Je, Ruge Mutahaba ni Mtanzania?

Status
Not open for further replies.

Babu Swahili

Member
Jan 8, 2009
41
6
Rege Mutahaba ni mkurugenzi wa Tanzania House of Talents (THT). Hivi karibuni alifanya interview na blog ya Mo.

Nime quote swali na jibu la kwanza kabisa hapo chini. Unaweza kusome interview mzima kupitia: http://www.mohammeddewji.com/blog/2009/12/exclusive-interview-with-ruge-mutahaba.html#comments

SWALI: Ruge mutahaba ni nani?

RUGE: Nimezaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970, Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.

Kwa sababu bwana huyu alizaliwa Marekani, swali moja limeibuka ya kuwa kama yeye ni raia wa Tanzania. Je huyu bwana ni Mmarekani au Mtanzania?

Sheria za uraia za Marekani zinaelezea kuwa mtoto yote atakatezaliwa katika ardhi ya Marekani (ukiondoa wale wanaozaliwa na wazazi walioko ubalozini), wanakuwa raia wa Marekani automatically (unless waukane uraia huo wafikapo miaka 18).

2 Possible sitations za uzaliwaji wa Ruge Marekani:
1) Alizaliwa kutoka kwa mzazi ambaye alikuwa afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani au UN? Kama mmoja wa wazazi wake alikuwa afisa wa ubalozi, basi hakupata uraia wa Marekani. Alichokipata ni chagua la kuchukua haki ya kudumu ya kuishi Marekani (Green Card). Well, huko mbele angeweza kuja kuchukua uraia huo baada ya kukaa na hiyo GC kwa angalau miaka 5.

2) Alizaliwa kutoka kwa wazazi ambao walikwenda kubeba box Marekani. Hivyo huyu jamaa alipata ganda la huko moja kwa moja.

Je kati ya hizo situation 2, ipi ni ya kweli ya huyu bwana?

Kama ni ya 1, na kama hakuja kuchuka uraia wa U.S. huko mbeleni, basi it's all good. Ni mwenzetu.

Kama ni ya 2, je alipofikisha miaka 18, alichagua uraia wa TZ? Kama alibakia na wa U.S., je ana kibali cha kuishi na kufanya kazi Bongo?
 
Mimi sioni cha kujadili hapa...yeye ni mtanzania,amesoma Tz, anajina la kitanzania na anaishi na kufanya kazi Tanzania. Vinginevyo ni majungu tu!!
 
Kwa hiyo kusoma, kuishi, na kufanya kazi Tanzania kunamfanya mtu awe rais wa Tanzania?

Well, inaweza kuwa ni majungu yenye hadhi ya kujunguliwa. Au vipi?
 
Kwani Ruge kaingia kwenye siasa??? Manake haya maswali huwa yanakuja mtu akijitosa kule
 
Baba wa taifa alisema kwamba tukianza kuchunguzana uraia tutakuta wote humu si raia.
kumchunguza mwafrika mwenzako uraia ni kukubaliana na ukoloni mkongwe wa fikra.
 
Rege Mutahaba ni mkurugenzi wa Tanzania House of Talents (THT). Hivi karibuni alifanya interview na blog ya Mo.

Nime quote swali na jibu la kwanza kabisa hapo chini. Unaweza kusome interview mzima kupitia: http://www.mohammeddewji.com/blog/2009/12/exclusive-interview-with-ruge-mutahaba.html#comments

Kwa sababu bwana huyu alizaliwa Marekani, swali moja limeibuka ya kuwa kama yeye ni raia wa Tanzania. Je huyu bwana ni Mmarekani au Mtanzania?

Sheria za uraia za Marekani zinaelezea kuwa mtoto yote atakatezaliwa katika ardhi ya Marekani (ukiondoa wale wanaozaliwa na wazazi walioko ubalozini), wanakuwa raia wa Marekani automatically (unless waukane uraia huo wafikapo miaka 18).

2 Possible sitations za uzaliwaji wa Ruge Marekani:
1) Alizaliwa kutoka kwa mzazi ambaye alikuwa afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani au UN? Kama mmoja wa wazazi wake alikuwa afisa wa ubalozi, basi hakupata uraia wa Marekani. Alichokipata ni chagua la kuchukua haki ya kudumu ya kuishi Marekani (Green Card). Well, huko mbele angeweza kuja kuchukua uraia huo baada ya kukaa na hiyo GC kwa angalau miaka 5.

2) Alizaliwa kutoka kwa wazazi ambao walikwenda kubeba box Marekani. Hivyo huyu jamaa alipata ganda la huko moja kwa moja.

Je kati ya hizo situation 2, ipi ni ya kweli ya huyu bwana?

Kama ni ya 1, na kama hakuja kuchuka uraia wa U.S. huko mbeleni, basi it's all good. Ni mwenzetu.

Kama ni ya 2, je alipofikisha miaka 18, alichagua uraia wa TZ? Kama alibakia na wa U.S., je ana kibali cha kuishi na kufanya kazi Bongo?

Ni Mtanzania
 
Kama ni ya 2, je alipofikisha miaka 18, alichagua uraia wa TZ? Kama alibakia na wa U.S., je ana kibali cha kuishi na kufanya kazi Bongo?[/Qaine....

NI MTANZANIA.......KAMA VP JINYONGE MAZEE.
 
Ni Mtanzania... kwani shida ni kuzaliwa nje ya nchi? That is very narrow minded... JF si sehemu ya kuja kuchafuana. Huyu kijana ni mtanzania na anfanya kazi nzuri sana, tujadili mambo yanayojenga nchi si kusengenya watu....
Ruge hajawahi kugombea kisiasa na ni mfanyabiashara, kama anasafiri kwa paspoti ya kibongo au marekani it is not our business....
 
Yeah, alishakana uraia wa USA, ni mtanzania na pia ana kitambulisho Cha mpipiga Kura Tanzania!
 
Ni Mtanzania
kama alizaliwa USA na kukulia TZ si mtanzania, anapaswa ajiandikishe tena kama raia wa Tanzania. Kwa nijuavyo sheria za uhamiaji anapaswa kuishi Tanzania kwa sasa akitumia passipoti na anatakiwa awe na visa ya kufanyia kazi na kulipa kodi kwa taifa. kama hivi vitu hana basi 'anaishi nchini kinyume cha sheria', ashukuru tu kwani 'sirikali' yetu ndiyo hivyo tena ya 'kidimokrasia'....
 
Siku hizi JF imekuwa kubwa sana kiasi kuwa inabeba mchwa na nguchiro bila mkwaruzo kama alivyo kichuguu.
 
I think ktk dunia ya sasa, hiyo hoja siyo big deal, some of us are 'global citizens'.

Kimsingi mi sioni issue hapo, kwa sababu watanzania wangapi wazalendo tunao lakini kama nchi hatunufaiki nao?? Mfano ni kina Chenge na wengineo!!!

Ni mtizamo tu wanaJF!!!
 
manashindwa kuwajadili wa-asia waliowekeza na kufanya developments huku masaki na osterbay,viwanja wanauziwa bei za kutupwa na wanajiita WAZAWA!mnapoteza time yenu mnamjadili RUGE!siasa bana!

ninyi ndio mliomjadili ULIMWENGU!yaani mkiona mtu anawahatarishia KA-MKATE KENU mnatuma watu jamvini waanze kumchafua!

POLENI VIBARAKA
 
kama alizaliwa USA na kukulia TZ si mtanzania, anapaswa ajiandikishe tena kama raia wa Tanzania. Kwa nijuavyo sheria za uhamiaji anapaswa kuishi Tanzania kwa sasa akitumia passipoti na anatakiwa awe na visa ya kufanyia kazi na kulipa kodi kwa taifa. kama hivi vitu hana basi 'anaishi nchini kinyume cha sheria', ashukuru tu kwani 'sirikali' yetu ndiyo hivyo tena ya 'kidimokrasia'....

You can't be serious aisee..Vipi kama akiukana uraia wa Marekani na kuwa Mtanzania..Ni sheria ya wapi hiyo unaizungumzia mkuu???,halafu mbona unajichanganya?,mara unasema anapaswa ajiandikishe tena kama Raia wa Tanzania halafu unasema anapaswa kuishi akitumia passport na Visa ya kufanyia kazi na kulipa Kodi kwa Taifa..Unamaanisha nini hapa mkuu,kama hutajali nieleweshe tafadhali
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom