kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au kugombea nafasi za kisiasa wakati akiwa ni mtumishi wa Umma.
Pamoja na Sheria hizo, hata Katiba ya CCM inatamka bayana kuwa mwanachama atakuwa na sifa na haki ya kugombea uongozi ndani au kupitia CCM iwapo atatimiza miaka mitano (5) tangu awe mwanachama.
Hata hivyo, wafuatao waliwahi kugombea au kutaka kugombea kupitia CCM wakati wakiwa watumishi wa Umma au mara tu baada ya kustaafu utumishi wa Umma na bila ya kutimiza masharti yaliyowekwa na Katiba ya CCM:
1.Andrew Chenge- Alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
2. Alfred Tibaigana- Alikuwa Kamanda Polisi wa Kanda ya Dsm
3.Balozi Ali Karume- Balozi wa Tanzania
4. .......................
5. ......................
Swali. Je ina maana kuwa waliendelea kuwa wanaccm wakiwa watumishi wa Umma.?
Na kama sio hivyo, ni lini walipata sifa ya kugombea kwa mujibu wa Katiba ya CCM ilhali bado au walikuwa hawamaliza miaka 5 tangu wamestaafu utumishi wa umma?